Mtoto wa miaka 17 ajiua kwa risasi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Andengenye Ar.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye


Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Edmund Rice, John Justine (17) mkazi wa Makao Mapya, ambaye anasubiria matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, amejiua kwa kujipiga risasi kifuani, baada ya kudaiwa fedha na baba yake mzazi Justine Kaiza.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 1:30 usiku, nyumbani kwa wazazi wa marehemu huko makao mapya.

Alisema kuwa siku ya tukio, mama mzazi wa marehemu, Betty Mushi alikwenda kwenye sherehe na aliporudi muda wa saa 1:00 usiku, alikuta mlango wa geti umefungwa na hapo aliamua kumwomba mtoto wa jirani, ili amsaidie kufungua geti gilo.

“Mama huyu baada ya kufunguliwa geti tu, aliingia ndani na alipoingia sebuleni alimkuta mtoto wake amelala chini, huku akihema kwa taabu na damu ikimtoka kwa wingi kifuani,” alisema.

Alisema mama wa marehemu alipoona hivyo alitoka nje kuomba msaada wa majirani ambao walifika na kumpeleka hospitali ya Ithna Asher Charitable, maarufu kwa Dk. Mohamed, iliyopo eneo la Tanki la Maji Ilboru.

Kamanda Andengenye aliendelea kueleza kuwa baada ya kumfikisha katika hospitali hiyo, walitakiwa kumpeleka mgonjwa wao Hospitali ya Mkoa Mount Meru na walipofika hospitalini hapo akiwa anapatiwa matibabu alifariki dunia.

Aidha, polisi walipopata taarifa hizo walikwenda eneo la tukio na kukuta bunduki aina ya Shortgun Pump Action na ganda moja la risasi na pembeni yake walikuta ujumbe wa karatasi uliokuwa ukisema kwa maandishi ya herufi kubwa, “Ninasikitika kulaumiwa na wazazi wangu, na pia ninawapenda sana.”

Pia polisi hao walifaniki wakuona michuliziko ya damu toka ndani ya chumba cha marehemu hadi sehemu alipoangukia sebuleni.

Andengenye alisema kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa awali waligundua baba mzazi wa marehemu alikuwa akimdai fedha kijana wake alizomwibia ambazo ni dola za Marekani 1,500 sawa na fedha za kitanzania zaidi ya Sh. milioni 2.3.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na Polisi wanaendelea kumwoji baba mzazi wa marehemu Justine Kaiza kuhusiana na tukio hilo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru ukisubiri uchunguzi zaidi.



CHANZO: NIPASHE
 
Hiyo silaha imeipata wapi na amejuaje jinsi ya kuitumia?
Kweli vijana wa sasa hatuna uvumilivu kiasi cha kujitoa roho.
 
Mi kitambo nimepata hbr hii lakini ckupata kusikia kama huyu kijana alikuja kufa!

Na hili nilitonywa na dada mmoja mwenye duka post eneo la tukio na hata nikakosa chanzi ya kudodosa zaidi!

Dogo alale kwa AMANI ya Bwana!

Amen!
 
What if it is a cover up, what if baba yake ndio kammaliza na akaandika hiyo barua. Story ina gaps nyingi, where was the dad wakati wa tukio? Kama amejishoot kifuani, sioni jinsi angeweza kutembea tena. Tafakari
 
What if it is a cover up, what if baba yake ndio kammaliza na akaandika hiyo barua. Story ina gaps nyingi, where was the dad wakati wa tukio? Kama amejishoot kifuani, sioni jinsi angeweza kutembea tena. Tafakari
Si hivyo tu, gazeti limeshatoa conclusion kwamba "akimdai fedha kijana wake alizomwibia." Washa conclude aliiba!

Unajua Mkuu, kwenye magazeti yenye hadhi ya kimataifa huwezi kukuta wameandika kitu kama "fulani kajiua." Umemuona anajiua? Wanatumia maneno kama "apparent suicide." Hivi waandishi wetu wanashindwa hata ku google kidogo kuibia ibia style za uandishi? Magazeti ya huko kulikoendelea ni bure mitandaoni, wahariri jisomesheni kidogo wajameni... dah!
 
I knw beyond reasonable doubt the father killed him. Could b accidentally or intentional bt he shot him. Labda hata walijibishana akachukua bunduki kumtishia and went off. Problem yetu ni kwamba wazazi wengi hatujui how to communicate na watoto wetu in a way, ukamuelewa mtoto wako ni wa aina gani and hw u can help him or her na hata watoto kama they were in good terms mayb asingeiba hiyo hela na angelewana tu akapewa bt poor communication na barrier btn father son. I still blame the old man.
 
mi ndo maana sitakuja kununua hiki kifaa...badala ya ulinzi kinaweza tumika vibaya.rip dogo
 
Spoiled brat! Kwanza limeiba hela, pili linataka ku-manipulate watu kwa kujiua? That is, kama amejiua and it is not a scam!
You can keep a gun ( and lots of money and valuable) if you don't raise lazy spoiled brats!
 
Angeweza kujiua kwa kisu ama dawa ya panya! Muhimu ni kulea kizazi kinachowajibika! Kama hakuiba hela ama aliiba alipaswa kuwa tayari kukabili kilicho mbele yake. Kutokuwa na gun sio suluhisho!
mi ndo maana sitakuja kununua hiki kifaa...badala ya ulinzi kinaweza tumika vibaya.rip dogo
 
Back
Top Bottom