Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,080
Mtoto wa Miaka 10 Afariki Kishujaa Akimuokoa Mama Yake
Friday, December 11, 2009 12:22 AM
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10 wa nchini Kenya amefariki dunia akipambana na fisi aliyemjeruhi vibaya mama yake. Mtoto wa Kikenya mwenye umri wa miaka 10 amefariki dunia kutokana na majeraha aliyopata baada ya kupambana na fisi aliyekuwa akimshambulia mama yake.
Fisi huyo alilipasua taya la mtoto Samatwa Kishibili pamoja na kukinyofoa kidole chake kimoja.
Mama yake Samatwa alijeruhiwa mikononi, kichwani na mgongoni katika tukio hilo lililotokea jumanne jioni katika maeneo ya ufukwe wa ziwa Naivasha katika ukanda wa Rift Valley.
Mama na mwanae walipoteza damu nyingi sana na ilibidi wawahishwe hospitali kwa matibabu lakini mtoto wake alifariki.
Taarifa iliyotolewa ilisema kuwa mama wa mtoto huyo alishambuliwa na fisi aliyekuwa akimfukuza asiwashambulie kondoo wake na ndipo mtoto wake alipoingilia kati kumuokoa.
Hata hivyo pamoja na kifo cha mtoto huyo, maafisa wa idara ya wanyamapori wa Kenya walisema kuwa familia ya mtoto huyo haitalipwa fidia yoyote kwakuwa walikuwa wakiishi kinyume cha sheria katika maeneo hayo.
"Haya ni maeneo yanayolindwa kwaajili ya wanyama, watu wanaojenga ndani ya maeneo haya wanavunja sheria", alisema afisa mmoja wa wanyama pori.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3722006&&Cat=2