Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
- Thread starter
- #21
Mkuu hapo kwenye Red, mama yake na wewe wote ni wazazi tu, kama wewe ulishindwa kama mzazi basi hata mama kama sio mwalimu wa primary hataweza, labda kama angekuwa mwalimu. Mimi mwenyewe mama na siwezi kufundisha wanangu, huwa tunaishiana kufinyana na kumwambia akalale hata kama katoka kuamka. maana sometimes nahisi kama hataki kusoma ili akacheze, kwa hiyo adhabu huwa kama hutaki kusoma basi na kucheza hakuna. kwa kweli inaumiza sana mtoto asipofanya vizuri, na hasa kama unaamini angeweza kufanya vizuri akiongeza juhudi.
Nimekupata mama. Binafsi naamini anaweza kufanya vizuri zaidi ya hapo. Yaani hajaweka nguvu zote hadi ile chembe ya kwenye mkia ili tubwage manyanga. Ushauri wako tutaufanyia kazi.
hii inategemea ww baba ulikuwaje enzi hizo kwenye Hisabati!
Kama ulikuwa unakuna kona vipindi vya hesabu basi umemwambukiza hata mke wako nae jaribu kuulizia kama alikuwa fit kwenye hisabati labda kachukua kipaji cha mama yake.
Naogopa kuingia kwenye mitego ya kujimwagia misifa hapa jamvini. Labda niseme tu kuwa wote (mimi na mama yake) tunaweza kwa kiwango cha kawaidia kufanya hesabu especially zile za primary
Mwambie "troublesome, crack headed halfcast from Harare" will come get him if he doesn't do his homework...lol!!
Hapo si ndo tutamharibu kabisa?
kabla sijatoa ushauri wangu niambie mwanao anajua kuhesabu hadi ngapi?
nikutahadharishe kuwa watoto ni saikolojia tupu......... hata unapoongea naye kuna vitu huwa anakuambia unashindwa kusikia kwa sababu ya kushindwa kumsoma saikolojia yake...........
naanza kwa kukupa kitu kimoja unachoweza kuona cha kipuuzi lakini kizingatie, halafu ukinielewa, uende kumwelekeza na mwanao, kama umeanza kumkaririsha tebo tafadhari sitisha kwanza hadi tutakapokuwa tumeelewana namna ya kumuelekeza kujifunza hesabu..........
step 1:
nakushauru usome avatar ya fixed points, halafu ujaribu kufumba macho na ujaribu kuweka namba mbalimbali kufuatana na mtiririko wa kuhesabu kwenye mistari ya mchoro wa ile avata bila kuitazama............. kisha fungua macho uone jinsi ulivyoweka namba zako na umbile linalojitokeza ukiziunganisha hizo namba kwa mstari............. hesabu idadi ya pembe/kona zinazotokea, angalia kama umbo liko katika sura inayoeleweka ama la.......... usijaribu kulazimisha umbo lako lifanane na lile la avatar ya fixed point na wala usisahihishe ukigundua halifanani na wala usichungulie avatar wakati ukiandika namba zako hadi umemaliza kuziandka......... na ukimaliza, kazi a avatar inakuwa imekwisha............. tuanaingia hatua nyingine...........
ukimaliza hilo zoezi, kabla hujaongea na mtoto niPM nitakupa hatua inayofuata yaani step 2..............
Mkuu hiyo homework imenishinda. Kichwa kime-jam. Kama una ushauri mwaga tu. Tutakushukuru mkuu.