abby shaaban
Member
- Dec 20, 2012
- 14
- 4
Wamakonde hawajielewi.
kabila gani linajielewa na sababu zake
Wamakonde hawajielewi.
Mtwara na Lindi sina uhakika kama waweza fanya mambo makubwa hivi....ila ingekuwa Mbeya ningekuwa na uhakika wa100% ges isingeondoka pangechimbika!
Kwa kweli huwa sijui kama mipango yetu ya Kitaifa hasa ya maendeleo kama hufanywa na watalaamu. Kama ndivyo basi hatuna watalamu kitu ambacho siamini. Kwa mtu wa akili ya kawaida tu siye mtaalamu wa uchumi wala wa nishati hawezi kutotambua yafuatayo kuhusu gesi au mafuta yaliyogunguliwa huko kusini mwa Tanzania:
1. Tunataka yazalishe umeme ili tupate unafuu wa bei ya umeme. Umeme huo unaweza kuzalishwa huko huko kusini na kuingizwa kwenye grid ya Taifa huko huko kusini. Kwani mbona huko Mtera, Tanga n.k. wanazalisha umeme huko huko na kuingizwa kwenye grid ya Taifa? Sasa sijui sisi ni majuha au vipi, tunataka umeme huo tukauzalishie Dar kwa kuisafirisha hiyo gesi gafi kwenye bomba lenye kipenyo cha urefu wa mtu (over 1.5 m) na urefu wa over 550 km la gharama ya over TShs 3 trions! Mitambo iliyopo pale Ubungo ya Symbions, PTL, Songas n.k. bei yake kila moja haizidi TShs 150 billion. At most yote kwa pamoja haizidi TShs 1 trion. Tungeweza hata kui dismantle na kuisafirisha na kuifunga huko Mtwara kwa gharama ndogo zaidi. Au tungeweza kununua mitambo mingine mipya mingi kuliko iliyopo Ubungo na kuifunga huko Mtwara kwa chini ya bei ya hilo bomba, na kuweza kuzalisha umeme kwa gharama ndogo. Viwanda vya Dar vinaweza kuendelea kupata gesi kwa kutumia meli toka Mtwara ambazo gharama zake ni nafuu kuliko bomba au lori. Wastage kwenye bomba ni mkumbwa sana, kwanza lazima lijae (over 1 trion cubic metre) excess ndiyo itafika Dar. Njiani cho chote kinaweza kutokea kwenye hilo bomba na inaweza ikawa disaster tupu.
2. Matumizi mengine ya hiyo gesi ni majumbani, kupikia hivyo kuokoa mazingira kwa kupunguza kukata miti kwa ajili ya mkaa au kuni hasa kule vijijini. Kuna sababu gani gesi hiyo isijazwe kwenye hiyo mitungi au containers za gas za Oryx n.k. huko huko Mtwara na kusafirishwa kwa meli au malori hadi huko Dar na kwingineko ambako inahitajika?
3.Kwa hiyo hata mafuta ya petroli yatakapoanzwa kuchimbwa huko kusini yatabidi yasafirishwe gafi kwenye bomba hadi Dar kwa refinary badala ya hizo refineries kujengwa Mtwara?
4. Mhhhh, ndiyo maana tunashindwa kufunga mitambo ya kufua umeme unaosemekana wa zaidi Megawatts 5,000 huko kwenye mafuriko ya Steinghlet kwa sababu tunashindwa kuyahamishia hayo mafuriko Dar? Vivyo hivyo kwa makaa ya mawe na hata uranium zingekuwa Dar mambo yangekuwa poa! Jamani Tanzania si Dar peke yake na wawekezaji waambiwe hivyo, wapo watakaoelewa tu. Wasiolewa waachane na sisi, yote ni kwa faida yetu sote kwani gharama zitakuwa nafuu kwa wote wala si Mtwara peke yao. Vinginevyo wananchi watashindwa kuwaelewa kwa maamuzi kama haya yasiyokuwa na logic. Watafikiri kuna mlungura umetembea! Si vizuri, muwaelimishe.
Big up Mtwara corridor, keep up and we all stand to benefit.
Wewe kweli ni Maamuma kama jina lako linavyosomeka!
Mkuu mimi kosa langu nini?nilichokifanya ni kutaja tu jina lako ambalo wewe mwenyewe ulijibatiza!Hujakosea Mheshimiwa.
Sikujua kwamba kuomba kuelimishwa ni kosa, nisamehe bure. Nilidhani bado tuko enzi zile za "nitatumia elimu yangu kwa faida ya wote". Hata hivyo nashukuru, nimepata majibu niliyohitaji kutoka kwa wachangiaji wengine. Naendelea kukushukuru na kukutakia baraka za Mwenyezi Mungu. Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mimi kumbi.
Matumizi ya Gesi naona watu wengi hawaelewi lengo sio kupeleka Dar peke yake bali nchi nzima Dar ni mwanzo tu. Vilevile leo la mbali ni kupeleka kila nyumba kama ilivyo Europe kwa matumizi ya nyumbani. Dar ni kituo tu lakini Gesi inatakiwa kutawanywa Tanzania nzima. Gesi ambayo itaenda nje inatakiwa kupakiwa kitaalamu kutoka Mtwara na hii ndiyo Investment kubwa vilevile Gesi inatakiwa kutawanywa Mtwara na Lindi pia.