MUAFAKA: Kusuasua na Ufafanuzi wa Kikwete - Je, Yote ni Msukumo Kutoka Nje?

PEMBA IJITENGE
CCM hawako serious waseme kabisa hakuna muhafaka mpaka baada ya uchaguzi wa 2010 kwani karume alishasema alishinda kihalali na hana mpango wa kugawana madaraka na mtu yeyote, kuwa wakweli kutawafanya CUF wajue wanafanya nini badala ya kuwambia kuwa watapewa nafasi za uwaziri wakati si kweli.

Majadiliano yasimamiwe na raisi mwenyewe kuonyesha kuwa yuko committed.

Mimi naona mambo ya muafaka yashashindikana. Sidhani kama kuna wakati ambapo CCM watakubali kushindwa kwenye uchaguzi wowote Zanzibar katika ngazi ya Rais, mpaka pale watakaposhindwa kwenye uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya muungano. Kitu ambacho kutokea siku za karibuni ni ndoto. Ni vigumu sana sehemu ya nchi kuendelea iwapo wananchi hawautaki uongozi uliopo, na kimsingi CCM wapo Pemba kimabavu (kama Bush Irak). Sasa natamka rasmi kwamba endapo CCM hawataki serikali ya mseto Zanzibar basi ni bora Pemba ijitenge. Haina maana, tena ni upimbavu kulazimisha utawala katika karne hii. tujifunze kwa yaliyotokea sehemu mbalimbali za dunia kwenye hii miungano feki, iko wapi USSR, Yugoslavia, na nyinginezo? Maana ya kuwa na muungano ni kujenga nguvu ya kiuchumi pamoja na mambo mengine, kunatengenezwa nini Zanzibar kwenye umoja huo unaolazimishwa kama siyo chuki tu kwenye vizazi vinavyokuja? Madhara ya chuki inayopandwa na CCM kati ya Waunguja na Wapemba itakujaonekana wakati akina kikwete na akina Karume hawapo tena duniani, ni itakuwa mbaya kuliko hata ya Wayahudi na Wapelestina huko mashariki gani sijui!
Kwa hali ilivyo sasa nadhani Pemba ingepata maendeleo ya haraka kama ingekuwa ni nchi inayojitegemea kuliko kuwa part ya Zanzibar. Kila siku muafaka muafaka, tumeshachoka sasa, kwanza muafaka gani huo usiopatikana kwa miaka yote hiyo? Maana yake ni kwamba huo muafaka haupo. Kuna nini wanacholazimisha hawa watu kwenye huo muungano? Kwa sababu ule mkataba wa muungano (TANGANYIKA NA ZANZIBAR) aliou-upload muungwana mmoja hapa JF hauna kipengele chochote kinachosema kuwa huu muungano ni wa milele!!! Sembuse Unguja na Pemba ambapo hata mkataba hamna!!!
KWANINI TUALAZIMISHA KUWA PAMOJA?? VISIWA VIPO TOFAUTI MUNGU ALITAKA VIWE HIVYO. SASA KWA NINI TUNALAZIMISHA WATU WAJE WAUANE BAADAE?? KWANINI? KWANINI? KWANINI? KWANINI? NA KWANINI????? SIPATI JIBU HATA NIKIJIULIZA MARA ELFU!!! MWEEE!!!

PS: Nachanganya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar NA Unguja na Pemba kwa sababu ni yaleyale tu, msichanganyikiwe waungwana!!! Kama visiwa vipo tofauti lakini kunautawala mmoja kwangu ni muungano tu.
 
Last edited:
Wanabodi,
Leo hii mimi nafunika kabisa mjadala huu na kama kuna mtu mwenye hoja naomba tuzungumze sisi badala ya kunyooshea vidole viongozi wetu kwa sababu hii habari ya Muafaka ni hatari tupu haina kichwa wala miguu...
Nasema hivi kwa sababu toka nimeuliza maswali yangu sijapata jibu toka kwa kiongozi yeyote hivyo imenijenga imani ya kusema yangu haya machache..

MUAFAKA ni UFISADI mwingine unaotaka kujengwa na baadhi ya viongozi wa CCM na CUF na ndio maana wanashindwa kufikia maamuzi kwa sababu kila chama kinavutia upande wake kutopoteza umaarufu wake...Hivyo limekuwa swala la vyama badala ya nchi nzima.
Swala zima halitawaliwi na Vyama hivi viwili kimsingi isipokuwa swala hili linatawaliwa na hitlafu zilizopo ktk Muundo ya JAMHURI YA MUUNGANO wa nchi hizi mbili - Kutotambua kuwa kuna nchi mbili hapa zimeungana kikatiba.

Ebu tufikirini kwa kina kwanza ktk hoja nzima ya Muafaka! Kwa nini CUF wanadai serikali ya Mseto?... na Pili kwa nini CUF wanadai nafasi ya Kiongozi toka chama chao?..
Bila shaka utakuta kwamba kama Muungano wa nchi zetu ungekuwa umejengwa toka mwanzo kama serikali mbili zilizoungana kuleta NCHI moja tusingekuwa na matatizo haya hata kidogo kwa sababu serikali ya Zanzibar ingekuwa na viongozi wake ktk state hiyo na Bara ambayo leo haitambuliki ingekuwa na utawala wake vile vile nje ya SERIKALI KUU.. lakini kutokana na ujenzi wa kiutawala uliopo sasa hivi Bara ni nchi inayojulikana mdomoni tu lakini hakuna nchi kama hiyo KIKATIBA..Tanzania bara haina viongozi wala uongozi kama nchi iliyoungana na Visiwani kwa hiyo CUF wanachoweza kukiona hapa ni Visiwani tu kama nchi na wameshindwa kuona kwamba Bara pia ni nchi na kuna kila haja ya kuwa na serikali yake ili maswala ya serikali ya mseto na Uongozi mdogo wa state hizi upate ufumbuzi.

Nitatoa mfano hapa mdogo sana..
Kama nchi yetu itakubali kuwa na serikali TATU yaani ile ya kujenga State ama Province 2 ni rahisi Zanzibar wakawa na viongozi wao watakao tokana na uchaguzi mkuu na Bara pia ikawa na wawakilishi wake ndani ya state hiyo na pia ktk serikali kuu. Kwa utaratibu huu kuna uwezekano kabisa kuwa Zanzibar kama state ikaongozwa na CUF na bara kama State ikaongozwa na Chadema kisha serikali kuu ikawa CCM.. How?..
Nitaeleza kwa kifupi..
Mathlan, huu ni mfano tu, kwamba katika Uchaguzi mdogo wa State ya Visiwani CUF wameshinda hivyo kuunda serikali ya huko na Uchaguzi mdogo Bara Chadema wameshinda na kuunda serikali ya Bara lakini unapokuja jumlisha chaguzi zote toka states zote mbili CCM wana wajumbe wengi kuliko vyama vinginevyo..
Nitasherehesha maneno yangu kwa mfano huu wa takwimu...
Uchaguzi CUF wamepata viti 60 kati ya 100 Visiwani na 3 kati ya 200 bara; Chadema kiti 1 Visiwani, 100 Bara; Na CCM wakapata viti 40 visiwani na 90 Bara...
Kwa hiyo ukitazama Zinzibar utaona CUF ndio mshindi kwa viti 60, Bara mshindi ni Chadema kwa viti 100 lakini tunapojumlisha viti vya kila chama kwa Taifa zima CCM ndiye mshindi mwenye jumla ya viti 130 Bara na Visiwani.. hivyo wataongoza serikali kuu.. Mara nyingi sii rahisi kupata hesabu za namna hii lakini hii ni ktk kuonyesha demokrasia ya kweli inavyoweza kufanya kazi ktk nafasi ndogo sana nya uwezekano kwani mara nyingi vyama vinavyoshinda majimbo mengi huwa ni vile vilivyojijenga vizuri Kitaifa.
Kwa utaratibu kama huu kila chama kitajaribu juu chini kujitangaza zaidi nje ya mipaka ya sehemu ambazo wamejijenga kisiasa kwa sababu Utawala ya nchi nzima ndio hutoa mwelekeo wa nchi nzima Kiuchumi ktk maswala ya taifa zima na rahisi kwa vyama na wananchi kuona vizuri ubora na mafanikio ya sera za chama kimoja toka state mojawapo na mapungufu ya chama kingine kutoka state nyingine hivyo wananchi wanaweza kuwa na picha kamili ya utekeleza wasera hizi.

kwa hiyo basi swala zima la Muafaka ni siasa za machakani.. hazifai na nasema binafsi sikubaliani nazo leo wala kesho baada ya kuwekwa sahihi ya muafaka kwa sababu source ya matatizo yote haya sio vyama isipokuwa mgawanyiko wa serikali hizi za muungano kiutawala. Tukiweza kutenganisha tofauti zetu kama nchi mbili tofauti zilizoungana basi ita solve tatizo la mseto ama utawala wa bara na Visiwani. haiwezekani kabisa Zanzibar wawe na sijui Waziri wao kiongozi hali tuna Waziri mkuu wa serikali ya Jamhuri..What about Bara ambayo imemezwa na huu Muungano?..hili ndilo swali litakalo fuatia baada ya Muafaka!..kwani huyu waziri mkuu atakuwa hawakilishi bara hata kidogo na pia katiba imeaacha wazi uwezekano wa rais wa jamuhuri kutoka CUF hapo swala la Uongozi Bara litapewa sura gani If CUF wins General election, Makamu wa rais na Waziri mkuu watatoka wapi and why?...
MUAFAKA hautyufai kinachotakiwa ni muundo mpya wa serikali tatu kuondoa uhasama wa kisiasa nchini... Ni muhimu kutambua kuwa nchi mbili hapa zimeungana na sio swala la kutambua vyama viwili vinavyotawala. Mustakabali wa nchi sio vyama ila ni utaratibu wa uongozi kikatiba kulingana na sheria za uchaguzi.
 
Back
Top Bottom