Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba

Habar ndugu zang. Ninaomba ushauri kwa wenye kujua suluhisho la kuwashwa mwili baada ya kuoga. Najarbu kutumia sabun za aina mbalimbal lakini tatzo bado liko vilevile.

Please wana JF naitaji msaada wenu kwa wenye kujua.
 
Habar ndugu zang. Ninaomba uxhaur kwa wenye kujua xuruixho la kuwaxhwa mwili baada ya kuoga. Najarbu kutumia xabun za aina mbalimbal lakin
tatzo bado liko vlevle.

Please wana JF naitaji mxaada wenu kwa wenye kujua.

Ukimaliza kuoga hakikisha unajikausha mara unapomaliza na hakikisha taulo kavu, usijikaushe na taulo bichi bichi, bacteria huwa wanapenda kukaa kwenye ubichi ubichi. Anika taulo lako juani au sehemu ambayo haiweki unyevu.

Kingine hakikisha umekauka vizuri ndio uvae nguo, na nguo hiyo iwe kavu... Usipake mafuta ya mgando kama una tatizo la kuwashwa, tumia mafuta ya maji maji ama lotion..
Hope nimekusaidia..
 
Pole mkuu, kwa hio sasa hv huogi?!
Km upo DSM, nenda pale posta duka la S.H Amons andaa sh 2,500 tsh nunua sabuni iitwayo protex oak!

Sina uhakika na hili neno oak, lkn ni neno km hili!

Box yake nyeupe, tatizo lako litapungua kwa 98%+

Pole sana!
 
Kuna baadhi ya watu huwa wana allergy na maji inawezekana na we ni mmoja kati yao. Km tatizo ni kubwa sana jaribu kuwaona Madaktari wa ngozi watakusaidia.
 
Mkuu,ni dawa ya minyoo wa aina ipi na taja dawa aina yake kama siyo ni tatizo la ngozi?
 
Hata mimi tatizo huwa linanisumbua, mara nyingi huwa naoga maji ya moto ili kupunguza tatizo.

Mara nyingi hutokea kukiwa na baridi au nikioga maji ya baridi. Siku za karibuni huwa naoga maji ya baridi iwe asubuhi au usiku lakini siwashwi.
 
It seems una alergy na some spices, hiyo hali ikikujia tumia vidonge vinaitwa claritine vitakusaidia, pia fanya uchunguzi wa vyakula unavyokula vimepikiwa na viungio gani.
 
Ndugu zangu huu ni mwaka wa 10 tangu tatizo la kuwashwa kila nikioga linianze nishazunguuka mpaka sasa nimechoka yoyote anae weza kunisaidia jinsi ya kupona naomba anisaidie
 
Pole Sana! Mie tatizo hilo linanikuta hasa nikioga maji ya baridi. Nafuu yangu ninapooga maji ya moto.

Kushindana na hali hiyo mara baada ya kuoga huwa navaa jacket zito ili mwili kupata joto haraka.

Hospitali zote nilizopita sijapata majibu ya kutatua tatizo wala kuweka hapa. Narudia kukupa pole maana shida hiyo ninaiishi.
 
Kumbe tuko wengi mimi nikoga maji baridi nawashwa sana ila maji moto aaahh napeta tu hujasema waoga maji gani
 
Minyoo imewasumbua watu wengi na kuwa na dalili kama hizo, kwa kuwa umepita hospitali nyingi pengine hili sio tatizo lako (itakuwa ulishapewa dawa ama angalau kupimwa na haikuonekana hiyo minyoo)

Usikate tamaa dunia ina miti mingi, naamini hujakutana na mti wa dawa yako (dawa zatokana na miti)
 
Mkuu hiyo itakuwa ni Water allergy au Aquagenic urticaria. Ni allergy dhidi ya maji ya moto au baridi au yenye chlorine au yasiyowekwa chlorine. Ni kitu kinachotokea watu wachache sana. Tiba yake inaweza ikawa ni supportive zaidi, kama:

1. Ikiwa chanzo chake ni maji ya moto basi oga ya baridi, kama ya baridi tumia maji ya moto na kama shida ni chlorine inayowekwa kwenye maji basi huwa kuna shower gel ya kuondoa chlorine mwisho wa kuoga au utafute purifier ambayo itatoa chlorine. Hapo kwenye chlorine ni issue kubwa.

2. Ikiwa unapata allegy ukigusa tu maji, basi waweza tumia oily cream au gel kupaka mwilini kabla ya kuoga au kuogelea. Hupunguza muwasho kiasi kikubwa.

3. Epuka kukaa muda mrefu ndani ya maji.

4. Nguo za pamba na linen husaidia kupunguza dalili. Tumia taulo lenye pamba asilimia 100.

5. Epuka kutumia vyakula vyenye viungo vingi na vyakula vinavyokaangwa. Pia epuka kunywa pombe na kahawa, maana vitu hivyo vitaongeza tatizo.

6. Muone daktari wa magonjwa ya ngozi.
 
Wagonjwa wenzangu nashauri mwende hospitali kufanya vipimo fasaha ili mjue tatizo ni nini, ila Mimi niko hivyo nikioga maji baridi tu chamoto takiona baada ya masaa najikuna saaaana hadi navimba na kuacha mabaka hivyo nilifatilia tiba kwa sana nikagundulika nina ugonjwa wa asthma ya ngozi.

Hivyo natumia dawa za Asthma za vidonge na kufata masharti na same times naonja onja kuoga ya baridi haswa kipindi hiki cha joto kwa kweli nafuu ipo na kuwa cwashwi! Hivyo nawashauri mkatibiwe!
 
Back
Top Bottom