Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Siasa si Uadui....SABODO J SABODO... mnazi wa falsafa za Mwalimu Nyerere... ni kada wa CCM na anasaidia upinzani!!
Anatafuta hifadhi in case cdm ikichukua nchi!
Siasa si Uadui....SABODO J SABODO... mnazi wa falsafa za Mwalimu Nyerere... ni kada wa CCM na anasaidia upinzani!!
.... kilichotokea hapo ni kwamba kijana alikuwa abambwe na biashara ambayo huenda amekuwa anafanya. Alichomoa mapema na WAKAWEZA kubadilisha kibao! habari ndo hiyo!!!!
Nzowa was right alipokejeli kwamba dau la USD 40K ni dogo sana ukilinganisha na mengine makubwa aliyokumbana nayo na AKAYAKATAA!!!
There is a lot more to this. Usanii tu!
Lazima wawepo walio na nia ya kukisafisha chama bila kukikimbia .mengi naye anatuzingua nindumila kuwili anasapoti ccm huku anapiga vita ufisadi while ccm=ufisadi
Mzee wetu Mengi alifanya BIASHARA gani zikamfikisha hapo alipo?
Kuna habari kwamba baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi na mfanyabiashara mmoja waliotajwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Abraham Mengi watafikishwa mahakamani kwa madai ya kutaka kumbambikizia mwanae dawa za kulevya.
Source; GP
Kuna habari kwamba baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi na mfanyabiashara mmoja waliotajwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Abraham Mengi watafikishwa mahakamani kwa madai ya kutaka kumbambikizia mwanae dawa za kulevya.
Habari zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya jeshi la polisi vimedai kuwa, vigogo hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili haki iweze kupatikana.
Taarifa hizo zimedai kuwa uhamisho wa vituo vya kazi uliofanywa ndani ya jeshi hilo ambapo Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kanda Maalum, jijini Dar es Salaam, Charles Mkumbo wamehamishiwa makao makuu ya jeshi hilo, ni mpango mahususi wa kutoa fursa kuwafikisha kortini ili tuhuma zao zikaamuliwe na chombo hicho.
Uhamisho uliofanywa ndani ya jeshi siyo wa kawaida kwani hata maofisa wengine waliohamishwa wamefanyiwa hivyo ili kufunika hili la watuhumiwa wa mzee Mengi.
Unajua swala hili hata sisi polisi linatuchanganya na sioni sababu ya kutolitolea tamko kwani hata tume iliyoundwa haikusema itachukua muda gani na mpaka sasa wananchi hawajui kinachoendelea, lakini watafikishwa kortini ili ukweli ukajulikane huko, kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina gazetini
Kwa upande mwingine askari mmoja wa ngazi za juu aliliambia gazeti hili kuwa tuhuma zilizotolewa na Mzee Mengi ni nzito na kitendo cha polisi kuwabadilisha kazi watuhumiwa kimeleta tafsiri mbaya kwa wananchi ambao wengi wanadhani kuwa uhamisho huo umekusudia kufunika kombe ili mwanaharamu apite, (yaani kuzima hoja).
Aidha, afisa huyo alisema ingefaa serikali ingetoa kwanza taarifa ya tume iliyoiunda kuhusiana na sakata hilo ndipo wahamishwe kuliko kuwahamisha wakati ukweli haujajulikana.
Aliongeza kwamba, suala la madai ya mzee Mengi lilikuwa rahisi kwa sababu mdai alisharuhusu jambo hilo lifikishwe mahakamani lakini serikali inajikanyaga, kitu ambacho kinaleta minongono isiyo na sababu katika jamii na kusababisha kitendawili kisiweze kutenguliwa.
Hata hivyo, afisa huyo alimsifu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema kwa kazi nzuri ya kuliletea heshima jeshi hilo hasa kipindi cha uchaguzi ambapo alisema kuwa demokrasia ilitumika kwa kiwango cha hali ya juu na hivyo kwa hali hiyo asikubali kukalia tuhuma ambazo baadaye zinaweza kuja kumchafua.
IGP Mwema tunajua kwamba kokoro linaweza kubeba kila kitu sasa ni kazi yako kuchambua samaki na kisichokuwa kitoweo, alisema afisa huyo.
Mwandishi wetu alifanya mahojiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SSP Advera Senso kuhusiana na suala la maofisa waliotuhumiwa na mzee Mengi kama watafikishwa mahakamani ambapo alisema sakata hilo linashughulikiwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini, (Takukuru).
Mimi nakushauri uende Takukuru, jeshi la polisi lilikabidhi kesi hiyo huko, alisema Kamanda Senso.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Takukuru, Doreen Kapwani alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alikiri kuwa wanalishughulikia.
Tunashughulikia malalamiko yale lakini taarifa za kupelekwa mahakamani watuhumiwa bado hazijanifikia, alisema Kapwani.
Gazeti hili lilimtafuta mmoja wa watuhumiwa, Bw. Nzowa alipohojiwa alisema hana la kusema bali suala hilo amelikabidhi kwa Mungu. Mkumbo hakupatikana.
Wakati huo huo, taarifa sahihi tulizozipata wakati gazeti hili likienda mitamboni zinasema polisi 12 wametiwa mbaroni jana kuhusiana na wizi wa mabomba 160 uliotokea Temeke.
Chanzo chetu cha habari kilisema mabomba hayo yaliibwa Novemba 16, mwaka huu katika ghala la vifaa vya ujenzi la Kampuni ya United Bulders Limited lililopo Barabara ya Nyerere .
Polisi hao 12 walikamatwa kwa tuhuma za kuwakamata majambazi waliohusika na wizi huo wakiwa na gari lililotumika kubeba mabomba hayo kisha kuwaachia, alisema mtoa habari wetu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alipoulizwa kwa njia ya simu juu ya tukio hilo jana Jumatatu alisema ni kweli limetokea na akaongeza kuwa raia saba na askari wanaotuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.
Source; GP
Mwema awe mwangalifu hili jeshi lisirudi enzi zile za kina Zombe kwani kipindi kile ilikuwa ni jehanamu