Mtoto wa Mkulima analima wapi?

mi naona ipo wazi kuwa yeye ni mtoto wa mkulima na siyo maanake yeye ni mkulima.
inawezakana hata kulima hajawahi kama nilivyo mimi ni mtoto wa mfanyabiashara ila mimi ni mtumishi wa umma na ndio maana matatizo ya wafanya biashara siyajui
 
Mtoto wa Mkulima analima wapi? Shamba la mtoto wa Mkulima lipo pale Mji mkuu wa Tanzania Dodoma Mjengoni akiingia tu anavuta jembe lake kubwa alilopewa na Watanzania analima pasipo kutoka jasho kwani kwa siku akivuta mpini tu wa jembe tulilomkabidhi tukidhani atatukumbuka wakulima wenzake pamoja na watoto wa masikini anajikuta ana shilingi za kitanzania laki 350,000 kwa siku akitoka nje tu anawakuta akina Matonya mtaalamu wa kuomba anawamegea kidogo ya Pembejeo sasa kama wewe hujui yupo wapi ndugu yangu wakulima wenzake ameisha tuacha mbali sana akitoka hapo yupo Katavi anasubiri X-mass akitoka huko utamkuta magogoni akila upepo wa pwani akisubiri mavuno mengine ya vikao vya wakulima na waendesha nchi zikiwamo posho za kina JairoAnatory Mujwahuzia.
 
Ana ka gesti kake huko kwao na wageni wakubwa ni wale anatoka kigoma anakwenda kigoma,shamba tosha hilo
 
Ndugu,

Nashukru kwa wote waliochangia mada hii, nimejifunza mambo kadhaa
1. Wachangiaji wengine lugha zao si nzuri
2. Viongozi wanaoingia madarakani kwa mbwembwe na misemo kibao huwa hawatimizi ahadi zao
3. Baadhi ya viongozi hawatetei maslahi ya wananchi wake
4. Ni bora kuwa wazi na msimamo dhabiti kwa jambo unalolifanya (timiza wajibu wako)
 
Back
Top Bottom