Mtoto wa wangwe awashutumu viongozi wa CHADEMA kwa kuwatelekeza

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Heshima Mbele,

Kwa mlio Nyumbani na ambao mmeweza kusoma gazeti la leo la Mwananchi naomba mtupe habari zaidi sababu mie nimepewa kwa kifupi tu na Mhariri wa Gazeti moja la Nyumbani.Habari hiyo inahusiana na mahojiano kati ya gazeti la Mwananchi na zakayo wangwe kuhusiana na kutelekezwa kwa familia yao na viongozi wa CHADEMA.

Inasemekana kuiwa toka Baba yao afaruiki hakuna hata kiongozi mmoja wa CHADEMA ambaye amekwenda kuwaona wala kuwasalimia nyumbani kwao.Zaidi ya yote hata hawajapewa msaada wa kifedha.

Pia imemfanya yeye na wezake wahame kwenye nyumba walioku wakipnaga na kuhamia Hosteli.

Kijana huyo pia ameeleza jinsi CHADEMA walivyomtenga baba yao kwa kumsingizia maneno ya uongo ikiwamo kuvujisha siri za Chama ili khali wangwe alidedicate muda wake mwingi ndani ya CHADEMA.

My TAKE:
1.Siyo kazi ya CHADEMA kusaidia watoto wa Marehemu,ila kama Chama hawana utaratibu wa kuwaenzi watoto wa watu ambao walijiotolea kuwa viongozi?

2.Hakuna mafao yoyote ambayo marehemu wangwe alitakiwa kupewa kama Makamu mwenyekiti wa CHADEMA?haya yangeweza kusaidia familia yake kwa sasa.

3.Je sisi kama JF hatuoni kuna haja ya kuwachangia watoto wa Marehemu wangwe ili kuwatia moyo wale wote ambo watakuwa wakiendesha Mapambano ya kisiasa?
 
Familia ya wangwe inajiweza sidhani kama huyo mtoto malalamiko yake yamebarikiwa na familia yake -- ntaongea na dadake
 
Mafao yake yanapatikana bungeni,
Sidhani kama kuna katiba ya chama chochote inayosema kiongozi wake aakifariki anapewa mafao
 
Ni kweli kabisa kama hawamjulii hata hali itakuwa wanafanya vibaya na watakapoona tangazo hili wajirekebishe kwani kuna tabu gani ,ikiwa wanapokea mshara wa mamilioni na posho kibao ,wanaweza angalau kwa muda fulani ikawa wanatenga kiasi fulani cha fedha na kuwatilia ,japo pale kijijini kwao au wakajenga japo zahanati ndogo kama kumbukumbu ,ni maendeleo fulani ndani ya chama na yatazidi kuwajengea na kuwapa moyo wengine wawe mstari wa mbele katika kutetea haki za wananchi msiwe kama Sultani CCM akishakuchoka anakutupa nje hata akikuona unavaa kanda mbili basi hakuulizi ,wangapi wamefanya kazi ndani ya CCM na serikali zake hadi leo hawajapewa mafao wala hakuna dalili kama watalipwa ,na ukienda kudai wanakuitia polisi wao.
 
Heshima Mbele,

3.Je sisi kama JF hatuoni kuna haja ya kuwachangia watoto wa Marehemu wangwe ili kuwatia moyo wale wote ambo watakuwa wakiendesha Mapambano ya kisiasa?

Wewe kaka wewe hili unalionaje? na umeshatoa msaada wowote kwa hii familia? (sihitaji kujua aina ya msaada).
 
Hi Wana JF,

Habari hii imetokana na mahojiano na mtoto. Je huyu mtoto ndiye aliyeachwa kama mrithi wa kuangalia familia? Kama sivyo amewasiliana kwanza na mwakilishi wa familia ya marehemu baba yake kabla ya kutoa malalamiko gazetini? Nijuavyo mimi Marehemu Wangwe alikuwa na wake zaidi ya mmoja na watoto wake vile vile wamezaliwa na mama tofauti sasa sijui kama huyu ni mtoto wa mke yupi kwa sababu hapo siku za nyuma kidogo Chadema kama chama kiliwahi kumkataa mmojawapo kama mke wa marehemu kwa kuwa hakuwahi kutambulishwa kwenye chama.

Ingawaje inawezekana kiutu Chadema inapashwa kufuatilia na kujua maendeleo ya familia ya marehemu Wangwe, sijui kama huu ni wajibu kwa chama.

Tiba
 
Wabunge Tz wanaofariki kama Watz wengine ni wengi tu!

Je Vyama vya siasa ndo vina wajibu kuwaangalia hawa watoto?

Kwani Mtz wa kawaida akifariki utaratibu wa kuwaangalia watoto vipi?
 
Umesahau hawa walisongwa songwa na chama chako mpaka wakawa wanaongea maneno mbofumbofu juu ya CHADEMA na mama yao mdogo.
 
Jamani mwee, hawa waandishi wa habari jamani heee!.. Mbona wanashindwa kumwacha marehemu apumzike kila siku wanakuja na maneno ya ajabu ajabu..

Hivi kweli kuna Utaratibu wowote kwa wototo wa Nyerere kupewa fedha au heshima kutokana na Mamlaka ya baba yao?..Kwa nini asianzie huko ili tupate mtililiko wa haki za mirathi ya Usultan (Royal) kwa watoto wa viongozi..

Hivi kweli leo hii mpiganaji Mkandara akiondoka duniani JF au Chadema inalazimika kusaidia familia yangu...huu Usultan umetoka wapi jamani..

Watoto wa Marehemu watarithi kile marehemu aba yao alichowaandalia, sio kazi ya chama wala serikali kuhakikisha kwamba maisha ya kizazi cha marehemu wanaishi vizuri..

Ama kweli waandishi wengine jamani...mkikosa habari basi huzitafuta mkazitia nakshi ya udi na Uvumba!..
 
My TAKE:
1.Siyo kazi ya CHADEMA kusaidia watoto wa Marehemu,ila kama Chama hawana utaratibu wa kuwaenzi watoto wa watu ambao walijiotolea kuwa viongozi?

2.Hakuna mafao yoyote ambayo marehemu wangwe alitakiwa kupewa kama Makamu mwenyekiti wa CHADEMA?haya yangeweza kusaidia familia yake kwa sasa.

3.Je sisi kama JF hatuoni kuna haja ya kuwachangia watoto wa Marehemu wangwe ili kuwatia moyo wale wote ambo watakuwa wakiendesha Mapambano ya kisiasa?

Matumizi mabovu ya masters yako!
 
3.Je sisi kama JF hatuoni kuna haja ya kuwachangia watoto wa Marehemu wangwe ili kuwatia moyo wale wote ambo watakuwa wakiendesha Mapambano ya kisiasa?

Mkuu Gembe, kuna waTZ kibao ambao walikuwa katika mapambano na wamefariki. Vipi watoto wao?, ama kuwa katika mapambano mpaka uwe Kiongozi wa Chama tu?. Wapiga kura na wafuasi wa vyama wasio na vyeo hawako katika mapambano?.
 
- Unless kuna contract iliyosainiwa na marehemu baba yake kuhusu mafao kwa watoto wake kutoka Chadema, huyu kijana apewe shamba na jembe tu i mean wanasota wa Mwalimu, itakwua yeye? Duh!

FMES!
 
- Unless kuna contract iliyosainiwa na marehemu baba yake kuhusu mafao kwa watoto wake kutoka Chadema, huyu kijana apewe shamba na jembe tu i mean wanasota wa Mwalimu, itakwua yeye? Duh!

FMES!

Duh! I love JF!

Huku ndiko kumkoma Nyani bila kumwangalia usoni!
 
Back
Top Bottom