Soma hizi habari tatu kwa makini, kisha naomba maoni yako:-
"Wabunge wa Chadema walikataa bungeni Pinda asiwe Waziri Mkuu na pia chama hicho hakimtambui Jakaya Kikwete kuwa ni Rais halali wa Tanzania. "
(Source: HABARI LEO HabariLeo | Wabunge Chadema wasusa
"SIKU mbili baada ya Mbunge wa Jimbo la Katavi, Mizengo Pinda, kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete na kupitishwa na Bunge, kushika wadhifa wa uwaziri mkuu, Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei, amepongeza uteuzi huo.."
(Source: MWANANCHI:Muasisi wa Chadema ampongeza Pinda)
"Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameamua kutoka nje ya Bunge mara baada ya Rais wa nchi, Jakaya Kikwete kuanza kuhutubia Bungeni. Wabunge hao wametimiza adhima yao ya kutoka nje ya Bunge kama walivyoahidi hapo mwanzo kwa kile kinachodaiwa kuwa hawamtambui Dkt Kikwete kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." (Source: Global Publishers, BREAKING NEWS: WABUNGE WA CHADEMA WATOKA BUNGENI! - Global Publishers)
Je hii habari ya pili kama ilivyotolewa na gazeti la MWANANCHI ni ya kweli? Na kama ni ya kweli, Je Mzee wetu Edwin Mtei alitamka pongezi hizi kama yeye (at personal level) au kama chama? Na kama alitamka kama chama, je kuna haja ya chama kubatilisha tamko hili?
NB: Ninavyofahamu, Uteuzi wa Waziri Mkuu ni moja ya shughuli ya Raisi. Waziri Mkuu ni Kiongozi Mkuu wa shughuli za serikali bungeni. Kupongeza uteuzi huo ni kumpongeza Raisi kwa kufanya shughuli yake kwa ufanisi. Ukipongeza shughuli za Raisi kwa lugha nyingine ni kusema unamtambua Raisi. Kama nimeelewa tofauti naomba nieleweshwe tafadhali.