Peasant
JF-Expert Member
- Sep 27, 2007
- 3,949
- 687
Hizo source zako hazina tofauti na Tanzania Daima, au Mwanahalisi! Mubarak yuko Misri na atahutubia Taifa usiku huu huenda akaachia madaraka kwa mujibu wa Katibu mkuu wa chama tawala cha Misri! na sasa naangalia live Aljazeera English hakuna hicho unachokipakazia! angalia hapa: Al Jazeera English: Live Stream - Watch Now - Al Jazeera English
Na hii issue haina uhusiano wowote na TZ! sisi tunayo Serikali iliyochaguliwa na Wananchi na sio haki kulinganisha Utawala wa Egypt chini ya Hosni Mubarak alie tawala nchi hiyo miaka zaidi ya 30 sasa!
Sisi katiba yetu hairuhusu Rais kutawala zaidi ya miaka 10! na nchi yetu ni ya vyama vingi sio kama Egypt huko hakuna demokrasia wala uhuru wa vyombo vya habari! TZ uhuru huo upo ndio maana magazeti kama Mwanahalisi yanaweza kumuita Rais Jakaya kuwa ni mwizi na fisadi!
Hivyo msichanganye mambo! h
Kuna tofauti gani kati ya miaka 30 ya utawala wa Mubarak na miaka 50 ya CCM kuwa madarakanio Tanzania?! Mimi sioni tofauti yoyote maana inachokifanya CCM ni kuhakikisha demokrasia ya vyama vingi inakiukwa ili wao wabaki madarakani, tofauti pekee ni kubadilisha sura za watu lakini sio mfumo. Kwangu mimi CCM inapractice mfumo wa kipekee kabisa wa kidikteta ambao lengo kuu ni chama kuhodhi madaraka forever kwa manufaa ya wachache walio madarakan tofauti na classical dictatorship.
Unaposema Tanzania kuna uhuru na demokrasia zaidi ya Egypt unadhihirisha kabisa ni jinsi gani usivyojua nini maana ya uhuru na demokrasia. Matukio mawili ya maandamo yaliyotokea hivi karibuni katika nchi hizi mbili ni kielelezo tosha, tumeona wanajeshi wa Egypt walivyokuwa wanajua nini maana demokrasia tofauti na kule Arusha amabko watu waliuawa kwa risasi za moto kutoka kwa polisi. Usitake kunidanganya kwamba Kikwete anaweza kuruhusu maandamo kama haya ya Egypt yakafanyika na kuonyeshwa kwenye TV ya taifa.