mtumwa hauawi jamani......

Lizzy sidhani kama umemuelewa vizuri Bishanga huyo Cindy hajalaumu kuhusu watoto wala divorce kilichotokea ni yeye kuongea na huyo mwanaume na baada ya hapo mwanaume akachanja mbuga! Hata ingekua mimi ningejiuliza kulikoni ina maana baada ya kujua kuwa ni mtaliki na ana watoto ndio kasoro mojawapo au?
Sikatai huyo Cindy ni binadamu na anaweza kuwa na mapungufu yake kama binadamu mwingine yoyote.
well said.....
 
Last edited by a moderator:

Yalikua matamanio....huwezi kupenda picha Bishanga.
Kupenda ni pamoja kuona na kujua facts za kimaisha za mhusika, na tabia
mimi nampenda mtu arusha ltd,nitampaje RR?
 
Last edited by a moderator:
Maswala ya kulea watoto sio wako kwa wanaume ngumu kumeza.Nafuu ya huyo mimi ningezimia kabisa halafu asingejua kilichonizimisha
 
The Boss na BabuDC,ina maana mtalaka mwenye watoto hadi deserve kuwa na mwenza?

mimi sikumaanisha hivyo
na wala nilivyomuelewa DC sivyo hivyo

mimi na DC tunaona hapa kitendo cha mdada kusema ukweli mapema ni cha kijasiri
na cha akili na cha kupongezwa

na vile vile kwa mwanaume kuwa mkweli hawezi na hataki pia ni kitendo cha ujasiri na cha kupongezwa

kuliko 'wangedanganyana' na kuwatesa watoto wasio na hatia....
 
Nimepokea ombi maalum toka kwa mama chanja wangu mtarajiwa ,anasema kuna mtu kamwomba ushauri,katika hili naye anaomba mchango wenu.
Ni hivi:
Kuna mdada mmoja (tumwite Cindy), Cindy aliolewa na akaachika.Alipata watoto wawili kwenye ndoa yake na anaishi mwenyewe na wanae.Majuzi kuna baba mmoja aliingia kwenye ofisi ya dada yake Cindy (tumwite Brenda) na hapo ofisini huyo baba aliona picha ya Cindy na akamtunuku. Alijitahidi kuomba contact za Cindy lakini Brenda akawa anakataa.Jamaa king'ang'anizi pamoja na Cindy kumwambia dada yake asitoe contact zake lakini tokana na presha yajamaa mwisho Brenda alimpa jama namba ya Cindy.Zikanza simu na sms zisizoisha mpaka Cindy akakubali akutane na jamaa.Wakakutana,wakala,wakanywa,in the process Cindy akamweleza jama ukweli kuwa yeye ni divorcee with two kids.Kuanzia siku hiyo hajamsikia wala kumwona jamaa tena.
Cindy anajiuliza hivi jamaa kakimbia kisa ana watoto? Au kisa ni u divorcee?apparently dada yake kumbe hakumweleza jamaa kuwa cindy aliwahi kuolewa na ana watoto.
Hivi wanaume mnakerwa kuwa na mwanamke mwenye watoto/divorcee,kwa nini?

Ki ukweli mwanamke ukiachika na watoto lazima tuwe makini sana. Watu watakumega sana kwa promise za kuoa. Kutokana mfumo wa maisha, ugumu, shekeli zimekuwa ngumu, wanawake wenye talaka na watoto tuwe makini. Kumegwa ni kukubwa kuliko hizo ndoa.

Kwenye hili sina lawama, ashukuru mungu mlengwa kaamua kusitisha kabla hajaenda mbali.
 
mimi sikumaanisha hivyo
na wala nilivyomuelewa DC sivyo hivyo

mimi na DC tunaona hapa kitendo cha mdada kusema ukweli mapema ni cha kijasiri
na cha akili na cha kupongezwa

na vile vile kwa mwanaume kuwa mkweli hawezi na hataki pia ni kitendo cha ujasiri na cha kupongezwa

kuliko 'wangedanganyana' na kuwatesa watoto wasio na hatia....


Ahsante sana mkuu,

Tafsiri yangu ni kuwa these guys are real....no faking!!


Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: LD
asante DC
umeonesha busara mno hapa..
mwanaume anapokimbia bila kufanya 'uchafuzi'
anapaswa kupongezwa


Nashukuru sana The Boss kwa compliments....!!

Nimefikiria sana kuhusu hii story ya ndugu Bishanga na kufikia hitimisho kwamba wadau wote wawili walitumia busara ya hali ya juu sana!

Ni nadra sana binadamu (mwanamume au mwanamke) kufunguka na kumweleza mtu mambo mazito kama aliyosema Candy tena kwa mtu ambaye ameonesha interest kubwa kwake, ukizingatia kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kumwingiza chaka. Huyo dada alitafakari sana na kuona kuwa hata akisema uongo, siku moja litafumuka na linaweza kusababisha madhara makubwa kwa watu wengine, wakiwemo watoto wake na huyo mtu aliyekuwa ame-develop mapenzi kwake!

Kwa upande wa mwanamume, amefanya jambo la maana sana ambalo nimekuwa nikilieleza hapa jamvini mara kwa mara. Nimesama mara nyingi kwamba, tukiongozwa na upendo (siyo mapenzi), basi hatutakuwa tayari kuwaumiza wenzetu. Binafsi ninge-freeze baada ya kusilikiliza hadithi ya Candy na nisingekuwa tayari kuendelea na agenda zangu.. Huyo mwanamume ana sifa zote za kiume na anahitaji pongezi..Angeweza ku-fake na kujibebea mzigo kirahisi kisha kuumwaga baada ya muda mfupi...Ila busara zimemtuma kufanya uchaguzi ulio bora...He is my cute boy and a real man!!

Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: LD
The Boss na BabuDC,ina maana mtalaka mwenye watoto hadi deserve kuwa na mwenza?

Bishanga,

Hatuongelei suala na kudeserve au la, tunaongelea suala la kuwa na mwenza amabaye yuko tayari kumbema mtalaka na mizigo yake yote...Mara nyingi watu wanakuja na ajenda zao na mtu kama huyo dada anatumiwa kwama daraja tu!!

Babu DC!!
 
Ahsante sana mkuu,

Tafsiri yangu ni kuwa these guys are real....no faking!!


Babu DC!!

Dark City naomba nikuulize swali ila mtu yoyote anakaribishwa kulijibu. Hivi wewe kama mwanaume ukiwa unamtaka mwanamke(na huna uhakika kama hana bwana) ukawa kila ukimpigia simu yuko home hata iwe late(yani mida yoyote,after working hrs)hana cha weekend wala nini. Huyo mwanamke utamfikiriaje???anafaa au anaogopesha kupelekea ww uchanje mbuga lol......nataka kujua wanaume in general(ama wengi wenu)huwa mnamuonaje mtu kama huyo.
 
Last edited by a moderator:
Samahani Bishanga kwa kuchakachua sredi yako kidogo.....usijali
 
Last edited by a moderator:
Dark City naomba nikuulize swali ila mtu yoyote anakaribishwa kulijibu. Hivi wewe kama mwanaume ukiwa unamtaka mwanamke(na huna uhakika kama hana bwana) ukawa kila ukimpigia simu yuko home hata iwe late(yani mida yoyote,after working hrs)hana cha weekend wala nini. Huyo mwanamke utamfikiriaje???anafaa au anaogopesha kupelekea ww uchanje mbuga lol......nataka kujua wanaume in general(ama wengi wenu)huwa mnamuonaje mtu kama huyo.

Naomba ueleze zaidi ili ueleweke,

Kwa kili hii ya uzee, bado sijakuelewa!!

Babu DC!!
 
Bishanga,

Hatuongelei suala na kudeserve au la, tunaongelea suala la kuwa na mwenza amabaye yuko tayari kumbema mtalaka na mizigo yake yote...Mara nyingi watu wanakuja na ajenda zao na mtu kama huyo dada anatumiwa kwama daraja tu!!

Babu DC!!

Ni kweli kuliko ujibebeshe majukumu ambayo hukutarajia kukutana nayo ni bora usepe fasta!
 
Naomba ueleze zaidi ili ueleweke,

Kwa kili hii ya uzee, bado sijakuelewa!!

Babu DC!!

Mfano:kuna mwanamke umempenda na unamtaka,kila kukicha ww unampigia simu na mara zote unapomtafuta yeye huwa yuko nyumbani,ukiacha mida ya kazi(hata ukisema umtegee umpigie usiku sana atapokea na mtaongea vizuri tu na anakwambia kabisa kuwa yuko nyumbani)sasa swali langu ni kuwa mwanaume anapokutana na mwanamke wa namna hii,anafurahia au anamshangaa kuwa kwanini hajichanganyi?.
 
jamaa alishindwa nini kuwa wazi kwamba asingeweza kuendelea na uhusiano na huyo dada kutokana na situation aliyomkuta nayo... kusepa kimyakimya ni kuonyesha kwamba huna balls za ku-face reality head-on
 
. swali langu ni kuwa mwanaume anapokutana na mwanamke wa namna hii,anafurahia au anamshangaa kuwa kwanini hajichanganyi?.

inategemea preferences binafsi... baadhi yetu tungefurahi kupata mtu ambaye siyo outgoing kivile
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom