Mualiko wa kikao cha wana jumuiya ya london

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
As received:

MUALIKO WA KIKAO CHA WANA JUMUIYA YA - LONDON

Uongozi wa muda wa Jumuiya ya Watanzania - London umekamilisha kazi mliyotupa ya kutengeneza mfumo mpya wa kiuendeshaji pamoja na kuitisha uchaguzi wa viongozi. Sasa tuko tayari kuwakilisha taarifa hii kwenu Wanajumuiya.

Shughuli hii itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 14 May 2010 kuanzia saa 11 jioni. Uchaguzi wa viongozi wa kudumu utafanyika tarehe 5 June 2010 na ili kufanikisha hayo kikao hiki ni muhimu sana hivyo tunaomba ushirikiano wenu, mhudhurie na kutupa mawazo pale inapohitajika.

AGENDA ZA KIKAO:
-- MFUMO: mfumo mpya wa kiutendaji
-- KATIBA: kuichambua katiba yetu
-- UCHAGUZI: kupata wagombea na upigaji kura.
-- KUSIMIKWA: maandalizi ya kusimika viongozi wapya
-- BALOZI: kuhusu wanajumuiya kumuaga balozi na kuwasimika viongozi
-- ADA : ada za uanachama, kiasi cha kulipa na jinsi ya kulipa
-- Mengineyo

Fika mapema, sote tutakuwa pale tayari kayapitia hayo yote.

- Kikao: kikao cha wanajumuiya
- Waalikwa: Watanzania London

- Mahali:
TANZANIA HIGH COMMISSION,
3 Stratford Place
W1C 1AS,
London .

Muda: Saa 11 jioni

N.B:
Iweke tarehe 5 June 2010 kwenye ratiba yako, inaandaliwa party safi .
 
Back
Top Bottom