Mtuhumiwa ma mauaji ya Mwangosi afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali

Yule dogo askari ashitakiwe kwa kosa la kuua, je wale wengine si washitakiwe kwa makosa ya kushambulia na kutaka kuua?. RPC naye anatakiwa kishitakiwa kwa kuchochea fujo zilizosababisha kifo na itakuwa vyema akastaafie jela.
 
Kwa hili taarifa ya tume/kamati ina kazi gani tena?? will it be tabled to the public?? Au Kova keshawakochi namna ya kusahaulisha watu?? hapa sasa unahitajika ushujaa wa watanzania tukiongozwa na wanahabar lingali la moto. Likipoa hili tumeliwa.
 
Kama wamemjua muuaji, tume ya nini? Na je wamejuaje Huyo ndiye muuaji? Hii ni danganya toto kwa serikali kukwepa hii kazia. Tutaona mwishowe Kama sio kukutwa Hana hatia.
 
Sikubaliani kabisa na kesi hii ni batili, Wanaharakati wote wanapaswa kuipinga hii kesi maana ni kuwafanya Watanzania ni wapumbavu kuliko maelezo.

Daudi-Mwangosi.jpg
Kwa picha hii hapo ndipo utajua kweli An army is a collection of fools.
 
Sasa ile kamati ya NCHIMBI na hadidu rejea uchwara itachunguza suala lenye kesi mahakamani jamani hii serikali yetu double standard kweli kweli.
 
Napata wasi wasi kama kweli mtu aliyeshtakiwa ndiye muuaji !!! Jina gani hili "PACIFICUS CLEOPHACE SIMON"full Eurocentric, kama la kutengezwa vile, halina ubini wa kibantu. Labda ndio maana hakuwa na roho ya utu !!! Lakini kwa kuwa atakuwa amesoma shule yo yote Taanzania na kuishi naye mtaani, atakuwa anafahamika. Kwa kuwa JF ni mwisho wa yote, naomba yeyote ambaye anakumbuka kukutana na jina la namna hiyo katika maisha yake aniondoe wasi wasi.
 
mtu anaitwa Pacific. haya mazingaombwe+

Nakuunga mkono Mkuu. Na kwa kuwa JF ni mwanzo na mwisho, je, kuna mwana JF yeyote alishakutana na huyo Mkaka iwe ni shuleni, kanisani, msikitini, michezoni, CCP, bar au sehemu yoyote hapa duniani ? Kama kweli ni jina halisi lazima tutakuwa tumeisha kutana naye hata mtaani kabla hajahamia Baracks.
 
No please...
Mshitakiwa wa kwanza alitakiwa kuwa RPC Kamuhanda, akifuatiwa na RCO na huyo muuaji pamoja na wale wengine sita kama wanavyoonekana kwenye picha mbalimbali zilizopigwa wakati wakimtesa Mwangosi.

Kutomshitaki Kamuhanda katika tukio hili la mauaji ya Mwangosi ni sawa na kuiminya haki ya marehemu na kuwatukana watanzania kwa ujumla wao.

Asante kaka.

Ina maana tayari kuna watu washasahau mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya Mwangosi ni nani?
 
sijaridhika na hatua iliyochukuliwa,wanapaswa wote walioshiriki kumua mwandishi wapandishwe kizimbani ,wakwanza huyo RPC wa iringa.
 
RPC si shahidi, bali ni 1.Mshukiwa 2. Mtuhumiwa na 3. Mshitakiwa, kwa hatua hizi tatu hatakiwi kujibu lolote......NI HIGH COURT KWA JUDGE TU.
 
Mnaenda kupigwa chenga ya mwili,
ataenda kupimwa akili na kuonekana ni mgonjwa wa akili, mahakama itamuachilia huru.

Hata atakayoyasema mahakamani itakuwa ameongea kichaa, changamkeni kupigania kamuhanda aunganishwe pamoja na wanzake nane kwenye mashtaka haya.
 
Jamani hivi Chagonjwa atafanywaje kwa kuudanganya umma kuwa eti bomu lilirushwa tokea upande wa wafuasi wa CDM?
 
Back
Top Bottom