Mtoto wa Membe ahamishwa ofisi asipoteze ajira

jamani mnajua kama Membe ni mmakonde. Mtageuzwa Simba. mimi simoooo....joke.

Upimwe uwezo wake wa kazi na sio jina la familia yake.
Mimi nilipata bahati miaka ya mwishoni mwa 80's kufanya kazi kwa karibu kabisa na Mh Membe. Naweza sema ni mmoja wa vichwa ambavyo JK anaweza kujivunia.
 
Nimelichunguza hili dai, nimekuta ni majungu matupu!! chuki na wivu na roho mbaya!! halafu huyo mtajwa si mtoto wa Mh. Membe bali ni jamaa yake tu. Ni kijana muadilifu mwenye kunyenyekea kazi yake. Jamii Forum isigeuzwe sehemu ya kupikia majungu, kuharibiana sifa au kiendeleza cuki binafsi. Ziletwe nyeti zijadiliwe kwa nguvu ya hoja na si majungu ya kienyeji enyeji kama haya.
 
vyeti vya nini na wewe..kwani vyeti ndo vinaonyesha uwezo wa kufanya kazi ..ndo nyie mnalalamika nime graduate degree yangu university kazi sipati..ni kwa ajili ya kuwa na mawazo haya ya ubongo wa panzi
wape wape vidonge vyao nipo nao wengi hao anatanguliza cheti kabla ya kazi
icon10.gif
 
tatizo la huyu bwana nionavyo ni kujigamba kwake kwamba hawezi kuguswa na zoezi hilo la upunguzaji wafanyakazi kwa kuwa anatoka kwenye familia ya mh membe..na sio kama mnavyoona kama wivu ama fitina! Mbona kuna wengi wa wawakubwa hawapigi kelele!


Huu pia unaweza kuwa uzushi 99.9% kwa maana mtu mwenye akili tena zama hizi za watu kutokubabaikia majina au vyeo si rahisi kutamka au kujigamba kiivo.
Wakubwa walikuwa enzi za Mwalimu bwana...siku hizi kuna wakubwa??Enzi zile wadhifa ulikuwa unatetemekewa eti!
 
Whether huyo mtoto kasema au hajasema, ukweli unabaki palepale.... wenye kuondoka mtaondolewa, Mataka na network yake ya JK na watu wake watabaki kula kiinua mgongo cha nchi hii hadi hapo mtakapoamua kumpa mtu mwadilifu uongozi wa taifa hili.
 
Naona JF tunajimaliza. Tuliyeishi na Membe Canada miaka ya mwisho ya 90 tunajuwa kwamba hana mtoto anayeitwa John Membe.

Hata hivyo ni kawaida kwa mtu mwenye jina linalofanana na mtu mkubwa serikalini kutumia jina hilo kwa manufaa yake. I think JF can do better than this.
 
Back
Top Bottom