Mtu Anapochemsha kwenye Interview ndo kusema hawezi kufaa kwenye hiyo post

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,943
Greetings
Mara nyingi nimeona watu wengi wakihudhuria interview zaid ya kumi na hawapati kazi na wakati huo kuna wengine wanahudhuria interview moja tu na wanapata kazi. nikawa najiuliza maswali mengi na kutokupata majibu sahihi. wakati mwingine nilifikiri labda ni mkono wa mtu ndo maana wengine wanashindwa kupata kazi.

Naomba ufafanuzi kutoka kwa wanajamii. Hivi inawezekana mtu akawa na vigezo vyote vya kupata kazi na akawa amewashinda wengine lakini siku ya interviewkutokana na uwoga na wasiwasi akashindwa kufanya vizuri katika ule usaili. Je kwa kigezo hicho tu ndo kinaweza kumfanya mtu huyo kukosa kabisa kazi hiyo
 
ndugu yangu kwenye hilo naona kuna tatizo sana hasa kwenye nchi za kiAfrika, ukweli uliopo asilimia nyingi ya watu wanapoomba kazi huwa wanajua nini wanataka ila tatizo la interview watu wengi kwanza hatuwezi kujielezea licha ukiwapa kazi wanaijua sana, hilo linaendana na uzoefu wa kazi hivyo vyote ni vigezo vya kubebana katika ajira
 
'Kuonekana' ndio nini?

Mkuu Mbona unauliza maswali ya ajabu ajabu wakati umeshapewa ufafanuzi wa swali? Manake huwa kuna kasumba za ajabu kana kwamba interview ndiyo kipimo pekee cha kumpatia mtu ajira.
 
Ofcoz sijakujibu ila kama huna cha muhimu cha kuandika piga kimya wenye maoni ya maana watoe.

Hivi wewe ni nani unayeamua maoni yepi ni ya maana na yepi si ya maana? Kwani umelazimishwa kusoma ninachoandika? Unachangia kulipia bandwidth? au kiherehere tu kama binti aliyevunja ungo?
 
Bwana Kabila01,nashuruku kwa hoja yako,kushindwa kwa watu kunatokana na sababu nyingi ambazo siyo lahisi kuzieleza yote:-

1.Maandalizi duni,hasa mtu asipokuwa amejipanga kuangangalia maeneo yote ambapo kuna uwezekano wa maswali kutokea wakati wa usahiri.
2.Mtu shindwa kuuliza maswali watu wanaomfanyia usahiri,hasa asipo elewa swali aliloulizwa,kwa kuogapa uenda ataonekana hajuia au sumbufu.
3.Kushindwa kuonyesha kujiamini wakati anapojibu maswali,hapa naimanisha kujiumauma
4.Mtu unapopewa nafasi ya kuuliza maswali na kushindwa kuuliza,hilo nalo huwa ni sehemu ya kupima kwa kiasi gani unajiamini,hivyo kutouliza kitu kunaweza pia kuonyesha kwa kiasi gani hujiamini.
 
hivi wewe ni nani unayeamua maoni yepi ni ya maana na yepi si ya maana? Kwani umelazimishwa kusoma ninachoandika? Unachangia kulipia bandwidth? Au kiherehere tu kama binti aliyevunja ungo?
mkuu umeishiwa points....AU kama vile viswali vyako ulikuwa unataka kuhit kwenye point fulani basi nenda moja kwa moja kwenye point
 
mkuu umeishiwa points....AU kama vile viswali vyako ulikuwa unataka kuhit kwenye point fulani basi nenda moja kwa moja kwenye point

Wewe unaacha kufanya yanakuhusu unaanza kuleta porojo na upumbavu. Kama nimeishiwa point lete pampu ya point basi tuzijaze hizo point..
 
Wewe unaacha kufanya yanakuhusu unaanza kuleta porojo na upumbavu. Kama nimeishiwa point lete pampu ya point basi tuzijaze hizo point..

Mheshimiwa nia yetu sio kukukasirisha manake hatujui umeamkaje.....ila kwa jinsi unavyokurupuka inaonyesha hizo hasira umezitoa sehemu nyingine ......
 
Mheshimiwa nia yetu sio kukukasirisha manake hatujui umeamkaje.....ila kwa jinsi unavyokurupuka inaonyesha hizo hasira umezitoa sehemu nyingine ......
Sikiza wewe gret sinker, kama huna la kuongezea kaa pembeni..hivi ni nani amekwambia nimekasirika? Hebu lione kwanza..
 
Mazee maswali yangu kama ni ya ajabu yaache kama yalivyo sijakuomba uyajibu. Ebo!
Hivi wewe ni nani unayeamua maoni yepi ni ya maana na yepi si ya maana? Kwani umelazimishwa kusoma ninachoandika? Unachangia kulipia bandwidth? au kiherehere tu kama binti aliyevunja ungo?
Wewe unaacha kufanya yanakuhusu unaanza kuleta porojo na upumbavu. Kama nimeishiwa point lete pampu ya point basi tuzijaze hizo point..
Sikiza wewe gret sinker, kama huna la kuongezea kaa pembeni..hivi ni nani amekwambia nimekasirika? Hebu lione kwanza..
god_test_sad%20face.jpg
 
Nilipofungua nimekuta ni mada nzuri sana na ambayo kwa namna moja ama nyengine inatugusa watu wote ambao tupo katika soko la ajira na wengine ndio wanaingia lakini baadhi ya wachangiaji katika hili wamejitahidi kwa kila namna kuhakikisha kwamba xhii mada inapoteza maana. Kama una moyo mwepesi ukisoma 'post' tano tu katika hili unaacha.

Hayo tukiyaweka kando, kwa mtazamo wangu suala la usaili ni tata mno hasa inapokuja katika kuchagua ni nani ambaye amefanya vizuri katika huo usaili na ni yupi anakuwa amefanikiwa kupata nafasi. Kitu kikubwa kinachopelekea watu wengi kushindwa ni kutokana na kushindwa kujieleza katika usaili. Unakuta mtu ukisoma CV yake ana kila kitu kinachomfanya awe likely candidate lakini inapokuja kwenye kusailiwa anakuangusha vibaya sana.

Kuwa na vigezo vyote vya kupata kazi tu haitoshi, bali unatakiwa pia kuwa na uwezo wa hali ya juu katika kujieleza in person ni what you have put down kwa CV yako. Katika interview ni pahala ambapo mtu unakuwa 'unajiuza' mwenyewe na kama ambavyo kila siku utasikia watu wanasema Biashara Matangazo... sasa katika interview wewe unakuwa ni bidhaa ambayo unainadi ili inunuliwe. Wengi wanashindwa katika hili.

Kingine ni lugha ya mawasiliano. Watu wengi wanapoingia katika interviews huwa inawawia vigumu sana kuweza kuongea lugha fasaha itakayoeleweka na hii nadhani inaletwa na kasumba ya kwamba kila interview ni lazima mtu uongee Kiingereza. Depending na nani ambaye atakuwa anakuhoji, unaweza tumia lugha ambayo unadhani utawa comfortable zaidi rather than kung'ang'ania lugha usiyoielewa vizuri itayosababisha ufanye vibaya katika hilo. Hii pia inategemea kama imewekwa wazi kwamba lugha ya mawasiliano iwe kiingereza ama hapana.

Kigezo cha mwisho ni Interviewers. Kwa kiasi kubwa huwa wana machaguzi yao so inakuwa shida kukubaliana na wewe in the first place... Especially kama ulivurunda!!!~
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom