Mtwara: Gari la 'Afisa Usalama' lapondwa mawe Msimbati

Kwa wenye marafiki walio Mtwara tufanye mawasiliano tuulize kama habari hizi ni za kweli. Sitaki kuamini kuwa serikali imekosa busara kiasi kikubwa namna hiyo!

Hutaki kuamini nini, !?? labda kama huijui serikali yetu... BTW huwa unafuatilia matukio ya nchini humu ndugu, hususani yale yahusuyo mgogoro wowote baina ya serikali na wananchi...!??
 
|Haya sasa! ngoma inogile - serikali itafakari na kuona uwezekano wa kufanya mipango shirikishi

kweli mkuu, sijui lini watajifunza kwamba mipango yoyote ya mendeleo haitafanikiwa bila kuwashirikisha wananchi na kusikiliza maoni yao/kuwaelimisha katika hatua za mwanzoni kabisa
wangewaaminisha wana Mtwara kwamba huu mradi ni wao kwa faida yao na taifa na waka plan nao projects zitakazowapa faida ya moja kwa moja kama part ya mradi mzima wa gesi, sidhani kama haya yote yangetokea.
 
Hutaki kuamini nini, !?? labda kama huijui serikali yetu... BTW huwa unafuatilia matukio ya nchini humu ndugu, hususani yale yahusuyo mgogoro wowote baina ya serikali na wananchi...!??

Mkuu nadhani hujanielewa. Ninajua kuwa serikali yetu imeshakosa busara, tena sana tu. Ila siamini kama imefikia hatua ya kuwacharaza wazee wa kimila. Hiyo hatua si ndogo sana, nduguye! BTW, nami ni mfuatiliaji wa mambo, kwa kadri yanavyopatikana mtandaoni na kwenye vyombo vya habari. Tuko pamoja kamanda
 
hawa wazee si ndio walipewa klofia za ccm wakairudisha madarakani?
viongozi wa upinzani, mzee mwanakijiji na members wengine wengi walionya hapa jukwaani 2010 kuwa mkiirudisha ccm madarakani mmekwisha na wakapuuza. Na sasa hivi tunavyoongeA kuna onyo lingine (naona hawakati tamaa) kuwa mkiirudisha ccm madarakani 2015 sasa itakuwa zaidi ya kwisha na bado kuna dalili ndogo ndogo kuwa huenda wakapuuzia!
Lakini ccm wenyewe (yale mafisi makubwa) wameshashtuka na ndio maana sasa wanaamua kuanzisha kijiji/mji/nchi wao ndani ya nchi ili wawe salama kwa lolote litakalotokea!

This is becoming more serious than we expected. Sasa wananchi wa Mtwara kama hawataki hata majadiliano kwa hiyo sasa wanataka nini? Wamejuaje kama alikuwa amekuja kuwashawishi wazee wa Mtwara wakubali na si kwamba alikuja kujadiliana nao juu ya nini kifanyike? Nafikiri ni wakati mzuri kwa wananchi wa Mtwara kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano.

Niliwahi kuuliza siku moja kwamba hivi wakiendelea kufanya haya wanayoyafanya, halafu serikali ikaamua kughairi kabisa mpango wa ama kupeleka gesi Dar au kujenga mtambo pale Mtwara, badala yake wakaelekeza macho kwenye makaa ya mawe kule Ludewa, wananchi wa Mtwara wataifanyia nini hiyo gesi? Watachota kwenye ndoo na kwenda kuuza au wataifanyeje?

Hoja yao ina msingi, lakini waruhusu majadiliano, kama haiwezekani kujenga mtambo kule basi wakubaliane na serikali terms nyingine zinazoweza kuapply ili na wao wanufaike. Lakini ubabe huu hauna maana kabisa, na unaweza usiwafikishe pazuri kabisa.

Serikali ndugu dhahiri haiko tayari kwa mazungumzo mkuu!
Hata huyo bwana,hakwenda huko kwa lengo la kutaka majadiliano. Alikwenda kwa lengo la kutaka kuwarubuni baya watu ili wagawanyike na huenda wajitokeze na kutoa matamko ya kuwa kinachoendelea HUKO ni uchochezi wa wa wapinzani na wana mtwara wenyewe wako tayari gesi iondoke,hii ni baada ya kupewa kitu kidogo.
Kwa nini aende usiku?TAFAKARI.....

Nawapongeza sana kwa walichokifanya, tena wasiishie kwa huyo, NA WAEPUKE KURUBUNIWA.
Hata dr Ulimboka alitekwa usiku na mtu aliyejifanya ana mazungumzo naye ya kutaka kuumaliza ule mgomo wa madaktari, kilichotokea sio siri.....NI HAO HAO WANAOITWA WANA USALAMA!
 
mkuu, nashukuru, hii nilikuwa sijaiona. Yawezekana ina uhusiano. Ila sasa swala la kupigwa wazee wa kimila nalo vipi, pamoja na polisi kumwagwa wengi? Haki, serikali inalikuza hili jambo na litakuja litugharimu sana watanzania

kwa mawazo yangu, polisi hawahusiki. Hawahusiki kwa sababu ya viapo na sheria mfu zilizotengenezwa na ccm. Ndio maana tunadai uongozi ubadirishwe kwa imani kuwa hata baadhi ya sheria za kishenzi zitabadilika.

Polisi wapo ili kushurutisha utii wa sheria za nchi, sasa kama sheria zinamapungufu, polisi wanalazimika kuzifanyia kazi. Kwa mfano, polisi wanaruhusiwa kutumia nguvu pale inapobidi. Sasa kwa suala la mtwara, wananchi inawezekana walianza kumtimua huyo ofisa, wakaenda mbali na kuamua kulichoma moto. Yeye kwa kuwa ni sehem ya serikali dhalimu, anajulisha kuwa nimepigwa na wamechoma gari langu, naombeni msaada. Kamati ya ulinzi mkoa wanamwamuru kamanda kupeleka vikosi na hivyo kitakachotokea ndo kama tunavyokuwa tukiyashudia sehemu zote za nchi ambazo utajiri umeporwa kwa kutumia sheria zetu wenyewe na wananchi wanajaribu kutetea rasilimali zao
 
Huyu mwana usalama mngemkung'uta kwanza. Kuchoma gari tu hakutoshi kwani wamenyanyasa na kuuwa watanzania wengi sana. Kwa sasa somo linaendelea kueleweka. Waliyomfanyia Dr. Ulimboka, Ally, Mwangosi na wengine sasa yanawarudia. Kikwete atajatambua hata Mtwara hakutawalika hata kwa mtutu wa bunduki. Yaani msakeni hadi mumpate msikubali atoke maendeo na huyo bibi asitoke hapo mtwara kwani wataenda kumwua mara moja.
 
Ni wakati wa Umma wa Watanzania hasa Mtwara kushikamana na kuwa kitu kimoja dhidi ya ulaghai unaofanywa na Watawala. Wengine tunajifanya hili ni la Mtwara halituhusu lakini kesho ni sisi. Hata lilimkuta Mwangosi na Dr. Ulimboka watu wa Mtwara walisema haliwahusu kwani wale ni wataalamu.
 
Mkuu watu wa mtwara nadhani wanauelewa sana,kama ni majadiliano kwanini yawe ni usiku na kwa kujificha???wanataka mjadala mpana kuhusu hili swala na sio kama ilivyo,utawalaumu sana hawa jamaa lakini elewa serikali ilikuwa inawachukulia kama wahaini na wanataka umaarufu,kuhusu kuhairisha haitakaa itokee kwenye serikali hii kwani wameshakula vya watu kama alivyosema mkuu ukila lazima na wewe uliwe!!!Time will tell!!
 
hata Askofu kakobe alitishia umeme wa nguzo za Tanesco atauzuia kupita kwa maombi kanisani kwani lakini bado ukapita

Pale Mtwara ina maana itatumika nguvu ya giza na siyo maombi.

Ni vitu viwili tofauti, nguvu ya giza ni imani ya kishirikina. Na mao,bi inategemea na imani yako kwa mwenyezi Mungu. Ukiwa na imani haba huwezi kufanya miujiza.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kosa hapa ni kuingiwa kwa mkataba.
laiti wangejadili kabla, wakaipa thamani gesi, mkataba ungeelekezwa kuheshimu thamani ya gesi kwa mwenye gesi dhidi ya kibarua aichimbaye na kuifikisha sokoni, wala soko lisingekuwa mjadala kama inavyotokea sasa, MJADALA UNALENGA TUIKUBALIE SERIKALI KWA FAIDA YA "VIBARUA" TUNAOWAAJIRI KUTUCHIMBIA GESI, NA WALA SI SERIKALI ITUELEWE NA KUTENDA KWA FAIDA YETU NA TANZANIA YETU.
 
hizi ni tetesi ambazo zimeenea hapa Mtwara kuwa mtu aliyejitambulisha toka magogoni ametumwa kwenda kumuchukua bibi wa msimbati(sakata la gesi). lakini kabla ya hapo bibi alioteshwa na kuwaambia watu kuwa watakuja watu kumdhuru hivyo wasitoke pale nyumbani. inasemekana gari lake li meharibiwa vibaya baada ya yeye kukimbia.
ukitaka ukweli zaidi fuatilia mwenyewe
 
This is becoming more serious than we expected. Sasa wananchi wa Mtwara kama hawataki hata majadiliano kwa hiyo sasa wanataka nini? Wamejuaje kama alikuwa amekuja kuwashawishi wazee wa Mtwara wakubali na si kwamba alikuja kujadiliana nao juu ya nini kifanyike? Nafikiri ni wakati mzuri kwa wananchi wa Mtwara kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano.

Niliwahi kuuliza siku moja kwamba hivi wakiendelea kufanya haya wanayoyafanya, halafu serikali ikaamua kughairi kabisa mpango wa ama kupeleka gesi Dar au kujenga mtambo pale Mtwara, badala yake wakaelekeza macho kwenye makaa ya mawe kule Ludewa, wananchi wa Mtwara wataifanyia nini hiyo gesi? Watachota kwenye ndoo na kwenda kuuza au wataifanyeje?

Hoja yao ina msingi, lakini waruhusu majadiliano, kama haiwezekani kujenga mtambo kule basi wakubaliane na serikali terms nyingine zinazoweza kuapply ili na wao wanufaike. Lakini ubabe huu hauna maana kabisa, na unaweza usiwafikishe pazuri kabisa.
Mawazo yako ya serikali ya ccm kuisusa gesi ni mepesi sana, hata wakiisusa gesi itatoweka ardhni? Na nani kakwambia Kikwete na ccm yake itatawala milele? Au hata CUF,CDM,NCCR wakishika madaraka na wao wataisusa? Tena wakiisusa wamakonde tunatakiwa kufanya sherehe kubwa ya ushind na then tuwashinikize wasuse na kununua korosho kwa mfumo wao wadhuluma. Kwa mawazo yako hayo, ungekuwa bondia basi ni wa uzito wa unyoya.
 
hizi ni tetesi ambazo zimeenea hapa Mtwara kuwa mtu aliyejitambulisha toka magogoni ametumwa kwenda kumuchukua bibi wa msimbati(sakata la gesi). lakini kabla ya hapo bibi alioteshwa na kuwaambia watu kuwa watakuja watu kumdhuru hivyo wasitoke pale nyumbani. inasemekana gari lake li meharibiwa vibaya baada ya yeye kukimbia.
ukitaka ukweli zaidi fuatilia mwenyewe

apo kwenye red,wewe ndio umetuletea habari unataka tufatilie tena,unataka twende mtwara au?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom