Mtoto wa mwisho hafai kuoa?

Masaki

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,463
752
Jamani kuna hii theory kwamba msichana ambaye ni wa mwisho kuzaliwa nyumbani kwao mara nyingi huwa anakuwa amedekezwa sana kwa hiyo hafai kuolewa. Hafai kuolewa kwa sababu anategemea kuendelea kudekezwa kupita kiasi hata kwenye ndoa na kusahau kwamba mume si mama au baba yake.

Kama kuna mtu yeyote ana uzoefu na hili tafadhali, maana mwenzenu maji yako shingoni!
 
wewe bwana acha uwongo..
km nampenda oa ustafute vsababu mbuz apa

nan anafaa sasa?
wa kwanza?
mmh....

wat if kazaliwa peke yake?
 
Sidahani kama ina uhalisia kivile.....Kama ishu ni kudekezwa, then inaweza kuwa ni mtoto wa namba yoyote ile na sio lazima wa mwisho. What if ni familia ya watoto wawili tu (wote wasichana au wa kwanza msichana), au ni familia ya watoto kumi wote wa kiume isipokuwa mmoja wa kwanza ndio msichana!
 
wewe bwana acha uwongo..
km nampenda oa ustafute vsababu mbuz apa

nan anafaa sasa?
wa kwanza?
mmh....

wat if kazaliwa peke yake?

Hilo la kuzaliwa peke yake nalo neno. Ila mtoto mwenzenu hizi kesi za mtoto wa mwisho kwao nimekutana nazo hii ni mara ya pili sasa. Same stuff, yaani huwa wanajiona kama malaika. Hawajui kusema SORRY kwa kuwa muda wote wanaamini wao wako sahihi, wanaamini huwa hawakosei kwa kuwa wazazi wao hawakuwa wanawakalipia kwa jambo lolote lile.

Na ukimwambia amekosea ananuna hata wiki mbili.....!!
 
wewe bwana acha uwongo..
km nampenda oa ustafute vsababu mbuz apa

nan anafaa sasa?
wa kwanza?
mmh....

wat if kazaliwa peke yake?

Rose I support you; mfano watu wameamua kuzaa kwa mpango akazaa first born mwanaume na second msichana ina maana huyu msichana hafai kuolewa kwa nini?
Mimi nina mvulana na msichana na hakuna kudekezwa wote wanapata equal treatments including bakora with some special consideration kwa binti. Sasa labda atutafsirie kudekeza maana yake nini?
 
Sidahani kama ina uhalisia kivile.....Kama ishu ni kudekezwa, then inaweza kuwa ni mtoto wa namba yoyote ile na sio lazima wa mwisho. What if ni familia ya watoto wawili tu (wote wasichana au wa kwanza msichana), au ni familia ya watoto kumi wote wa kiume isipokuwa mmoja wa kwanza ndio msichana!

Mara nyingi mtoto wa kwanza hujikuta akibeba majukumu bila kupenda pale wadogo zake wanapozaliwa. Na mara nyingi hutaka kuonyesha kwamba yeye ni mkubwa. Kwa hiyo huacha kujiendekeza na kujidekeza akiwa katika umri mdogo!
 
Jamani kuna hii theory kwamba msichana ambaye ni wa mwisho kuzaliwa nyumbani kwao mara nyingi huwa anakuwa amedekezwa sana kwa hiyo hafai kuoa. Hafai kuoa kwa sababu anategemea kuendelea kudekezwa kupita kiasi hata kwenye ndoa na kusahau kwamba mume si mama au baba yake.

Kama kuna mtu yeyote ana uzoefu na hili tafadhali, maana mwenzenu maji yako shingoni!

kwa tamaduni za kiafrika msichana anaoa au anaolewa???? Nimeshindwa kukuelewa kabisa
 
Rose I support you; mfano watu wameamua kuzaa kwa mpango akazaa first born mwanaume na second msichana ina maana huyu msichana hafai kuolewa kwa nini?
Mimi nina mvulana na msichana na hakuna kudekezwa wote wanapata equal treatments including bakora with some special consideration kwa binti. Sasa labda atutafsirie kudekeza maana yake nini?

Kudekeza ni pale ambapo mtoto analelewa kama yai. Yaani hafokewi hata akikosea. Anabembelezwa hata pale ambapo alitakiwa kuomba msahamaha. Yaani kwa kifupi mtoto anakuwa anaamini kwamba yeye yuko perfect na huwa hakosei kwa kuwa wazazi wake hawajawahi kumwambia kwamba anakosea.

Hii inatokea mara nyingi sana kwa watoto wa mwisho kwa kuwa wazazi huwa siku zote wanawaona ni wadogo hata baada ya kubalehe.
 
he ancle ,inaa mana mimi sifai kuolewa? bcz mm ni last born as well.. lakin nahis tabia za watu haziendani kwa kuzaliwa zinaendana na malezi ,, nahsi hivyo ,
 
Jamani kuna hii theory kwamba msichana ambaye ni wa mwisho kuzaliwa nyumbani kwao mara nyingi huwa anakuwa amedekezwa sana kwa hiyo hafai kuolewa. Hafai kuolewa kwa sababu anategemea kuendelea kudekezwa kupita kiasi hata kwenye ndoa na kusahau kwamba mume si mama au baba yake.

Kama kuna mtu yeyote ana uzoefu na hili tafadhali, maana mwenzenu maji yako shingoni!

Hawa hawafai kabisa

Akiunguza maharage ukimsema kwa nini yameungua anakimbilia kwa wazazi wake.

Ukimnyima pesa ya saloon kosa anaenda kwa baba ake kumwambia hawa bana hawafai.

Usipo mbembeleza tu ni kosa kubwa anakwambia kwa baba na mama nadeka napewa kila kitu
 
Jamani kuna hii theory kwamba msichana ambaye ni wa mwisho kuzaliwa nyumbani kwao mara nyingi huwa anakuwa amedekezwa sana kwa hiyo hafai kuolewa. Hafai kuolewa kwa sababu anategemea kuendelea kudekezwa kupita kiasi hata kwenye ndoa na kusahau kwamba mume si mama au baba yake.

Kama kuna mtu yeyote ana uzoefu na hili tafadhali, maana mwenzenu maji yako shingoni!
Mtadanganywa sana. Position katika kuzaliwa inahusika vipi katika mahusiano ya kindoa. Mbona mi ni mtoto wa mwisho lakini sina deko? Wacheni longolongo.
 
basi hata mtoto wa kiume wa mwisho na yeye atakuwa toto la mama tuu kwa fikra km hizi!
 
Na wewe bwana kama unataka kuoa oa ,,Masaki usitafute kisingizio bwana ...kudeka ni jadi ya mtu..
mwenye hapa ni wa tatu lakini napenda kudekezwa
 
he ancle ,inaa mana mimi sifai kuolewa? bcz mm ni last born as well.. lakin nahis tabia za watu haziendani kwa kuzaliwa zinaendana na malezi ,, nahsi hivyo ,

Ni kweli inategemea sana na malezi, lakini asilimia kubwa sana ya watoto wa mwisho huwa wanadekezwa sana na wazazi. Tena kama amepishana miaka zaidi ya mitatu na anayemfuatia ndio kabisaaa, wanamwona kama mjukuu vile! Yaani hakosei.
 
Mtoto wa kwanza na wamwisho ni yupi anae subiliwa kwa hamu?

Wa kwanza. Na hudekezwa sana tu. Ila akishakuja mwingine na mwingine tena yeye hadeki wala hadekezwi tena. Wazazi wanategemea aonyeshe mfano wa kuigwa na wadogo zake!!
 
Back
Top Bottom