Muafaka CCM, CUF na CHADEMA upi bora?

dos santos

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
256
128
Baada ya chama cha CUF kufanya maridhiano na CCM juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa huko visiwani Zanzibar,chama cha CHADEMA kilikuwa mstari wa mbele kupinga na kubeza maridhiano hayo,huku kikiishutumu CUF kama CCM B.Uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa unatokana na kura za maoni ya wazanzibar.Hivyo uundwaji wa serikali hiyo umetokana na maamuzi ya wananchi.
Majuzi CHADEMA wameafikiana na serikali ya CCM juu ya kuridhiana mwenendo wa uratibu wa uundwaji wa tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya.Wamekubali muswada usainiwe(tayari umeshasainiwa jana) na kama wana maoni yao basi wapeleke bungeni mwezi januari.Wamekubali na kutia saini kitu ambacho hata wenyewe hawajui maslahi yake.Bila shaka walipenda kwenda ikulu,waliwahi kuahidi kwa gharama yoyote watafika ikulu.Na kweli wamefika na Juice wamekunywa.
Sasa angalia baina ya miafaka hii miwili CCM,CUF na CCM,CHADEMA upi bora na wenye tija kwa wananchi,na ambapo kulikuwa na ulazima wa kukaa meza moja na kufanya maridhiano?
 
CHADEMA HATUNA MUAFAKA NA CHAMA CHOCHOTE ,

HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE period;;;
 
Heri wa çcm & cuf una tija na tumeiona. Mf. Daftar la mpiga kura tunalo sasa. Serikali ya mseto ZNZ. wa CDM Maazimio bado ni siri na saini niya watu wawili nchimbi/mnyika. Mazungumzo afanye jk saini atie nchimbi.
 
muafaka ni kati ya CHADEMA na Serikali sio CHADEMA na CCM

Serikali ya chma gani?TLP? Kwa mfmo wa TZ ulivyo huwezi kutofautisha CCM na serikali ndio maana hata CEO ma Taasisi na mashirika ya Umma kuna wakati wanatoa maelezo ni jinsi gani wametekeleza Ilani ya CCM.
 
Deus Kibamba kaachwa solemba na CDM yeye kabaki kupiga kelele wenzake watinga ikulu na kurudi wanatabasamu!
 
Kilichojadiliwa na kutiwa saini pale juzi ni Muafaka? CDM walijua jamaa atasaini tu ila wao wana wajibu wa kumueleza ukweli atakachokiasaini na akaubaliana na hoja hasa pale alipokiri "Nimewaelewa Mnazo hoja, tena za msingi". Kikwete kama enactor,alielewa somo la makamanda ila u-CCM ndio umemtisha kwa vile upinzani dhidi yake ndani ya chama ni mkubwa sana hasa pale alipokiri "Hata mimi naona mnazo hoja za msingi, lakini nikigoma kutia saini, wenzangu kwenye chama hawatanielewa". Kwa hiyo shule imemkolea ila anaogopa kung'olewa uenyekiti CCM Taifa. Makamanda walimpa shule kilaza wenu jinsi spika anavyoua taifa na alishangaa na kuuliza "kama hoja ni hii, mbona imeshindikana bungeni?" yaani kimaantiki anauliza hivi wabunge wake na spika wa CCM hawakuona hizo points. So mazungumzo yale hayakuwa na suala la kugawana madaraka bali kumtahadharisha ubaya wa ule muswada (sheria sasa). Na CDM walifanya hivyo kwa usalama wa nchi maana maelfu ya wazalendo tuko tayari anytime kuingia Tahrir square tukiambiwa neno tu na makamanda wetu.
 
mbona unadanganya watu wewe?? acheni kutetea CDM, Leo wenzako wamekasirika mswada kusainiwa wewe unasema walijua,...which is which??
 
Back
Top Bottom