Muarobaini wa Hospitali kuu ya Taifa, Muhimbili

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,195
1,417
Habari za jioni GT's, amani iwe nanyi.

Leo Tumeona Mhe. Rais akitembelea Hosp ya Taifa Muhimbili na kujionea wodi ya wazazi wakiwa wamelala chini.

Yafuatayo ni maoni yangu nini kifanyike kutatua matatizo haya ya Muhimbili.

1. Wagonjwa wanaotakiwa kulaza Muhimbili wawe ni referral case tu. Case Kama kujifungua mtu hana madhara basi aende Hosp za wilaya.

2. Kutokana na wingi huo wa wagonjwa na madaktari na manesi kidogo basi ni dhahiri mzigo unaopigwa Muhimbili sio wakawaida.

3. Muhimbili na MUHAS inahitaji kuajiri vijana wengi wenye nguvu na kasi ya hapa kazi tu!! Muhimbili imejaza wazee kila kona na hawataki kuajiri, hili ni tatizo kubwa. Wengine wanakimbilia miaka 80 sasa, hivi Muhimbili hakuna succession plan??? Hii inavunja moyo vijana. Na hawa vigogo ni mbogo hawataki new blood ziajiriwe kabisa. Wako buzy kupeana promotion even at above retirement age. Pia wana mtandao wao wakupeana vyeo kulinda retires. Hivi inakuwaje vyeo vya juu karibu vyote vishikwe na retirees. Hata pale anapotokea mwenye uwezo na elimu na uzoefu sawa na huyo retirees bado huyo retiree anakuwa ni chaguo lao. Ubinafsi Wa namna hii unaipeleka wapi sekta ya Afya???

Kama mtu ana miaka 75 sasa hebu jiulize tangu amestaafu akiwa na miaka 60, je ameshindwa kumuandaa mtu Wa kurithi hiyo nafasi yake??? Hii ni dalili hawa Ma prof ni wabinafsi Wa kufa mtu, na ndio wanaoua Muhimbili. Kila new blood wakija na new ideas HAWATAKI!!!

4. Muhimbili inahitaji kuajiri CEO mwenye background ya MBA au nyingine tofauti na medicine. Hawa Ma doctor na Ma professa wabaki wakitumikia profession yao. Wawaachie wengi mambo ya uongozi.

5. Hospitali za wilaya nchi nzima ziboreshwe mtu asione haja ya kwenda Muhimbili kwa case ndogo ndogo.

6. Kuna vijana kibao wamemaliza medicine na speciality wanao uwezo Wa kufanya hizo kazi usiku na mchana. Na NIA ya dhati na kweli wanayo. Serikali itoe ajira za kutosha kwa manesi na madaktari. Ukimuondoa Profesa mmoja aliyestaafu anayelipwa kiinua mgongo kila miaka miwili, mshahara na pensheni, hapo unaajira madaktari tena wenye speciality watatu.

7. Muhimbili ianzishe mradi Wa KULIPIA shs 200 kwa saa kwa kila Gari inayoingia. Pesa zitumike kuboresha wodi za wamama na watoto. Pia vile vitegauchumi vyote vilivyoko Muhimbili vipitiwe upya. Pia waangalie new income generating projects.

8. Mashirika yote ya umma yana fungu la "Corporate Social Responsibility" pesa hizi ambazo minimum ni shs milioni 100 kwa kila CEO kwa mwaka zitumike kwenye huduma za jamii hasa wanawake na watoto na madawati kwenye shule zenye uhitaji. Mambo ya kupeleka misaada shule za Academy kwa kweli haileti maana na kuna watoto wanakaa chini. Huko Academy wana kila kitu. Pia mchango Wa NHIF kwenye sekta ya Afya Iangaliwe upya!!! Mbona makusanyo ni makubwa nini kinaendelea??

9. Muhimbili inahitaji kufanyiwa thorough auditing. Pesa zinazoingizwa kila siku ni ngapi na ngapi zinaenda hazina nk. Pia kuna watoa huduma mbali mbali (service provider) wametoa mabei makubwa mno ya huduma wanazotoa. Hili ni jipu.

10. Muhimbili inahitaji system nzuri ya ku monitor mapato, natamani wajifunze huku private Hosp Kama Agakhan, Regency, Kairuki, TMJ nk huko makusanyo yako wazi na system iko wazi hata kubaini kwa siku wamehudumia wagonjwa wangapi kila idara.

Hapa unahitaji kupeleka barua vyuo vikuu kuna vijana wa IT na computer science wako vizuri up stairs. Wapewe terms of reference watengeneze system inayo suite needs ya hospital yetu. Washindi kumi wachukuliwe kuanzia yule Wa kwanza. Haitagharimu hata mil 50 na ina advantage kuwa ni In-house na customary based. Hao vijana 10 waajiriwe hapo Muhimbili na project iko take off waendeleze kwenye hospital zote za Serikali. Itaokoa mapato na itaboresha huduma. Na vijana wetu watapata ajira.

11. Maslahi ya watoa huduma za Afya yaboreshwe.

12. Mapato na matumizi - Budget ya Muhimbili iwekwe wazi na ijadiliwe kwa UZALENDO.

13. Mashine ziongezwe tena za kisasa zikiwemo theatres kupunguza foleni kubwa za wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji. Hii ni chanzo cha rushwa wakati mwingine.

14. .. (Ongezea hapo TUSAIDIE Muhimbili ambako sasa ni India ya TZ) uzalendo utumike zaidi maana hatujui nani kesho ataenda kulala pale.

Queen Esther
 
Kuajiri?
muhimbili ijipanue zaidi?
mnazidisha tatizo

Muhimbili ingewekwa tu limit ya madaktari kufanya kazi pale
karibu kila daktari bingwa yuko pale kwa kung'ang'ania kuishi Dar
wakihamishwa wanafuta excuse wanarudi

kwa ufupi serikali iache kuajiri kitaifa
iajiri kimkoa..sio madaktari tu hadi walimu na watumishi wengine

hao madaktari vijana wakaajiriwe hospitali za mikoa
na hivyo weatazuia wagonjwa wa mikoani kuja Dar kufuata madaktari bingwa
na hivyo kuzidisha watu pale

Serikali ijifunze ku decentralize na ndo maana tunarudi kwa katiba mpya

hadi formation za tawala za mikoa na taasisi iundwe upya....

madaktari wote wanataka kufanya kazi Dar
na walimupia....mwisho Dar ndo kama Tanzania
kila taasisi inajipanua
mara upanuzi wa muhimbili
mara bandari mara airport mradi kuongeza foleni tu
 
Hapo namba nne sidhan kama inatekelezeka,achen wajiendeshe wenyewe.MBA iongoze medicine naona kama hakutakua na maelewano
 
Ngoja wataalamu waje wakuwekee taarifa ya kila daktari anatakiwa kuhudumia wagonjwa wangapi ndio utajua kuna uhaba Wa Ma daktari au la!!!

Queen Esther

Kuajiri?
muhimbili ijipanue zaidi?
mnazidisha tatizo

Muhimbili ingewekwa tu limit ya madaktari kufanya kazi pale
karibu kila daktari bingwa yuko pale kwa kung'ang'ania kuishi Dar
wakihamishwa wanafuta excuse wanarudi

kwa ufupi serikali iache kuajiri kitaifa
iajiri kimkoa..sio madaktari tu hadi walimu na watumishi wengine

hao madaktari vijana wakaajiriwe hospitali za mikoa
na hivyo weatazuia wagonjwa wa mikoani kuja Dar kufuata madaktari bingwa
na hivyo kuzidisha watu pale

Serikali ijifunze ku decentralize na ndo maana tunarudi kwa katiba mpya

hadi formation za tawala za mikoa na taasisi iundwe upya....

madaktari wote wanataka kufanya kazi Dar
na walimupia....mwisho Dar ndo kama Tanzania
kila taasisi inajipanua
mara upanuzi wa muhimbili
mara bandari mara airport mradi kuongeza foleni tu
 
Kuajiri?
muhimbili ijipanue zaidi?
mnazidisha tatizo

Muhimbili ingewekwa tu limit ya madaktari kufanya kazi pale
karibu kila daktari bingwa yuko pale kwa kung'ang'ania kuishi Dar
wakihamishwa wanafuta excuse wanarudi

kwa ufupi serikali iache kuajiri kitaifa
iajiri kimkoa..sio madaktari tu hadi walimu na watumishi wengine

hao madaktari vijana wakaajiriwe hospitali za mikoa
na hivyo weatazuia wagonjwa wa mikoani kuja Dar kufuata madaktari bingwa
na hivyo kuzidisha watu pale

Serikali ijifunze ku decentralize na ndo maana tunarudi kwa katiba mpya

hadi formation za tawala za mikoa na taasisi iundwe upya....

madaktari wote wanataka kufanya kazi Dar
na walimupia....mwisho Dar ndo kama Tanzania
kila taasisi inajipanua
mara upanuzi wa muhimbili
mara bandari mara airport mradi kuongeza foleni tu

I salute you the Boss. nakubaliana nawe kuhusu suali la decentralization of power kwa serikali. Infact Dar is over crowded! Wahamishe hata makao makuu wapeleke Dodoma. sio kila kitu Dar! jamani watukumbuke hata sisi wengine tunaokula viwavi jeshi!
 
Ni kweli lakini hao Leo waliokuwa wamelala chini ni wamama wanaosubiri kujifungua. Je wapelekwe Dodoma?? Rate ya KUZAA (Birth Rate) TZ iko juu sana kila mkoa my dear. Nchi zilizoendelea zimepunguza kuzaa ndio maana wewe ukishika tu mimba unaanza kulipwa. Huku kwenye nchi zinazoendelea kila mtoto anakuja na RIZKI Yake.

Queen hio issue ya birth control ni suala zima la elimu ya kinga ya afya. Tatizo ni kwamba mfumo wetu wa afya bado umejikita zaidi kwenye tiba kuliko kinga! Hili lilipaswa lijadiliwe kwenye mitaala yetu ya Elimu tangu grassroot level na sio kuanza kuwalaumu wazazi! na ndio maana tunasema elimu , elimu, elimu. Hapa nina suali la uzushi kwako hivi ni mara ngapi kwa mwaka wewe mwenyewe unamuona dentist? ama unasubiri jino linauma ndio unakwenda kumuona daktari?
 
Wameshindwa kutatua matatizo gani??? Natamani Mungu akurushie ka ugonjwa hata kadogo ukaone Kama huduma zimebadilika ktk nchi yetu tangu Dr. JPM ameingia madarakani au la!!!!

Ukitoka huko utakuja na critical evidence. Ile ya Mhe. Sumaye na wengine naona haijakutosha.

Queen Esther

Sasa kama matatizo ya hospitali moja wanashindwa kutatua watawezaje kuboresha huduma za afya nchi nzima? Kwa ziara za kushtukiza?
 
Daktari na daktari bingwa ni tofauti
madaktari bingwa asilimia 70 au zaidi wako Muhimbili

Boss mi nakubali huku nakataa...

Nakubali kwamba watawanywe hao madactari bingwa lakini kumbuka mfano vifaa operation kubwa kubwa kama vile vinavyopatika MOI au Taasisi ya Moyo ya JK huko mikoani bado sana ama hakuna kabisa,,, je unataka orthopedist akatibu malaria?! Yaani mtu kakaa zaidi ya 10 years shule aende akatibu malaria tu?!

Trust me .. Muhimbili hao ma specialist hawatoshi na waliokuwepo hawakidhi idadi ya wagonjwa...

Nlikuwepo pale na nimejionea..

Pili., suala la kuwapeleka ma dr mikoani well hapa lina kuja swala la maslahi.. Ma dr wenyewe wanaita vijiwe! Kumbuka wakati wao wapo shule kuna wenzao walisoma miaka mitatu na kupata degree na kuanza maisha , trust me kwa junior Dr yeyote hilo ndilo analowaza ndio maana inakuwa ngumu sana kukubali kwenda vijijini au mikoani asubiri mshahara wa laki nane kwa mwezi wakati dar anaweza akawa na kijiwe aka make x 2 ya hapo..

All in all ni maslahi zaidi, wakiboreshewa maslahi na mazingira ya kazi watakwenda huko mikoani
 
Habari za jioni GT's, amani iwe nanyi.

Leo Tumeona Mhe. Rais akitembelea Hosp ya Taifa Muhimbili na kujionea wodi ya wazazi wakiwa wamelala chini.

Yafuatayo ni maoni yangu nini kifanyike kutatua matatizo haya ya Muhimbili.

1. Wagonjwa wanaotakiwa kulaza Muhimbili wawe ni referral case tu. Case Kama kujifungua mtu hana madhara basi aende Hosp za wilaya.

2. Kutokana na wingi huo wa wagonjwa na madaktari na manesi kidogo basi ni dhahiri mzigo unaopigwa Muhimbili sio wakawaida.

3. Muhimbili inahitaji kuajiri vijana wengi wenye nguvu na kasi ya hapa kazi tu!! Muhimbili imejaza wazee kila kona na hawataki kuajiri, hili ni tatizo kubwa. Wengine wanakimbilia miaka 80 sasa, hivi Muhimbili hakuna succession plan??? Hii inavunja moyo vijana. Na hawa vigogo ni mbogo hawataki new blood ziajiriwe kabisa.
Kama mtu ana miaka 75 sasa hebu jiulize tangu amestaafu akiwa na miaka 60, je ameshindwa kumuandaa mtu Wa kurithi hiyo nafasi yake??? Hii ni dalili hawa Ma prof ni wabi nafsi Wa kufa mtu, na ndio wanaoua Muhimbili. Kila new blood wakija na new ideas HAWATAKI!!!

4. Muhimbili inahitaji kuajiri CEO mwenye background ya MBA au nyingine tofauti na medicine. Hawa Ma doctor na Ma professa wabaki wakitumikia profession yao. Wawaachie wengi mambo ya uongozi.

5. Hospitali za wilaya nchi nzima ziboreshwe mtu asione haja ya kwenda Muhimbili kwa case ndogo ndogo.

6. Kuna vijana kibao wamezaliwa medicine wanao uwezo Wa kufanya hizo kazi usiku na mchana. Na NIA ya dhati na kweli wanayo. Serikali itoe ajira za kutosha kwa manesi na madaktari. Ukimuondoa Profesa mmoja aliyestaafu anayelipwa kiinua mgongo kila miaka miwili, mshahara na pensheni, hapo unaajira madaktari tena wenye speciality watatu.

7. Muhimbili ianzishe mradi Wa KULIPIA shs 200 kwa saa kwa kila Gari inayoingia. Pesa zitumike kuboresha wodi za wamama na watoto. Pia vile vitegauchumi vyote vilivyoko Muhimbili vipitiwe upya. Pia waangalie new income generating projects.

8. Mashirika yote ya umma yana fungu la "Corporate Social Responsibility" pesa hizi ambazo minimum ni shs milioni 100 kwa kila CEO kwa mwaka zitumike kwenye huduma za jamii hasa wanawake na watoto na madawati kwenye shule zenye uhitaji. Mambo ya kupeleka misaada shule za Academy kwa kweli haileti maana na kuna watoto wanakaa chini. Huko Academy wana kila kitu. Pia mchango Wa NHIF kwenye sekta ya Afya Iangaliwe upya!!! Mbona makusanyo ni makubwa nini kinaendelea??

9. Muhimbili inahitaji kufanyiwa thorough auditing. Pesa zinazoingizwa kila siku ni ngapi na ngapi zinaenda hazina nk. Pia kuna watoa huduma mbali mbali (service provider) wametoa mabei makubwa mno ya huduma wanazotoa. Hili ni jipu.

10. Muhimbili inahitaji system nzuri ya ku monitor mapato, natamani wajifunze huku private Hosp Kama Agakhan, Regency, Kairuki, TMJ nk huko makusanyo yako wazi na system iko wazi hata kubaini kwa siku wamehudumia wagonjwa wangapi kila idara.

11. Maslahi ya watoa huduma za Afya yaboreshwe.

12. Mapato na matumizi - Budget ya Muhimbili iwekwe wazi na ijadiliwe kwa UZALENDO.

13. Mashine ziongezwe tena za kisasa zikiwemo theatres kupunguza foleni kubwa za wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji. Hii ni chanzo cha rushwa wakati mwingine.

14. .. (Ongezea hapo TUSAIDIE Muhimbili ambako sasa ni India ya TZ) uzalendo utumike zaidi maana hatujui nani kesho ataenda kulala pale.

Queen Esther
Ninapoingia jukwaa husika,mathalan jukwaa la siasa kabla sijafungua bandiko lolote huwa napitia roughly majina ya watuma post,kuna baadhi ya majina ninapoyaona huwa nalifungua bandiko kwa kuwa nna imani na mtuma bandiko na moja ya majina hayo ni lako Queen Esther,tazama post hii ilivyoshiba points.Naendelea kufikiria cha kuongeza lakini point ya kwanza mpaka ya kumi na nne hapo juu wazifanyie kazi.
 
Asante mpendwa.

Mungu akubariki kwa such a compliment.

Queen Esther

Ninapoingia jukwaa husika,mathalan jukwaa la siasa kabla sijafungua bandiko lolote huwa napitia roughly majina ya watuma post,kuna baadhi ya majina ninapoyaona huwa nalifungua bandiko kwa kuwa nna imani na mtuma bandiko na moja ya majina hayo ni lako Queen Esther,tazama post hii ilivyoshiba points.Naendelea kufikiria cha kuongeza lakini point ya kwanza mpaka ya kumi na nne hapo juu wazifanyie kazi.
 
Wameshindwa kutatua matatizo gani??? Natamani Mungu akurushie ka ugonjwa hata kadogo ukaone Kama huduma zimebadilika ktk nchi yetu tangu Dr. JPM ameingia madarakani au la!!!!
...Queen, hii inapishana na thread post yako hapo juu.

...Anyways, kazi ya kuboresha sekta ya afya hapa ni kubwa. Tuwe wavumilivu.
 
Kutatua matatizo au changamoto ni mchakato. Sitegemei yaishe over night. Ni kweli WOTE tuwe WAZALENDO na wavumilivu bila kupenda kurusha lawama hata ktk mambo yanayohitaji kwenda level nyingine Unakuta mtu anataka kuturudisha back to square one kanakwamba hakuna kilichofanyika.

Mnyonge mnyongeni haki Yake mpeni.

...Kuwa wavumilivu ni pamoja na kutokutoa sifa au kuponda prematurely!

...My main point here is, kuna kazi kubwa sana huko mbele, inayohitaji fedha na usimamizi wa rasilimali, kama tunataka kufanikiwa katika maboresho ya sekta hii. Kazi hii inahitaji muda, tuwe na subra! Tuache ku speculate!
 
Umeongea neno la Hekima sana sana jamani. Ungeuliza ushauri wangu hata Dr. Kidantu yule Ag. DG aliyetolewa Muhimbili alikuwa victim of circumstance.

Asante kwa kusimamia kweli na UZALENDO. Ni wakati Wa kuweka mambo ya vyama pembeni sasa na tujikite kuishauri Serikali objectively sio kuponda kila kitu.

HOSPITALI sote tutaenda kutibiwa na ndg zetu na wake au waume na watoto wetu. The same to ELIMU.

Tuache sasa ushabiki wa siasa unatosha, pia tuachane na wana siasa ambao kwa maslahi yao binafsi hawataki kuona tunapiga hatua. Tunaoumizwa na wana siasa ni sisi na watoto na ndg zetu. Wote tulitamani mabadiliko, basi tupambane objectively kuona mabadiliko ya kweli na kwa vizazi vyetu yanakuja.

Yale mambo ya kutetea kwasababu ni ndg yako ameguswa basi unaongea la kuongea nayo sio mazuri. Kama ni jipu bila kuangalia chama, itikadi au undugu basi wote tuwe na lugha moja. Pia Kama mtu ameonewa time will tell na anaporudishwa basi Tunamshukuru Mungu. Pia naamini kuna washauri wabaya wapo huko juu. Mhe. Rais inabidi asaidiane na TISS wachuje washauri.

Tanzania ni nchi yetu hatuwezi kuikimbia, ni wajibu wetu kumsaidia Mhe. Rais a baraza zima kuijenga TZ.

Usiku mwema.

Back
Top Bottom