Mtwara kumekucha; Maandano ya kupinga kusafirisha gesi yaja

Status
Not open for further replies.
THE BIG SHOW,

alfumia support...hakikisheni mikataba itakua wazi...na musikubali mpaka 25% ya mapato yabaki Mtwara....huu ndio wakati wenyewe mukikosa sasa mujue ndio basi....wachagizeni mpaka kieleweke....mali hio ipi mtwara mnatakiwa mufaidi...
 
Last edited by a moderator:
Nyinyi watu wa mtwara acheni ubaguzi,mbona barabara zenu zimejengwa na almasi na dhahabu iliyokuwa inachimbwa kanda ya ziwa?

elewa kwanza mada,umeme upelekwe kwenye grid ya taifa ila uende kwa njia ya nguzo,km ulivyo pelekwa shinyanga nk,ila ule mtambo wa kinyerezi urudi mtwara
 
Bro kwa almas na dhahabu ya shy haisafirishwi?!think big,sasa hata km shy 2ngeandamana yasisafirishwe,kuna viwanda kutengemeza products zitokanazo na madini?na je soko la bidhaa hizo liko wap kwa nchi maskin km hii?!khs mtwara,serikali imesema itasafirisha gesi yote inayozalishwa?!sidhani!gesi yote ibaki mtwara ili iweje ikiwa kuna walaji wachache kabsa?!mwekezaji huwez kumlazimisha ajenge kiwanda mtwara et kisa kuna gesi!viwanda vingi ukiacha vya chuma,cement hujengwa karibu na MASOKO!pia wanamtwara kumbuken gesi n moja ya rasilimali za taifa kwa ujumla!au mnataka kujitenga na taifa kisa gesi?!mnapaswa kuibana serikal ihakikishe gesi inakuwa chachu ya mageuz ya kiuchumi mkoan kwenu Lakini sio kwa KUZUIA GESI ISISAFIRISHWE!vinginevo mtapigwa virungu mfe bure!over.
endelea kufikilia hivyohivo,utapata jibu kesho
 
Huu ni ubinafsi wa hali ya juu. Kwanini gesi isisafirishwe? Miaka yote wakati mtwara hakuna gesi, mtwara imesurvive vipi kama sio kutumia raslimali zingine za nchi ambazo hazitoki mtwara? Wafanyakazi wote wanalipwa mishahara na serikali ambayo sehemu ya mapato yake inatokana na raslimali za mikoa mingine. Sasa gesi inayohitajika mtwara kwa matumizi mengine tayari inatumika huko. Umeme ni wa gesi, na wawekezaji waliokuwa wanasingizia umeme bado hawaendi, wanasema ni mbali na masoko. Serikali ikilegea hapa kuna wapuuzi watasema mtwara ijitenge iwe nchi, kisa gesi!! Stupid!!

what you say is simply raw rubbish, mbali na masoko yapi?
 
elewa kwanza mada,umeme upelekwe kwenye grid ya taifa ila uende kwa njia ya nguzo,km ulivyo pelekwa shinyanga nk,ila ule mtambo wa kinyerezi urudi mtwara
Bado nasema huu ni ubinafsi wa hali ya juu,mbona tumbaku inazalishwa Tabora lakini kiwanda cha sigara kipo Dar es salaam?Mbona pamba inazalishwa mwanza na shinyanga lakini kiwanda cha nyuzi kipo Tabora?
 
Mtwara waonyesheni njia Watanzania! Hiyo nimeipenda sana.
 
kati ya huko mtwara na Mwanza wapi zilianza kujengwa barabara za kiwango cha rami?

1. rami = lami
2. Nadhani sikueleweka. Nilikuwa nauliza kama hizo dhahabu na almasi zilijengewa viwanda Dar?
Naomba kuelimishwa kabla sijapotoka. Asante.
 
Bro kumbuka watakaojenga viwanda n makampun binafsi na si serikali!yani umlazimishe bakhresa aje kujenga kiwanda mtwara kisa et kuna gesi!mwekezaj anaangalia faida yake kwanza!,ni waz kujenga kiwanda kwa lindi na mtwara sio Profitable ukilinganisha na dar!usitegemee mwekezaj kutia maguu huko km faida haion.Over!
 
1. rami = lami
2. Nadhani sikueleweka. Nilikuwa nauliza kama hizo dhahabu na almasi zilijengewa viwanda Dar?
Naomba kuelimishwa kabla sijapotoka. Asante.
Wewe kweli ni Maamuma kama jina lako linavyosomeka!
 
Last edited by a moderator:
Sabal kheri wana bodi

eti kuna mtu anauliza mbona mnapigana vikumbo kupanga foleni kuuza korosho katika vyama vya msingi ili isafirishwe na kwenda katika viwanda huko india?

mbona hamjawahi kulalamika kwamba hamko tayari kuuza korosho ghafi hadi vijengwe viwanda mtwara vya kuchakata korosho hapa hapa mtwara?

eti gesi itawanufaisha watu wa Dar es salaam? ila hamuoni korosho inavyowanufaisha wahindi?

mwaka huu mkipalilia na kupulizia mikorosho vuneni korosho mjaze katika magunia kisha muandamane kuishinikiza serikali kuwa hamko tayari kuuza korosho mpaka vijengwe

viwanda hapa hapa mtwara kwani kwa sasa korosho inawanufaisha wahindi kama gesi itakavyowanufaisha wanadar es salaam.


wasalaaam

Mkereketwa wa kusini
 
Ni upuuzi kurundika kila kitu Dar!

Naungana nawe Nyangakeni, hakuna sababu ya kurundika kila kitu Dar es salaam.

Kama lengo la kuipipe hii gesi kwenda Dar ni kwaajili yakuzalisha umeme, nashauri hilo lisifanyike badala yake mitambo hiyo ifungwe huko huko Mtwara badala ya kufungwa tena Dar es Salaam. Kwa maoni yangu, kwa sasa Dar es Salaam, hususani Ubungo, ni eneo hatari sana kwa binadamu kutokana na mrundikano wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi (Songas, Symbion na Aggreco) katikati ya jiji lenye wakazi wengi. Mbali na kuzalisha joto kali na hewa nyingi ya Carbondioxide katika eneo lisilokuwa na miti ya kuiabsorb, inahatarisha maisha ya wakazi wa Dar es Salaam. Sijui kama kulifanyika utambuzi wa madhara ya kimazingira na kijamii (Environmental and Social Impact Assessment) kama inayotakiwa kisheria kabla ya kuanzishwa miradi hii katika eneo la Ubungo, maana mitambo ile inayaweka maisha ya wakazi wa Dar es Salaam rehani. Hitilafu yeyote kwenye ile mitambo inaweza kuiangamiza Dar nzima kwa moto. Tuendelee kumuomba Mungu atuepushe na maafa lakini tusiendelee kuongeza uwezekano wa kupata maafa kwa kuendeleza ujenzi wa miatambo ya kuzalisha umeme wa gesi katikati ya jiji lenye wakazi wengi, yaani Dar es Salaam. Tujifunze kutokana na makosa ya wenzetu yaliyosababisha maafa makubwa kutokana na milipuko ya gesi na hata yale ya milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo Mboto. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Wtanzania ili wafikiri na kutenda ipasavyo.
 
Mijitu mingine bwana! Hiyo gesi mnayo hapo miaka kibao mbona hamkuendelea?
Hata hayo maendeleo kidogo mliyanayo yanatokana na mapato ya maeneo mengine ya nchi hii na misaada ya nje.
Mliwahi kuambiwa maendeleo hayaji bila KULIWA. Kwahiyo mtake msitake hiyo gesi itatumika kama mipango ilivyo sasa.
Maendeleo katika maeneo yetu yatatokana na Uadirifu wa wale tunaowachagua kusimamia na kuongoza na sie wengine kufanya kazi kwa bidii.
 
mi ninachopinga ni Why Dar? Imefikia hatua watu wanafikiria kujenga flyovers wakati vijijini hakuna maji. Kutafuta maji ni siku nzima
Haya ni matatizo ya kutokuwa na serikali za mtaa zenye mamlaka. Mf majimbo chini ya magavana wenye kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi ndio imesababisha maendeleo yote yawe Dar. mfano kama chuo cha IFM kimejaa kwanini wanajenga kingine ndani ya Dar? Kwanini Mzumbe imefungua tawi dar na lina wanafunzi wengi kuliko la Morgorogo?. Ukipata majibu ya hayo utajua kwanini ni muhimu kuwa na utawala wa serikali za mtaa
 
Tatizo lenu huko N'twara na Lindi mmelala sana shime amkeni mke wako alafu iweje uanze kupangiwa ratiba na mtu baki kulala nae.
 
Matokeo ya serikali legelege kila kitu msebwemsebwe> Huu ni mwanzo na mengine mengi yaja.
Kuna tetesi kuwa mmoja wa mawaziri toka mikoa hiyo ndiye anayeratibu harakati hizo kwa mgongo wa wananchi. Tusubiri tu habari kamili tutaipata.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom