Mtoto wa miaka 10 kuwa shareholder wa prvate company inawezekana?

FUPITAM

Member
Mar 15, 2012
43
5
Wanajamvi nina mtoto wa miaka kumi na ninataka kufungua private company,je wanahisa tunaweza kuwa mimi na yeye tu? Au ni lazima niwe na mtu mzima? na je kama inawezekana kwa sisi wawili yaani mimi na mtoto wangu ninatakiwa nifanyeje na inakuwaje taratibu zake? Naombeni msaada wenu tafadhali
 
Inawezekana ndugu yangu kuwa na mtoto mwenye umri mdogo kwenye hisa na kuwa mkurugenzi. Kwenye kashfa ambazo zilitokea nchi hii na wanasheria wakasema yawezekana mtoto wa miaka kumi au chini kuwa shareholder. Ilikuwepo kashfa ingawa sikumbuki ila kwenye uongozi wa awamu ya nne mwanzoni au ya tatu mwishoni. WanaJF wanaweza kukumbuka.
 
Wanajamvi nina mtoto wa miaka kumi na ninataka kufungua private company,je wanahisa tunaweza kuwa mimi na yeye tu? Au ni lazima niwe na mtu mzima? na je kama inawezekana kwa sisi wawili yaani mimi na mtoto wangu ninatakiwa nifanyeje na inakuwaje taratibu zake? Naombeni msaada wenu tafadhali

Issue kubwa hapo ni kuwa mtoto hawezi kuingia mkataba au kufungwa na matakwa ya makataba.

Unapozungumzia kufungua kampuni, kimsingi unazungumzia pia mikataba. kwa mafano kunakuwa na mkataba/katiba kati/baina ya wanahisa (Memorandum of Association) na pia taratibu za uendeshaji wa kampuni (Articles of Association). Kitendo cha mtu kukubali kusaini documents zote hizi mbili kimsingi anakuwa anakubali kubeba wajibu unaoainishwa katika documents hizo. Kama una muda unaweza ku-google concept inaitwa 'veil of incorporation' na pia 'lifting the veil of incorporation', unaweza kuona vizuri zaidi ninachokisema hapa.

Sasa, kisheria mimi naona mtoto anaweza kuwa mwanahisa lakini sharti kuwa na mdhamini ambaye atawajibika kwa niaba yake mpaka pale mtoto atakapokuwa mtu mzima na akifikia umri huo atatakiwa kuamua ama kuendelea au kujitoa uanahisa huo.
 
Back
Top Bottom