Mtwara kumekucha; Maandano ya kupinga kusafirisha gesi yaja

Status
Not open for further replies.
Huu ni ubinafsi wa hali ya juu. Kwanini gesi isisafirishwe? Miaka yote wakati mtwara hakuna gesi, mtwara imesurvive vipi kama sio kutumia raslimali zingine za nchi ambazo hazitoki mtwara? Wafanyakazi wote wanalipwa mishahara na serikali ambayo sehemu ya mapato yake inatokana na raslimali za mikoa mingine. Sasa gesi inayohitajika mtwara kwa matumizi mengine tayari inatumika huko. Umeme ni wa gesi, na wawekezaji waliokuwa wanasingizia umeme bado hawaendi, wanasema ni mbali na masoko. Serikali ikilegea hapa kuna wapuuzi watasema mtwara ijitenge iwe nchi, kisa gesi!! Stupid!!
 
Maandamano halali, makubwa na ya kihistoria
yanatarajia kufanyika Alhamis hii tar
27.Disemba.2012 kupinga GESI isiondoke Mtwara
ikiwa GHAFI. Maandamano yataanzia maeneo ya
Mtawanya saa tatu asub. Mlioko Newala. Masasi,
Tandahimba, Nanyamba. maeneo ya Lindi na Kwingineko tuungane kutetea maendeleo ya KUSINI
kwa ujumla.

Majuzi Jumamosi iliyo pita kulikuwa na mdahalo BBC ukiongozwa na Barihani Mwihuza na ulikuwa ukiongelea Faida ya Rsilimali zetu kwa watu esp wanao husika katika hayo maeneo kama huko Geita, Kahama Mwadui, Nyamongo Nzega Mererani na Mtwala esp Gesi ila watu wengiu walikuwa wametupia Macho kwenye GESI. Viongozi wengi walichangia na wananchi walitoa maoni yao. Ila upande wa maoni ya wanananchi kuna mtu mmoja alisema Hivi hii GESI kama Ingekuwa inapatikana Arusha kweli ingetengenezewa Bomba na kwenda DAR akasema sidhaani kama wananchi wa Arusha wange afiki hilo. Hii ni tosha wazi kuwa wanana mtwara sasa wana funguka wanaanza kujitambua na kutambua haki zao za kimaendeleo.

Serikali inapo shindwa kuandaa mikataba maslahi kwa wananchi kweli ndio watakao tutolea hii amani ambayo wao viongozi wanakaaa majukwaani wakihuriuri amani ingali wao ndio wachochozi wa kuvuruga amani na mara nyingi huwa nasema kwa JF amani ya sehemu yeyeote huvurugwa na viongozi tulio wapa dhamana ya kutuongoza na kusimamia asilimali zetu.

Sasa haya yaja mtwara yametimia sasa kuutuliza huu moto ni kushusha vinu vyote vya mitambo kwa mkoa huo na kila aina ya kiwanda kinacho husika na GESI kufanyika hapo then wasafirishe ilisha kamilika then pata tulia na sio viongozi kuingia mikataba kwa minajili ya wao binafsi na wanalisahau Taifa.

My close friend aliniambia alikuwa mtwara akasema nyie serikali inatudanganya sasa mwasema GESI bado yafanyiwa majaribio hiyo ni uongo mkubwa twastahili kupata faida ya gesi effectively from now na sio kesho ni kuweka mikataba bora kwa manufaaa ya Taifa letu.

Sasa Police mnao penda kuuwa watu mwende sasa this time HUMAN RIGHTS watakuwa nyuma tena GESI na mwajua Gesi ilivyo na thamani Duniani.

Police mjipange kuiambia serikali huku sasa ni kugonga hodi The HAGUE COURT bila kulazimishwa. Chonde chonde



 
Bro kwa almas na dhahabu ya shy haisafirishwi?!think big,sasa hata km shy 2ngeandamana yasisafirishwe,kuna viwanda kutengemeza products zitokanazo na madini?na je soko la bidhaa hizo liko wap kwa nchi maskin km hii?!khs mtwara,serikali imesema itasafirisha gesi yote inayozalishwa?!sidhani!gesi yote ibaki mtwara ili iweje ikiwa kuna walaji wachache kabsa?!mwekezaji huwez kumlazimisha ajenge kiwanda mtwara et kisa kuna gesi!viwanda vingi ukiacha vya chuma,cement hujengwa karibu na MASOKO!pia wanamtwara kumbuken gesi n moja ya rasilimali za taifa kwa ujumla!au mnataka kujitenga na taifa kisa gesi?!mnapaswa kuibana serikal ihakikishe gesi inakuwa chachu ya mageuz ya kiuchumi mkoan kwenu Lakini sio kwa KUZUIA GESI ISISAFIRISHWE!vinginevo mtapigwa virungu mfe bure!over.
 
Nyinyi watu wa mtwara acheni ubaguzi,mbona barabara zenu zimejengwa na almasi na dhahabu iliyokuwa inachimbwa kanda ya ziwa?
 
Naunga mkono hayo maandamano kwa 100% kama kusini sasa wamejitambua basi 2010 tutarajie mabadiliko makubwa.
 
Huu ni ubinafsi wa hali ya juu. Kwanini gesi isisafirishwe? Miaka yote wakati mtwara hakuna gesi, mtwara imesurvive vipi kama sio kutumia raslimali zingine za nchi ambazo hazitoki mtwara? Wafanyakazi wote wanalipwa mishahara na serikali ambayo sehemu ya mapato yake inatokana na raslimali za mikoa mingine. Sasa gesi inayohitajika mtwara kwa matumizi mengine tayari inatumika huko. Umeme ni wa gesi, na wawekezaji waliokuwa wanasingizia umeme bado hawaendi, wanasema ni mbali na masoko. Serikali ikilegea hapa kuna wapuuzi watasema mtwara ijitenge iwe nchi, kisa gesi!! Stupid!!

Mkuuu Hahahahaha, Kwa upande fulani umesema sawa ila kwa upoande fulani hujafanyia utafiti, sawa miaka yote watu wa kule esp wafanya kazi wanalipwa mishahara sawa hatukatai je ni mikakati gani ya kimaendeleo ya kukuza mji wa mtwara yanafanyika kuimarisha uchumi uwe endelevu kwao? ni wapi dunia una rasilimali umeikali chini alafu leo unajua unayo na uikatae isikusaidie huo si ndio utakuwa wenda wazimu sera za rasilimali kokote dunia ni wajibu kuboresha mahali inapotoka pia sasa kama serikali yetu haionyeshe hata dalili za kukuza au kuimarisha mji wa mtwara wategemea kweli pale patatulia msiingize siasa hapa na kuwafanya wananchi wawe madunga embe Tatizo kubwa katika nchi yetu ni kutokuwa na uongozi bora siasa safi na ndio maana mikataba mingi wananchi wanaipigia kelele sasa mi sikuelewi wewe huko kwa taifa gani?

Uongozi wako ukiwa legelege na unamashaka wananchi hawato weza kuwa na imani nawe ila uongozi wako ukiwa imara na ukawahakikishia wananchi unao watawala watakuwa na imani nawe uta tenda. hebu nipe mifano ya maendeleo ya Nyamongo leo esp wananchi wa eneo lile wanafaidika vipi na Dhahabu inayo chimbwa pale, nipe maendeleo ya Mwadui Mining pale maganzo wanakijiji wa pale wana maisha gani? Nenda leo Merelani unipe jibu pia na uliza Tanzanite One inachangia pato la taifa kiasi gani kwa mwaka alafu ndio uijende hoja yako tena upya.

Nenda kusini mwa afrika Botswana nchi ndogo tu ni kama tuchukuwe Kaskazini Moshi tanga Arusha mfano wake wana ufugaji wa ngombe ndio unawaingizia pato kubwa pia katika nchi yako sasa ukigawa tanzania katika majimbo kama nilivyo toa basi na tukasimamia rsilimali zetu vyema je tutakuwa maskini? sasa kama uongozi wetu haujajipanga tutakuwa wajinga mpaka lini kwanini leo tusiwapigie kelele waha viongozi wetu wajue nasi twajua angalau machache juu ya rasilimali zetu.


 
kwann viwanda vinavyotumia gas kuzalisha umeme visingejengwa kusini kulikuwa na sababu gani ya msingi kujenga dar kama sikuna siri imejificha hapo ni haki yao kufanya wanachotaka kufanya na pia hayo ndio maendeleo jamii kutambua haki yako ni moja ya hatua katika maendeleo msiwazingizie chadema watanzania wanajua kila kitu wamepevuka wamesoma na wamejitambua kuwa ni watanzania
 
Kazi kwenu wana-ntwara na lindi, msipokuwa na mshikamano wa pamoja mtabaki kuwa watazamaji tu huku rasilimali zenu zikichukuliwa mbio mbio. Chezeiya magamba weye? kuwatia umasikini wananchi ndio agenda yao ya kudumu.
 
Naona kuna ushamba kidogo hapa wa Gesi ya asilia. Gesi haisafirishwi na matenka kama mafuta sasa mnataka Gesi iende vipi kwenye matumizi ya nyumba zaidi ya pipeline. Kwa matumizi ya nyumbani Gesi inabidi kusafirishwa kwa pipeline lakini kwa kupekeza nchi za nje wawekezaji watajenga kituo cha kuifanya gesi kuwa liquid na kuishafirisha nje hii itajegwa hukohuko inakotokea ni miradi tofauti. Gesi ya Dar ni kwa matumizi ya umeme na nyumbani tu.

hiyo ya matumizi ya umeme na nyumbani ianze kusambazwa mtwara na lindi kwanza ndo iende kwingine, kwa nini dsm kwanza ?, nahisi ubongo wako umeoza.
 
kusini ndo wanakotoka membe,ghasia,mkuchika,chikawe, majaliwa na mama kikwete....! haiwezekani wakaacha mambo yaharibike kiasi hicho!
 
Mkuu ungemuuliza na THE BIG SHOW CCM wanaingiaje ningefurahi sana kwa ababu na yeye ameanza na CCM sasa sijui anataka kutotoa kwenye mada ili tuanze malumbano yasiyo na tija kwetu sisi???!!

CCM wanaingia hapa moja kwa moja kwasababu nichama kilicho shika dola na dola ndiyo inafanya maamuzi kama haya...
 
Huu ni ubinafsi wa hali ya juu. Kwanini gesi isisafirishwe? Miaka yote wakati mtwara hakuna gesi, mtwara imesurvive vipi kama sio kutumia raslimali zingine za nchi ambazo hazitoki mtwara? Wafanyakazi wote wanalipwa mishahara na serikali ambayo sehemu ya mapato yake inatokana na raslimali za mikoa mingine. Sasa gesi inayohitajika mtwara kwa matumizi mengine tayari inatumika huko. Umeme ni wa gesi, na wawekezaji waliokuwa wanasingizia umeme bado hawaendi, wanasema ni mbali na masoko. Serikali ikilegea hapa kuna wapuuzi watasema mtwara ijitenge iwe nchi, kisa gesi!! Stupid!!

You too stupid.
 
Mtwara na Lindi sina uhakika kama waweza fanya mambo makubwa hivi....ila ingekuwa Mbeya ningekuwa na uhakika wa100% ges isingeondoka pangechimbika!
 
KESHO NDO KESHO wale wote wanao zani tulikua hatujui watajua kesho,watajuta kukiuka katiba ibara ya tisa kifungu kidogo cha d(9-d)kuleta maendeleo kwa ulinganifu,kesho nitakuwepokutetea ukombozi wa watu wa kusini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom