Muasisi wa CCJ kugombea makamu mwenyekiti UvCCM!

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Muasisi wa CCJ Paul Makonda amechukua form ya kugombea makamu mwenyekiti UVCCM taifa.

Paul Makonda founder wa chama kisicho na usajili wa kudumu amekabidhiwa form leo saa 5 asubuhi na katibu mkuu wa UVCCM Taifa Martin Shigela.

Paul Makonda ameshindwa kujibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari aliyetaka kujua kama ameshakana u-CCJ ama bado anashikilia kuwatumikia mabwana wawili CCM na CCJ.

Makonda pia aliwashangaza watumishi wa UVCCM makao makuu kwa kujaza HAPANA kipengele kinachouliza, Je? umewahi kujiunga na chama cha upinzani? Badala ya makonda kujaza NDIYO yeye amejaza HAPANA.
 
Paul Makonda si alishawahi kufukuzwa huko kilimanjaro? Ashamliza shule Ushirica Muccobs?
 
Inaelekea na wewe ni mgombea,umejipima ukaona kuwa anakufunika ukaona uanze kutafuta vikashfa vya kuunga unga.hayo hayatuhusu hapa jf.
 
Hata hao kina slaa,shibuda,maalim seif,kafulila wamehama vyama mpaka wamechoka lakini bado wapo juu,kwa hiyo na wewe kama ulikuwa umejiandaa na hilo kama kashfa,umeshindwa.makonda tunamjua,ni jembe.
 
Dahhhh.. Siasa bwna haina tofauti na kuwa mchawi... Watu wanakuwa waongo waongo tuuuu, wanayosema sio wanayoyaamini.. wanadanganya hadi wazazi wao kipindi cha kampeni kwa ahadi ambazo hawatekelezi yani vurugu tupu.

BETA TO BE LOW PROFILE
 
Naomba nimulize aliyeleta thread hii kama anajua anachokiongea na wakati tulionao kwa sasa kwanza si rahisi kutokuamini kuwa wewe si mwama CCM, lakini jambo la msingi kwa sisi tunaombea ukuaji wa demokrasia nchini ni kwamba tasisi zinazobeba hatima ya demokrasia nchini ikiwemo zile za vyama vya siasa lazima zilenge kuwapata vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwa umakini wa hali ya juu na kwa manufaa ya watanzania, ungekuwa makini endapo ungetuambia ni kwa nini Makonda asichanguliwe kwenye kiti hicho alichokiomba kwa kuhusianisha utendaji kazi wake katika ngazi mbalimbali ndani na nje ya C.CM.

Kwetu sisi watanzania hatuoni tatizo la ujio wa CCJ kama unavyofikria,bali tunaimani na wale wote waliokuwa kwenye huo mchakato wa kuendelea kuimalisha demokrasia nchini,lakini kumbuka kuwa UVCCM kwa sasa inahitaji vijana makini watakaoweza kujadiliana na kushindana na vijana wa upinzani kwa hoja na si kwa propaganda zisizokuwa na tija kwa wananchi vinginevyo UVCCM hataweza kuwavutia vijana kujiunga na CCM.
 
hivi wale waasisi vigogo mbona mmewasahau? sasa hivi wanakula bata... wanasubiri uchaguzi mkuu 2015 mtandao ufufuke. ccm poleni.
 
Huyu kamanda mm namkubali sana,coz najua historia yake alikotoka alikuwa jirani yangu pale Mwanza, jamaa tuweke mbali u si si em,huyu kamanda ni mchapa kazi na ni mtaji mzuri kwa CCM kama watamtumia vizuri..ata Nape hamwezi huyu kamanda kwa uchapa kazi.
 
Muasisi wa CCJ Paul Makonda amechukua form ya kugombea makamu mwenyekiti UVCCM taifa.

Paul Makonda founder wa chama kisicho na usajili wa kudumu amekabidhiwa form leo saa 5 asubuhi na katibu mkuu wa UVCCM Taifa Martin Shigela.

Paul Makonda ameshindwa kujibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari aliyetaka kujua kama ameshakana u-CCJ ama bado anashikilia kuwatumikia mabwana wawili CCM na CCJ.

Makonda pia aliwashangaza watumishi wa UVCCM makao makuu kwa kujaza HAPANA kipengele kinachouliza, Je? umewahi kujiunga na chama cha upinzani? Badala ya makonda kujaza NDIYO yeye amejaza HAPANA.

Hoja yako ni dhaifu kupita kiasi. Kwani kuwahi kuwa mwanachama wa chama kinachotambulika na kilichoundwa kwa mujibu wa sheria za nchi na baadae kuondoka kuna shida gani? CCJ halikuwa kundi haramu la kigaidi na watu kuhama vyama ni kitu cha kawaida sana katika maisha ya siasa.

Wassira, Bagenda, Nsazugwanko, marehemu Fundikira, Adam Malima na hata Ngeleja kwa nyakati tofauti walikuwa ni wanachama wa vyama vya upinzani na baadae wakarejea CCM na kupewa nyadhifa mbalimbali za kiuongozi na hawakuonekana wahaini au wasaliti.

Hii ni cheap politics ambayo haiwezi kupata manunuzi popote pale! Makonda na wengine watakaothibitisha uadilifu wao na wakawa wanachama wa CCM wana haki ya kugombea uongozi kwenye chama.

By the way, kama kweli alihama kwa nini UVCCM hawakumfuta kwenye orodha yao ya uanachama and I believe Shigelah anafahamu kwamba Makonda ni mwanachama wa jumuiya yake na ndiyo sababu akampa fomu ya kugombea.
 
Issue ni kuwa alikataa hadharani kuwa hajawahi.
 
Back
Top Bottom