Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
Mtukufu Ramadhani!
Date: 7 September, 2007
Masjid Qiblatain English Medium Primary School,
DAR ES SALAAM
Date: 7 September, 2007
- Bismilahi Raufu, Mhariri gazetini,
Mimi sio maarufu, hapo kwenu kilingeni,
Nataka kuwaarifu, Islamu na Misheni,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Mwezi huu mtukufu, jina lake Ramadhani,
Utende matakatifu, ninatoa ilani,
Utapata utukufu, mwisho wake duniani,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Najaribu kuhubiri, bado kupata yakini,
Imekuwa desturi, ifikapo Ramadhani,
Kutuuzia futari, bei juu magengeni,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Mwezi huu mashuhuri, asiyejua ni nani?
Biashara hushamiri, dukani hata sokoni,
Yafaa ujihadhari, unapo uza sokoni,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Kiumbe fanya nadhari, bei ziwe wastani,
Usitake utajiri, kudhulumu maskini,
Watu wote si tajiri, wanunuao sokoni,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Imekuwa staili, ifikapo Ramadhani,
Bei zenu kubadili, sokoni na madukani,
Bidhaa kuuza ghali, hata haya hamuoni,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Natoa hii kauli, AN-NUUR gazetini,
Wasikie Waswahili, walio bara na pwani,
Lanikera jambo hili, tumugope Manani,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Huo ndio ukafiri, mimi nawaambieni,
Kudhulumu mafakiri, waliojaa madeni,
Hii kweli sio siri, mimi sijui kwa nini?
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Mohammadi na kakiri, huko kwao Arabuni,
Alizifanya safari, akiwa biasharani,
Aliuza kwa kadiri, hakufanya uhaini,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma. - Katitamati shairi, Mhariri samahani,
Mungu atakusitiri, uiendeleze fani,
Na akujaze na heri, upate nishani,
Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
Masjid Qiblatain English Medium Primary School,
DAR ES SALAAM
Last edited: