souljah meditater
JF-Expert Member
- Oct 15, 2012
- 2,146
- 2,094
Bado unarudia "mweusi", nimesema; Uarabu si rangi ya mtu, uarabu ni lugha.
Sasa sijuwi ni nani alikujaza ujinga kuhusu Waarabu kuwa si weusi pia.
Mkuu tupe fact kuhusu Waafrika au mtu mweusi kama uzi unavyosema sababu historia ya waarabu ipo wazi ila leo ulimwenguni kuna watu wanaojinasibisha na Waarabu kwa sababu hizi zifuatazo:
- Kila anayeishi katika nchi ya Kiarabu na kuwa na uraiya wa nchi ya Kiarabu
- Kila anayezungumza Kiarabu na kufuata mila na ada za Kiarabu
- Kila ambaye anajua kuwa asili yake na ya wazee wake ni Waarabu hata ikiwa hajui Kiarabu
1- Waarabu (Al-Baida): Nao ni Waarabu ambao leo hawako tena ulimwenguni kwa sababu ni kaumu zilizoangamizwa na Mwenyezi Mungu baada ya kukataa kufuata maamrisho yake na kwenda kinyume na Mitume yao, nao ni: Kaumu ya Hud ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la A'ad, na kaumu ya Saleh ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Thamud. Kaumu mbili hizi ziliangamizwa na Mwenyezi Mungu kwa kumuasi na kutofuata amri na maelekezo ya Mitume yao, na waliobakia katika makundi haya mawili ndio waliokuja kufanya makundi ya Waarabu wanaojulikana kwa jina la Waarabu (Al-A'ariba).
2- Waarabu (Al-A'ariba): Nao ni Waarabu waliotokana na mtoto wa Nabii Hud (AS) ajulikanaye kwa jina la Qahttaan na kutokana na kizazi chake ndio hawa Waarabu wanaoitwa Al-A'ariba wakaenea kila upande. Waarabu hawa ambao makabila yao makubwa wakati huo yalikuwa ni Himyar na Kahlaan walikuwa wakiishi Yemen na kuwa na ufalme na ustaarabu mkubwa mpaka yalipotokea mafuriko makubwa hapo Yemen yakawatawanya na kuwasukuma kwenda sehemu nyengine mbali mbali za Bara Arabu na Shamu na Iraqi na Misri na Afrika Mashariki.
3- Waarabu (Al-Mustaariba): Nao ni Waarabu waliotokana na Nabii Ismail (AS) ambaye aliletwa na babake Nabii Ibrahim (AS) na kuwekwa katika bonde la Makka pamoja na mamake Hajar na kuachwa hapo kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Nabii Ismail hakuwa Mwarabu lakini baada ya kukaa hapo Makka na kutifuka chemchemu ya Zamzamu, walikuja Waarabu wa Kiyemeni wa kabila la Jurhum na walipoona maji hapo waliomba kubakia hapo na ndipo Nabii Ismail akakulia kwenye kabila hilo na kujifunza Kiarabu na kuoa katika kabila hilo. Kwa hivyo, kizazi chake kiliinukia kuwa Waarabu kwa kuchanganyika na kabila la Waarabu na wakawa wanajulikana kama Waarabu Al-Mustaariba.