Huyu Eddo Kumwembe.
Huyu Edo Kumwembe jinsi anavyonikoroga mimi katika makala zake Fulani Fulani ni hivyo hivyo angemkoroga na Advocate Kumwembe, nimeisha muonya mala nyingi lakini mbishi, hasa katika suala la kuwalinganisha King Pele na eti akina Messi na mwenzie Ronaldo.
Niliisha mueleza usiwalinganishe hawo vijana na wazee kama akina Pele katika suala la kusakata gozi la nyamafu watu hao wala hawakalibiani, kwa nini huyu kijana mbishi? Mfano katika gazeti la mwanasporti toleo No.1623 la jumamosi tarehe18-19 ukurasa wa 17 katika makala yake nyuma ya pazia Miaka 10 ya Messi Barcelona nyuma ya pazia, amenikera, amenikera, amenikera. Anasema eti nani amemona Pele akicheza, anajibu yeye Hapana , pia Diego Maradona na wengine.
Mimi wachazaji wote uliowataja nimewaona na pia ninaendelea kuwaona wachezaji wa sasa ambao mnasema ni wa kizazi kipya. Nasema hakuna wa kuwalinganisha na akina Pele, hawafikii hata robo. Kwanza huyo Ronaldo hana kipaji chochote zaidi ya mambio afadhari hata Messi.
Tafauti zao kubwa ni hii ifuatayo, kwamba Pele angerudi katika enzi zake anaweza kabisa kucheza na walinzi(Defence) ya wachezaji wa sasa, wakati Messi au Marodana hawawezi kabisa kucheza na walinzi waliokuwa wanamkaba Pele, kwa hakisa akina Messi au Ronaldo wangekutana na walinzi wa akina Pele au wangevunjika vipande vipande au wangeacha kabisa kucheza. Pele angeweza kucheza kipindi hiki cha kizazi kipya lakini Messi wa sasa akutane na walinzi wa zamani haweizi kabisa kufurukuta.
Mfano Mwalimu wa sayansi anaweza kufundisha masomo ya art, wakati mwalimu mahili wa art hawezi kufundisha masomo ya sayansi sasa nani zaidi?
Au Sisi tuliosoma zamani pamoja na advocate Kumwembe tulikuwa tunauwezo wa Ku-calculate Quadratic equation kwa kutumia njia nne yaani Kufactorise, Kutumia master formula, kucomplete the square na kutumia graphing method kwa kutumia rogarismic table wakati hawa akina Edo Kumwembe ambao wanatumia scientific calculator hawawezi kabisa kutumia hizi njia mbili za mwisho, kwa hili sitaki ubishi nimeisha wajaribu sana, sasa jee, katika ya sisi na hawa wanaotumia nyenzo na zaidi? Wakati mimi nikitumia Calculator itakuwa kama nakula nyama ya ubongo tu wenyewe wape Log table hawawezi hata kuitumia sasa je Nani zaidi?
Hebu pimeni kutumia jedwali lifuatalo halafu mumweleze Eddo Kumwembe:-
Edo Kumwembe nakuonya kwa mala ya mwisho usiwalinganishe Pele na Messi au Ronaldo ni ukosefu wa adabu mulio karibu na yeye mumwabie.

Kigezo | King Pele | Christiani Ronaldo |
Umri wa kuanza kucheza world cup | Miaka 17 | Ameanza kijeba |
Maback(walinzi) | Walikuwa wanapiga kiatu bila huruma lakini Pele aliweza kucheza | Walinzi wamedhibitiwa kwa sheria kali za kuwalinda mastaa |
Viwanja | Vilikuwa vibovu hata hivyo Pele alikuwa anacheza | Viwanja vimeboreshwa sana kiasi unaweza ukasota hata mita 10 |
Ustadi (skills) | 1 A.Mfalme na muasisi wa style zote 1.Tik-taka 2.Guard Muller (zile alikuwaakipiga Tony Yeboah) 3.Scorpion kick 4.Biycle kick ( alikuwa akipiga Bebeto) 4. Vichwa 5.Free Kick B. Alikuwa anatumia viungo vyote na miguu yote pia mpira uje vyovyote anaumiliki, anaweza kukimbia na mpira ukiwa mbele, nyuma , kichwani hata mgogongoni. | Hana jipya ni mambio tu kama anafukuza paa. B. Ni mpaka uje kwa mbele tu ndipo akimbie nao nyuma ni mpaka ageuke.Anatumia miguu tu kudrible. |
Kucheza Ulaya | King Pele hakuwahi kucheza ulaya kwa sababu alikuwa ni nyara za serikali. Bunge la Brazil lilikaa likaamua Pele hauzwi kwa bei yoyote ni shara ya serikali mpaka alipostaafu ndipo alienda kucheza Amerika (USA) | Amecheza Ulaya kule ndipo akina Edo Kumwembe wanamwona sana na kudhani yeye ni mchezaji . |
Mabao | 1300 katika mechi za kimataifa | Hata nusu ya Pele hafikii. |
Kombe la dunia | Amecheza mala 4. 1958,1962,1966 na 1970 kati ya hapo amenyakua ndoo mala3 na mchazaji bora 1970. | Ameenda mala 3, 2006, 2010, na 2014 mala zote ameenda kuuza magazeti na sura tu. |
Ukipekee (unique) | Akiwa na club chake cha Santos huko Columbia Pele alifanya rafu mbaya ya kulipiza kisasi akapewa kadi nyekundu , lakini uwanja mzima uliikata kadi hiyo matokeo yake refa akatolewa Pele akaendelea na mchezo. Hajawahi kufanyiwa mchezaji mwingine tena jambo hilo | Sijui, labda Edo Kumwembe anafahamu. |