Mtwara: Gari la 'Afisa Usalama' lapondwa mawe Msimbati

ungeleta picha ya hiyo gari au namba zake ungekuwa umepungaza udaku wa taarifa hii kwa kiasi kikubwa
 
Hu bibi chizi tu hawezi kuzuia gas, mi siamini ktk uchawi na ushirikina.
 
Mimi siwezi kushangaa kwa viongozi waandamizi wa Serikali kuendekeza hayo mambo, kwa sababu huko serikalini UCHAWI na ULOZI ndio kinga ya mtu ku-maintain position yake, pia nao wanaona jinsi JK alivyo speed kwenye mamb hayo kila week end lazima aende pale kwa mzee MAARIFA bagamoyo...
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ni kuwa usiku huu majira ya saa tatu na nusu kwa saa za Tanzania , gari moja aina ya saloon iliyokuwa imembeba mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni afisa wa TISS kutoka makao makuu dar imechomwa moto na wananchi wa kijiji cha Msimbati ( hiki ndio kijiji chenye gesi ) .

Afisa huyu alikuwa ameitisha kikao usiku huu ili ,aweze kukutana na wazee wa Msimbati kwenye kikao na kilikuwa kinafanyika nyumbani kwa mzee Shabani, ajenda za kikao ni kujaribu kuwashawishi wazee ili wawaonye vijana wao kuhusiana na msimamo wao kuhusu gesi kutotoka mtwara bila wana mtwara kunufaika na rasilimali hiyo.

Gari hiyo baada ya kuchomwa moto, polisi wa FFU wameenda kijijini hapo na sasa wanapigq mqbomu kwani wananchi walikuwa wanamsaka huyo aliyetumwa kuwahqdaa wananchi, na mpqkq ninaandika hapa muda huu wa saa tano na nusu usiku ni kuwa mambomu yanaendelea huko kijijini.

Mengine ntawajuza kadiri niyapatavyo....
 
Hali huko ni mbaya na difender za FFU zinaongezeka , tutarajie kutokea kwa maafa makubwa huko....
 
This is becoming more serious than we expected. Sasa wananchi wa Mtwara kama hawataki hata majadiliano kwa hiyo sasa wanataka nini? Wamejuaje kama alikuwa amekuja kuwashawishi wazee wa Mtwara wakubali na si kwamba alikuja kujadiliana nao juu ya nini kifanyike? Nafikiri ni wakati mzuri kwa wananchi wa Mtwara kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano.

Niliwahi kuuliza siku moja kwamba hivi wakiendelea kufanya haya wanayoyafanya, halafu serikali ikaamua kughairi kabisa mpango wa ama kupeleka gesi Dar au kujenga mtambo pale Mtwara, badala yake wakaelekeza macho kwenye makaa ya mawe kule Ludewa, wananchi wa Mtwara wataifanyia nini hiyo gesi? Watachota kwenye ndoo na kwenda kuuza au wataifanyeje?

Hoja yao ina msingi, lakini waruhusu majadiliano, kama haiwezekani kujenga mtambo kule basi wakubaliane na serikali terms nyingine zinazoweza kuapply ili na wao wanufaike. Lakini ubabe huu hauna maana kabisa, na unaweza usiwafikishe pazuri kabisa.
 
Kama ni Ramadhani Ighondu mbona itakuwa raha sana ! Wananchi wasiogope mabomu , yako kidogo sana , kwanza karibu yanaisha ! waendelee kupinga dhuluma kwa vitendo ! Mtwara Oyeeeee !
 
Hali huko ni mbaya na difender za FFU zinaongezeka , tutarajie kutokea kwa maafa makubwa huko....

Sasa hivi ni usiku sana, polisi wana guts gani kwenda kwenye kijiji gizani namna hii.
Au watu wa Msambati ni waoga sana.
I thought ndo wangewafundisha somo hawa waonevu wa demokrasia.
 
This is becoming more serious than we expected. Sasa wananchi wa Mtwara kama hawataki hata majadiliano kwa hiyo sasa wanataka nini? Wamejuaje kama alikuwa amekuja kuwashawishi wazee wa Mtwara wakubali na si kwamba alikuja kujadiliana nao juu ya nini kifanyike? Nafikiri ni wakati mzuri kwa wananchi wa Mtwara kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano.

Niliwahi kuuliza siku moja kwamba hivi wakiendelea kufanya haya wanayoyafanya, halafu serikali ikaamua kughairi kabisa mpango wa ama kupeleka gesi Dar au kujenga mtambo pale Mtwara, badala yake wakaelekeza macho kwenye makaa ya mawe kule Ludewa, wananchi wa Mtwara wataifanyia nini hiyo gesi? Watachota kwenye ndoo na kwenda kuuza au wataifanyeje?

Hoja yao ina msingi, lakini waruhusu majadiliano, kama haiwezekani kujenga mtambo kule basi wakubaliane na serikali terms nyingine zinazoweza kuapply ili na wao wanufaike. Lakini ubabe huu hauna maana kabisa, na unaweza usiwafikishe pazuri kabisa.

Mkuu, hayo ya afisa usalama kwenda kwa bibi ni majadiliano?
Bibi ndo wana Mtwara? Huo ni ushawishi.
Serikali ikitaka kufanya majadiliano inaweza kufanya, lakni sio kijanja janja kwa kutuma viroboto.
Tushukuru kwamba maisha ya mtu huyo yapo salama.

Huwezi kumkejeli na kumpa maneno ya dharau mtu then, uende kushawishi badala ya kuonyesha intention to talk.
 
Sasa hivi ni usiku sana, polisi wana guts gani kwenda kwenye kijiji gizani namna hii.
Au watu wa Msambati ni waoga sana.
I thought ndo wangewafundisha somo hawa waonevu wa demokrasia.

Wengi wa vijana wanatoroka kwa hofu ya kukamatwa na hata niliokuwa nawasiliana nao eneo la tukio siwapati naona network huko ni shida , nitawajuza pindi nikiwapata hewani ...
 
Sasa hivi ni usiku sana, polisi wana guts gani kwenda kwenye kijiji gizani namna hii.
Au watu wa Msambati ni waoga sana.
I thought ndo wangewafundisha somo hawa waonevu wa demokrasia.

ukimung'unya . . . . . . . . . .ukitema. . . . . labda ni msamiati tu haina uhalisia.
 
Mkuu, hayo ya afisa usalama kwenda kwa bibi ni majadiliano?
Bibi ndo wana Mtwara? Huo ni ushawishi.
Serikali ikitaka kufanya majadiliano inaweza kufanya, lakni sio kijanja janja kwa kutuma viroboto.
Tushukuru kwamba maisha ya mtu huyo yapo salama.

Huwezi kumkejeli na kumpa maneno ya dharau mtu then, uende kushawishi badala ya kuonyesha intention to talk.
Hakukuwa na haja ya kumshambulia, badala yake ulikuwa ndiyo wakati mzuri kwao kumweleza black and white wanachokitaka, na yeye kusema anayofikiria. Na hiyo ndiyo njia za kiutendaji kazi za serikali. Huwezi kukurupuka kuitisha talk na umati wa watu kabla hujapata tips ya nini kilichopo kwenye ground.
 
Wananchi wa kijiji cha msimbati mkoani Mtwara ambako ndiko gas imegundulika, leo wameanza kupinga kwa vitendo ujenzi wa bomba la kusafirishia gas kuelekea dar baada ya kuchoma moto gari la afisa wa upelelezi kutoka ikulu jijini Dar-es-salaam. Habari kutoka kijijini hapo zinasema kwamba, intelijensia huyo alitumwa na viongozi wa ngazi za juu kuja Msimbati kumsawishi bibi kizee aliyefanya zindiko (tambiko) visima hivyo vya gas akubali kusafirishwa kwa gas na waondoke naye kuelekea Dar. Baada ya mvutano huo ndipo wanafunzi walipozingira gari hilo na kulibusha moto.....Ikumbukwe kuwa hivi karibuni kikongwe huyo aliichimbia mkwara serikali kuw hata ikitumia mabavu kutandika mabomba,gas kamwe haitofika Dar-es-salaam bali ni maji chumvi....
 
hao wananchi na huyo bibi wakapimwe akili

ndo uwezo wao wa kufikiri ulipoishia?
Kwamba huyo bibi anaweza kuzuia gesi isisafirishwe?
Kwa nini asingezuia gesi isivumbuliwe
 
Ni habari za uhakika kabisa kwamba kuna wanausalama kutoka dar na mwenyeji wa mtwara 1 walienda msimbati ili kutaka kumuua bibi kwani wametumwa na uongozi wa juu wakiamini kuua bibi ndio gesi itatoka mtwara ,hapa ndipo tunapoona uwozo na dhuluma za viongozi wetu,
na gari lao limechomwa moto ndani likiwa na silaha mbalimbali na mmoja wao amechinjwa hapo hapo.
"gas haitoki mtwara ng'oooo"
 
hiyo ni habari njema kwa wajinga hao wanaopenda kutekeleza mauaji ya raia wanaoitakia mema nchi yetu
 
Wadau samahani waliozingira gari si wanafunzi bali ni wanakijiji. (shushushu lenyewe lilikimbia na kujificha kuokoa uhai wake msako juu yake ulikuwa unaendelea)
 
Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom