Muandaaji wa Mashindano ya Miss Utalii 2011 ataweza kutoa zawadi alizohaidi ?

Kudadadeki

Member
Oct 7, 2010
70
3
Muandaaji wa Miss. Utalii 2011 ni Ndugu Chipungahelo.

Huyu jamaa hana historia nzuri katika uandaaji wa mashindano na concert mbali mbali. Mnaokumbuka, ameshawatapeli wasanii chungu nzima.

Kwa mfano muulize Nyota Ndogo wa Kenya "ni Promoter gani wa Ki TZ unayemkumbuka sana ?"- atakujibu "Chipungahelo". Jamaa alimfanyisha kazi kwenye matamasha kibao across Tanzania kisha akaingia mitini. Ilibidi Nyota Ndogo atumiwe nauli toka Nairobi.

Sasa, ameandaa Miss Utalii, Mshindi wa Kwanza 150m...... Ataweza kutimiza ahadi ? Yangu macho.

Ameingia ubia na Star TV kuonyesha shindano hilo live next weekend pale Kiromo Hotel, Bagamoyo. SUBIRINI MTAONA VITUKO VYA KUFUNGUA MWAKA....
 
Huyu jamaa nishawahi kusikia mambo yake.... kuna mwaka mmoja nadhani 06 aliandaa hilohilo shindano na kukawa na minong'ono kutoka kwa washiriki kuwa alikuwa anawachakachua.... na vilevile kambi ilikuwa nyumbani kwake mbezi!!!! Lakini tusubiri tuone litakalojiri!!!

:msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela:
 
jamaa ni muandaaji kituko kwa kweli haaminiki kabisa,nishaona akiwalisha chipsi kuku na soda warembo wake pale cine club miaka ya nyuma 2002 hivi kama sikosei,bili ilipoletwa kulipa ilikua kazi ngumu sana aiseee.ngoja uone viroja kwenye hayo mashindano tena.
 
Back
Top Bottom