Mtumishi upo masomoni, uliomba ruhusa na mwajiri hakupitisha.

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,629
2,288
Mtumishi ameomba ruhusa, na mkuu wa idara kapitisha, ila mkurugenzi hakupitisha. Nikaamua kwenda kupiga kitabu. Ghafla nikaandikiwa barua ya utoro kazini na nikajieleza. Ni kapewa ovyo, na ofisi ya mkurugenzi ikanipa barua ya kwamba jaza mkataba wa ruhusa ya kwenda masomoni rasmi. Nikajaza, ghafla mkurugenzi tena hakusaini mkataba wakati mwanasheria na boss wangu tayari wamesaini. Mara nikakatiwa mshahara, miaka miwili ila salary slip zinakuja kila mwezi. Sina barua ya kufukuzwa kazi, je?? Nina haki ya kulipwa pesa yangu yote ya mshahara tangu nilipokuwa nasoma hadi sasa? Au sistahili.
 
Je hili la kukata mshahara pia taratibu na sheria zilifuatwa za kukatwa mshahara? Tatizo hili analo mwalimu mwenzangu, kaomba niulizie humu. Msaada please
 
Kati ya hao uliotaja kusaini barua yako Na mikataba yako nani Ni mwajiri wako? Je mwajiri wako kasaini? Kama hajasaini basi wewe n mtumishi hewa Na ulienda Shule bila ruhusa yawajiri wako.

Je ulikuwa kwenye mpango wa kwenda masomoni au nyie ndio mnabebwa Na maafisa elimu Na wakuu wenu wa Shule?

Kama umetimiza hayo mawili hapo Juu basi unastahili kulipwa haki zako, ila kama unajitambua kuwa mwajiri wako Ni DED Na sio Mkuu wa Shule au DEO.
 
Ni kwamba, barua ya kuniambia jaza mkataba ilitolewa na ofisi ya mkurugenzi, afisa utumishi akaisaini kwa niaba..!!! Yeye hataki tena kufanya kazi serikalini, ila anataka kujua hatma ya hiyo mishahara yake. In turn, ukumbuke hajafukuzwa kazi..
 
Ukiachia udhaifu mwingine wa watendaji wetu, watumishi pia tunachangia ktk matatizo tunayoyapata. Hivi unawezaje kwenda masomoni bila barua/document ya kukuruhusu? Ikiwa mtu unafahamu udhaifu wa baadhi ya watendaji wetu, iweje usipate muda wa kufuatilia mpaka upate barua? Hata shetani wakati mwingine huwa anatushangaa.
 
Mkuu umenena Si ajabu hata barua hizo kafoji, utaendaje masomoni bila mkataba kusainiwa? Unashindwaje Kufuatilia ili uondoke kialali? Atakuwa Na matatizo au alionga mkuu wake wa shule ili aende kimya kimya sasa kimenuka
 
Tatizo ni kwamba rushwa ya ngono imetawala sana mtu yupo masomani miaka yote hamalizi lakini mshahara anapata hii manispaa ya kinondoni io sana hasa hawa maafisa utumishi ninoma sana inakera wengine wanafanya kazi wengine wapo masomoni hawamalizi miaka inaenda tu
 
Yani wengi mna comments hapa nahisi si wanasheria. Mna majibu mepesi mepesi sana..!!! Yaani afisa utumishi kasaini barua kwa niaba ya mkurugenzi kumruhusu mtumishi kujaza mkataba aondoke, halafu mkurugenzi hakusaini huo mkataba, hamuoni kwamba ofisi ya mkurugenzi tayari imejichanganya?
 
Halafu nyie mnaoshangaa shangaa, mlisha wahi kufanya kazi halmashauri nyie? Hamjui hata ruhusa za masomo watu wanatoa pesa? Aya, mkurugenzi alimuomba laki tano ili aeweze kumpitishia mkataba. Na yeye hakakataa. Sasa afatilie ruhusa ya nini
 
Mtu anauliza swali la msingi mnaleta pye pyete nyingi utafikiri nyie waajiri. Haya kama nyie ndo waajiri ni nini kilishindikana kumfukuza kazi??
 
Pili kumbukeni hakuna mtu mpuuz wa kuamua kwenda masomoni pasipo barua ya ruhusa. Ina maana kafatilia akachoka, kila hatua vigingi na sababu Kibao? Kila boss analeta mbwembwe kuhusu kuruhusiwa. Mwingine utasikia anasema, kwenye vikao vya Shule huwa una maswali mengi ya kuhoji hoji, sasa hapa utatujua si nani? Halafu mtu unasema ufuatilie ruhusa, kwa model gani sasa? Mtueleze
 
Ni kwamba, barua ya kuniambia jaza mkataba ilitolewa na ofisi ya mkurugenzi, afisa utumishi akaisaini kwa niaba..!!! Yeye hataki tena kufanya kazi serikalini, ila anataka kujua hatma ya hiyo mishahara yake. In turn, ukumbuke hajafukuzwa kazi..
kwakuwa salary slips bado zinakuja maana yake ni kwamba mshahara haujasimamishwa na kwamba wewe bado ni mtumishi halali. dai mishahara yako yote ! kama mkurugenzi ni mzembe shauri yake.
 
Pili kumbukeni hakuna mtu mpuuz wa kuamua kwenda masomoni pasipo barua ya ruhusa. Ina maana kafatilia akachoka, kila hatua vigingi na sababu Kibao? Kila boss analeta mbwembwe kuhusu kuruhusiwa. Mwingine utasikia anasema, kwenye vikao vya Shule huwa una maswali mengi ya kuhoji hoji, sasa hapa utatujua si nani? Halafu mtu unasema ufuatilie ruhusa, kwa model gani sasa? Mtueleze
Ajira ni suala la kisheria hivyo kila kinachofanywa huwa kinakuwa na utaratibu ambao unaweza kuhojiwa kisheria. Kusoma ni haki ya mtumishi kama ana sifa zinazomruhusu kutumia haki yake hiyo lakini kama nilivyosema awali lazima taratibu zifuatwe. Cha msingi ni kuwa na nyaraka zote zihusianazo na suala hilo, mfano barua ya kuomba ruhusa na majibu yake kama yapo, mkataba uliojazwa na huyo mtu kama ana nakala yake...
Kama ruhusa iliombwa lakini hakupewa bila sababu basi angehusisha vyama vya wafanyakazi vimsaidie kuhakikisha kuwa anapata hiyo ruhusa. Pia ufuatiliaji wa karibu unahitajika ikiwemo kupeleka barua wewe mwenyewe na sio kuiacha masjala ukisubiri wakupelekee, hao maDED wana kazi nyingi zinazoweza kupelekea ashindwe kupitisha ruhusa yako kwa wakati, pia lazima uwepo kwenye mpango wa masomo..
Kwa suala lako ilitakiwa uhakikishe mkataba huo umesainiwa na mkurugenzi wako ndipo uwe halali maana bila hivyo ni kuwa huna mkataba (maana hata kopi yako ya mkataba itakua haijasainiwa)..kama walikataa kusaini ungeweza kwenda kutoa malalamiko yako kwa RAS ambae angeweza kumpa agizo mkurugenzi akupitishie ruhusa au hata yeye mwenyewe kukuruhusu...
Ila kwa maelezo uliyoyatoa ni wazi huyo mtu akishtakiwa kwa utoro kazini hachomoki..kuhusu salary slip hiyo haifanyi mtu kuwa mfanyakazi maana inawezekana ofisi ya utumishi walichelewa kupeleka taarifa za kufukuzwa kazi huko hazina.
Nafasi uliyonayo ni kulalamika kuwa taratibu za kukufukuza kazi hazijafuatwa (hii inaweza kukusaidia)
 
Kesi iliisha wakubwa. Tunasubiri hukumu. Ila ktk ushahidi wa mwisho, afisa utumishi aliulizwa swali, kuwa mwl. Deo mpaka sasa ni mtumishi au siyo mtumishi?? Akakiri kuwa ni mtumishi kwa kuwa hajapewa barua ya kufukuzwa kazi...!!!! Hii kesi ilisimamiwa na wakili wa labour laws kutoka Kenya.
 
Mtumishi ameomba ruhusa, na mkuu wa idara kapitisha, ila mkurugenzi hakupitisha. Nikaamua kwenda kupiga kitabu. Ghafla nikaandikiwa barua ya utoro kazini na nikajieleza. Ni kapewa ovyo, na ofisi ya mkurugenzi ikanipa barua ya kwamba jaza mkataba wa ruhusa ya kwenda masomoni rasmi. Nikajaza, ghafla mkurugenzi tena hakusaini mkataba wakati mwanasheria na boss wangu tayari wamesaini. Mara nikakatiwa mshahara, miaka miwili ila salary slip zinakuja kila mwezi. Sina barua ya kufukuzwa kazi, je?? Nina haki ya kulipwa pesa yangu yote ya mshahara tangu nilipokuwa nasoma hadi sasa? Au sistahili.
Barua hata ikisainiwa na ofisa elimu kama mkurugenzi haja ipitisha ni kazi bure kwa sababu mkurugenzi mdio mwajiri wako na ndio bosi wako namba moja. Hivyo kama ulienda ni dhahiri ulikiuka taratibu
Pili kitendo cha kuto pata mshahara na salary slip zikawa zinakuja pia nalo ni tatizo sababu inaonesha hazina inatuma pesa na bado inatambua kuwa wewe ni mtumish wa umma ,kwenye pesa hapo kuna usanii, kuna mtu ana access acount yako kinyume cha sheria.
Kuhusu kuto pewa barua ya kusimamishwa nalo ni kosa sababu pasipo barua halali wewe bado ni mtumishi na kwa kigezo hicho cha mshahara wako kuendelea kutoka ni dhahiri hawana pa kujificha.
 
Back
Top Bottom