Mtoto wa mke wangu amenishinda, anaelekea kuvunja ndoa yetu

kapari nesta

Member
Jul 28, 2015
22
32
Nawasalimu wote

Nilimuoa mke wangu wakati akiwa na mtoto mkubwa wa darasa la saba, Mimi nimezaa nae watoto wawili, tulifunga ndoa bomani kutokana na utofauti wa dini

Tatizo linaloninyima usingizi ni huyu mtoto wa wife, amekuwa na tabia zisizofaa, wakati tunafunga ndoa makubaliano yalikuwa ni kwamba aje na mtoto wake maana amezoea kuishi nae tangu mchanga.

Baba yake mtoto Alishafariki, nikakubali, miaka minne yote ya sekondari nimekuwa nikiitwa shuleni for serious displinary problems.

Ikiwemo uvutaji bange, hasa alipofika form 3 na kupigana, na kuwa gang leader wa genge lilikuwa linasumbua shuleni kwa utovu wewe nidhamu.

Mwaka Jana huyu mtoto amemaliza form four na alipata zero, baada ya kumaliza shule mwaka jana, tabia yake halisi ndipo ikajitokeza maana alikuwa anashinda nyumbani akisubiri matokeo.

Amekuwa akiuza vitu vya nyumbani mfano alifungua tairi la akiba kwenye gari yangu na ya mama yake akauza, aliiba ndani flat screen na deki zake akaenda kuuza, tulidhani ni vijana wa Mtaani.

Baada ya miezi miwili housegirl akaniambia TV ilichukuliwa na huyu mtoto na akaambiwa angepewa mgao lakini yeye akakataa.

Baadae akaja akaiba motor ya maji ya kupandisha Maji akishirikiana na vijana wa mtaani, ameuza viti vyangu vya plastic zaidi ya Kumi na viwili, alianza kuchukua store kimoja baadae ya kingine, kwa ujumla ameuza vitu vingi sana, achilia mbali simu zetu.

Nimekuwa nikimpa kipigo kizito na kitakatifu kila napogundua kaiba au kafanya tukio, lakini mama yake amekua akiniona mbaya kwa kumuadhibu mwanae, kiasi kwamba ananichunia wiki nzima, hatuongeleshani na ninaambiwa nafanya hivyo kwa kuwa sio mwanangu.

Hata mtoto mwenyewe Mara kadhaa huwa anatamka wazi kwamba usinipige mimi sio mwanao.Sasa nimeshachoka na huyu mtoto na mama yake pia, naishi huku nikificha vitu vyangu nakua sina amani

Wiki tatu zilizopita nilimlaza ndani polisi, baada ya kuiba tsh 500,000 iliyokua kwa bahasha, alipobanwa polisi akakiri na kuonesha ilipo kwa jamaa mmoja Dukani, tangu siku hiyo mama yake kanichunia na tuna ugomvi mkubwa kwa nn nilimpeleka mwanae polisi.
.
Wana Jf nimekata shauri kuacha na na huyu mwanamke ili aondoke na mtoto wake na mimi nibaki na wa kwangu,Nilim treat huyu mtoto kama wa kwangu na kumpa maisha mazuri ili ajione ana baba maana baba yake alifariki long time ago lakini amekua ni kinyume nimetumia njia nyingi bila mafanikio na sasa nimechoka

Ambao hamjaoa msithubutu kabisa kuoa mwanamke aliekwisha kuzaa ni very complicated, mimi nimeyaona, ndugu zangu wengi walipinga mimi nikalazimisha.

Huyu mtoto amesababisha mimi na mama yake kugombana Mara kwa Mara na kufanya ndoa hii kuwa ya mizozo isiyoisha, nimemuomba mama yake atafute pa kumpeleka kama hataki kuishi kulingana na sheria zangu ndani, amedai nimuoneshe pa kumpeleka.

Sasa nitamuonesha majibu kwa kuwatimua, nimeshakata shauri, yaani haya mambo ya familia unaweza kuweuka kwa kweli,inafikia pahala mtoto anauza viatu vya wadogo zake, suti, mapazia, hataki shule hataki chochote.

Najua cha kufanya
 
Ambao hamjaoa msithubutu kabisa kuoa mwanamke aliekwisha kuzaa ni very complicated, mm nimeyaona, ndugu zangu wengi walipinga mm nikalazimisha

ushauri ungeelekeza pande zote kuwa ambao hamjaoa na kuolewa, make hata hao wanao pia wanaweza kuja kuwa mwiba kwa mama yao wa kambo....pole kwa changamoto
 
Pole!
Nakumbuka mwaka 2009 nilishinikizwa na mama wa mtoto wangu. (Mzazi mwezangu) kumuoa agali na watoto wawili wa nje !

Mama aliniokoa kwa kunieleza kama hilo linalokupata na mengine mengi. Sasa hivi ningekuwa Nalia !

HÖGERA MAMA KWA KUNIOKOA
 
Ambao hamjaoa msithubutu kabisa kuoa mwanamke aliekwisha kuzaa ni very complicated, mm nimeyaona, ndugu zangu wengi walipinga mm nikalazimisha

Pole sana na najua umekwazika mpka kujisahau na kuandika (kwenye nyekundu)sio wote wako hivyo la hasha..
Nije kwenye ushauri muangalie huyo dogo ajaanza kutumia madawa ya kulevya?
Pili kumbuka ulipopenda boga ukapenda na uwa lake lakani lile Boga limekuwa tikiti maji na limearibikia ukubwani,,

Ukiwa likizo safiri na huyo dogo nje ya eneo mnaloishi kuwa nae karibu mimi napenda au nataka wewe ubadirike uwe kama Baba yake mzazi ongea nae mwambie kama ulivyotumbia uyapendi na unachukizwa na anayoyafanya,,Jaribu mara mbili tatu alafu muangalie je atabadilika au lah!

Hayo yashawatokea wengi na walijaribu wakafaulu,,Jaribu ndugu yangu usikate tamaa...
 
Pole sana huyo alitakiwa kukunjwa tangu mbichi.

Tatizo la watoto wa kamboau wa ndugu ni pale unapowakanya vitu/tabia fulani na wao kuchukulia wanaonewa na hivyo kuleta upinzani kwa kuendeleza tabia hizo na mwishowe ni kukosekana kwa maelewano kabisaaa.

Nakumbuka kesi za namna hii kutoka kwa baadhi ya ndugu na jirani zangu kwa vipindi tofauti.
 
pole ndugu ngoja nikuitie wajuvi wa haya mambo
cc Eli79 miss chagga faizafox atoto Rubi

Mie haya mambo yananipaga kigugumizi haswaaa, ila kulea mtoto aso wako ni kipaji kwakweli, huyo mtoto hana malezi mazuri tangu awali kilichopelekea yeye kuwa hivyo mamaye aweza kuwa sababu, ila pia wakati mwingine wazazi mwaweza jitahidi ila jamii na peer groups zikamuharibu, ila bado lawama ni kwa wazazi, mie kwa hili ngoja nisubiri wajuvi.
 
Last edited by a moderator:
Maneno yako matatu ya mwisho hayana afya kwenye mnakasha huu.


Nakushauri punguza hasira, MPE ushauri nasaha kama mtu mzima; akieleweka mpeleke shule ya ufundi VETA Dodoma baada ya miezi 6 atabadilika 100%.


Usikate tamaa kiasi hicho mkuu ndio dunia ilivyo na kumbuka kuwa kuna wenye makubwa kuliko yako ila wanakabiliana nayo kiutu uzima.

Nothing is impossible to the willing heart. NEVER!!
 
kapari nesta

Mkuu hilo ni janga,ni heri mama yake angekuwa upande wako kidogo inaleta sense,mbaya zaidi mama ake anamtetea na kukuona wewe kama unamtesa mwanae.Haya mambo yapo sana mkuu ni wengi yanawakuta haya,sio wanawake wote wako hivyo ni baadhi tu, mwisho ni kusubiria atakapomtenda mama yake mwenyewe ikamuuma ndio atajua kuwa alikuwa anafuga maradhi,pole sana mkuu,endelea kupata ushauri kabla ya kufanya maamuzi,ila inauma sana.
 
Last edited by a moderator:
Hapo uliposema wanawake wenye mtoto wasiolewe umekosea. Huyo mkeo ndio mwenye makosa kwa kumtetea mwanae na wakati mtoto anakosea.
Alitakiwa yeye angekuwa kipaumbele kuonyesha anachukia vitendo vya mwanae na kukuruhusu wewe baba umkanye mtoto bila yeye kuingilia au kumtetea.
 
Back
Top Bottom