mashikolomageni
JF-Expert Member
- Jan 5, 2010
- 1,570
- 187
Tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikiambiwa mikoa ya kusini hasa mkoa wa Mtwara ni masikini sana, na kutokana na umasikini huo serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania haiwezi kuendeleza kusini kwa kujenga miundo mbinu mbalimbali kama barabara, kupanua bandari, reli, hospitali, Shule pamoja na vyuo vya elimu ya juu, maji na nisharti. Sababu kubwa ni kwamba mkoa huu unachangia kiasi kidogo cha mapato ya serikali. sina hakika sana kama majibu haya yaliyotolewa na wengi yalikuwa ya kweli lakini yalielekea kuwa ya kweli maana yalisemwa na wengi tena wengine wenye nafasi kubwa kubwa kwenye ofisi zao.
Ahaa!!! leo hii kwa mujibu wa takwimu za TRA "TRA Quaterly Revenue collection 2011_2011". Mkoa wa Mtwara ni wa 7 katika kuchangia kwenye pato la taifa kwa kodi. Kwa lugha nyepesi ndio wanunuzi wakubwa wa mashangingi ya serikali, au ndiyo wachangiaji wakubwa wa mafuta ya Jet stream ahaa na posho za wabunge, looh na posho za vyama vya siasa.
Swali langu: Imekuwaje mbona hayo maendeleo tuliyonyimwa tangu uhuru kwa kisingizio cha uchangiaji mdogo kwenye pato la taifa hayaletwi
hivi sasa tunapochangia kwa kiasi kikubwa au vigezo vimebadilika?
Tafadhali naombeni mchango wenu na ushauri wenu kwetu sisi wana Mtwara.
Nimeambatanisha jedwali la makusanyo kwa mujibu wa report za TRA: www.tra.go.tz
Region Million TShs Million TShs Million TShs Million TShs Ranking Direct Tax Indirect Tax Customs and Excise Total Ilala 56,801.9 32,545.3 - 89,347.2 1 Kinondoni 32,858.7 16,414.7 - 49,273.4 1 Temeke 12,987.0 10,677.7 - 23,664.6 1 Arusha 15,101.3 10,111.9 9,383.1 34,596.3 2 Coast 1,478.9 562.4 91.1 2,132.5 Dodoma 3,787.6 1,385.8 17.5 5,190.8 Iringa 3,471.4 1,941.9 20.5 5,433.9 Kagera 967.1 1,082.9 1,938.7 3,988.7 Kigoma 694.5 342.1 786.5 1,823.1 Kilimanjaro 6,834.2 2,947.3 11,389.3 21,170.8 3 Lindi 284.2 154.5 22.9 461.5 Mara
1,264.0 914.4 13,882.2 16,060.7 4 Mbeya 2,605.4 2,241.0 7,446.3 12,292.8 Morogoro 5,359.6 2,427.2 70.2
7,857.0 Mtwara 7,608.5 6,838.5 270.4 14,717.4 7
Mwanza
8,905.0 3,889.9 4,577.3 17,372.2 5 Ruvuma 667.1 469.8 32.7
1,169.6 Shinyanga 1,355.0 1,068.8 37.8 2,461.6 Singida 331.0 269.1 51.3 651.4 Tabora 1,087.4 896.2 15.1 1,998.7 Tanga 2,849.7 2,231.8 9,755.7 14,837.3 6 Rukwa 748.1 235.4 97.6 1,081.2 Manyara 686.2 263.6 - 949.9
Kweli nkonde chi ntu!
Hizo ranking zenye green ndio vipi?