Mtu yeyote atakayetaka kulindwa na polisi wakati anakwenda benki atoe elfu 10

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Bank.png

Jeshi la Polisi limesema mtu yeyote atakayetaka kusindikizwa na polisi kwenda kuchukua fedha nyingi benki, anaruhusiwa kwa kulipia Sh 10,000 au Sh 20,000.

Unakionaje kiwango hicho cha ada, kikubwa au kidogo sana?

==========

MBINU ZA KUJIHAMI NA UJAMBAZI WA BENKI

Kamanda Sirro alisema iwapo kuna mtu yeyote anataka kubeba kiasi kikubwa cha fedha, ni vema akatoa taarifa kwa jeshi hilo kwa kufuata hatua zifuatazo:

1. Mtu yeyote anayetaka kwenda kuchukua fedha nyingi benki atoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ili apate ulinzi.

2. Unaruhusiwa kulipia Sh 10,000 au Sh 20,000 ambapo utapewa askari mwenye silaha ili akulinde.

3. Toa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi unapohisi kuna dalili ya tukio la kuvamiwa.

4. Epuka kupanda bodaboda pindi unapokuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

5. Kutumia njia mbadala ya kuchukua fedha benki ili kuepuka uhalifu huo.
 
Hiyo hela ni kidogo kutokana risk involved. Kuna haya makampuni ya ulinzi nafikiri nayo huwa yanatoa huduma hii ya kusafirisha hela...sina hakika na gharama zao.
 
HUYO POLISI MWINGINE NI JIRANI YANGU ,,,JAMAA YUPO PEACE SANA ,,,,NADHANI NOW YUPO KISUTU MAHAKAMANI;; sa kwa mfano unataka kusindikizwa ukaweke milioni let say million #50_ ,,,utawapa kumi elfu kweli
 
[QUOToto halali na hela, post: 15097065, member: 96921"]Kama nachukua milion zaidi ya moja labda[/QUOTE]
Hiyo gharama ipo siku nyingi tu ila kuna mlolongo kibao hadi upate huduma hiyo na kuna hiden cost kibao, bado usafiri sio unampakiza kwenye daladala, au mkatishe kwa miguu.
 
Nani kwanza mwenye imani na hao Polisi ???? Mimi naona nikumpa mfupa fisi tu
 
Back
Top Bottom