CCN breaking news Mubarak chali jeshi limetwaa hatamu kulinda maslahi ya nchi!
Mubarak aelekea Sharm el sheikh, mji ulio karibu kabisa na mpaka wa Israel na Saudia tayari kwa safari ya lala salama.
Habari za uhakika ni kua jeshi chini ya mkuu wa jeshi Tantawi limechukua nchi. Habari zinaeleza pia Mubarak anataka kuhutubia Taifa kwa njia ya redio kumwachia nchi Suleiman lakini jeshi limekataa. Katika kikao cha supreme Council Mubarak na makamu wake hawakuepo. Tetesi pia zinasema Rais wa muda atakua (jina sikulipata sawa sawa, linaishia Hassan) na makamu wake atakua katibu mkuu wa Arab League Amr Mousa. Brotherhood website wanasema Mubarak ameondoka kabisa Egypt na hotuba inayo daiwa ataitoa ni pre-recorded.
Pasco anaangalia ccn sijui ndio media outlet gani hiyo...Acha uongo. Mmeanza eh?
Hizo source zako hazina tofauti na Tanzania Daima, au Mwanahalisi! Mubarak yuko Misri na atahutubia Taifa usiku huu huenda akaachia madaraka kwa mujibu wa Katibu mkuu wa chama tawala cha Misri! na sasa naangalia live Aljazeera English hakuna hicho unachokipakazia! angalia hapa: Al Jazeera English: Live Stream - Watch Now - Al Jazeera English
Na hii issue haina uhusiano wowote na TZ! sisi tunayo Serikali iliyochaguliwa na Wananchi na sio haki kulinganisha Utawala wa Egypt chini ya Hosni Mubarak alie tawala nchi hiyo miaka zaidi ya 30 sasa!
Sisi katiba yetu hairuhusu Rais kutawala zaidi ya miaka 10! na nchi yetu ni ya vyama vingi sio kama Egypt huko hakuna demokrasia wala uhuru wa vyombo vya habari! TZ uhuru huo upo ndio maana magazeti kama Mwanahalisi yanaweza kumuita Rais Jakaya kuwa ni mwizi na fisadi!
Hivyo msichanganye mambo! h
Mubarak hataki kung'oka madarakani, atangaza kuendelea, jamaa ana roho ya paka (live speach inaendelea)
Mubarak hataki kung'oka madarakani, atangaza kuendelea, jamaa ana roho ya paka (live speach inaendelea)