mtoto wa maskini asitisha masomo chuo kikuu Dar na kuingia mtaani kusaka 60% kisa....

Andindile

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
304
16
Ni kweli yametokea, kijana alikuwa anasoma Bsc. Engineering geology . Wazazi wake ni maskini wa kutupwa. Ni wa kulima wa kujikimu mkoani mbeya. Mtoto wao baada ya kufaulu vizuri alichaguliwa kujiunga chuo kikuu Dar mwaka 2007/2008 hivyo mwaka huu alikuwa anamalizia mwaka wake wa pili. Bodi ya mikopo ilimpatia asilimia 40% tu ya mkopo hivyo kutakiwa kumalizia iliyobakia. Kwa vile hakuwa na uwezo alilikata rufaa lakini ilitupiliwa mbali. Ulipotokea mgomo wale wasio na uwezo waliambiwa kuwa wakate rufaa kwa waziri. Zile rufaa ziliishia kushugulikiwa na bodi ya mikopo hivyo kijana kujikuta rufaa yake ikigonga mwamba kwa mara ya pili. Alijaribu kumwona waziri mwenye dhamana lakini wapi. hivyo akawa hana jinsi zaidi ya kuomba kuahirisha masomo na kuingia mtaani kushika chaki labda atadunduliza hiyo ailimia 60% ya miaka minne. Hivi ninavyo andika ujumbe huu kijana yupo mtaani akishika chaki.
Ukitaka kupata taarifa zaidi tembelea tovuti ya HESLB utaona ni kwa jinsi gani wale wote ambao wazazi wao ni maskini rufaa zao zilivyotupwa kasoro tu wale ambao ni yatima na wenye ulemavu. Kwa bodi ya mikopo kama wewe wazazi wako ni maskini hicho si kigezo cha kupewa 100%.

-Je ni wanafunzi wangapi watakosa/wamekosa elimu ya juu kwa sababu ya umaskini wao?
-Je tunataka vijana wafoji vyeti vya vifo vya wazazi wao ndipo tuwahurumie na kuwasomesha? Kwa nini tufike huko?
-Ndugu wana JF tunajenga taifa la watu gani kama mtu tutamsubject kwenye shida zote hizi ili tu apate elimu katika nchi yake?

Nawasilisha
 
Nampa pole jamaa. Asikate tamaa. Adundulize tu halafu arudi Chuo. Hakuna kizuri kisichokuwa na gharama. Ukiona "kizuri" hakina gharama, basi ujue ni bomu!
Lakini yote haya yanatokana na mfumo wetu uliojaa ufisadi. ungekuwa na uadilifu katika mikopo, naamini kijana huyo angeweza kupatiwa mkopo kwa asilimia 100.
 
Hii bodi ya mikopo inatakiwa iwe reviewed kunzia uundwaji wake, utendaji kazi, usimamiaje sera etc...vijana wanapata shida sana kutokana na double standards za bodi hii.....the policy on allocation of loans to students is not objective vey subjective and bias!
 
Ni kweli yametokea, kijana alikuwa anasoma Bsc. Engineering geology . Wazazi wake ni maskini wa kutupwa. Ni wa kulima wa kujikimu mkoani mbeya. Mtoto wao baada ya kufaulu vizuri alichaguliwa kujiunga chuo kikuu Dar mwaka 2007/2008 hivyo mwaka huu alikuwa anamalizia mwaka wake wa pili. Bodi ya mikopo ilimpatia asilimia 40% tu ya mkopo hivyo kutakiwa kumalizia iliyobakia. Kwa vile hakuwa na uwezo alilikata rufaa lakini ilitupiliwa mbali. Ulipotokea mgomo wale wasio na uwezo waliambiwa kuwa wakate rufaa kwa waziri. Zile rufaa ziliishia kushugulikiwa na bodi ya mikopo hivyo kijana kujikuta rufaa yake ikigonga mwamba kwa mara ya pili. Alijaribu kumwona waziri mwenye dhamana lakini wapi. hivyo akawa hana jinsi zaidi ya kuomba kuahirisha masomo na kuingia mtaani kushika chaki labda atadunduliza hiyo ailimia 60% ya miaka minne. Hivi ninavyo andika ujumbe huu kijana yupo mtaani akishika chaki.
Ukitaka kupata taarifa zaidi tembelea tovuti ya HESLB utaona ni kwa jinsi gani wale wote ambao wazazi wao ni maskini rufaa zao zilivyotupwa kasoro tu wale ambao ni yatima na wenye ulemavu. Kwa bodi ya mikopo kama wewe wazazi wako ni maskini hicho si kigezo cha kupewa 100%.

-Je ni wanafunzi wangapi watakosa/wamekosa elimu ya juu kwa sababu ya umaskini wao?
-Je tunataka vijana wafoji vyeti vya vifo vya wazazi wao ndipo tuwahurumie na kuwasomesha? Kwa nini tufike huko?
-Ndugu wana JF tunajenga taifa la watu gani kama mtu tutamsubject kwenye shida zote hizi ili tu apate elimu katika nchi yake?

Nawasilisha

Ni kweli kabisa mdau, katika taasisi ambazo zimeshindwa kabisa kumudu majukumu yake ni hii bodi ya mikopo.
Mimi nina mfano hai wa rafiki yangu mtumishi wa serikali(jeshi)ana wadogo zake wawili.Mmoja ni mtumishi wa serikali(mwalimu) na mwingine hana ajira.Walifanikiwa kupata nafasi za kujiunga na chuo kikuu cha dsm mwaka jana wote wakichukua kozi ya ualimu.Cha ajabu ni kwamba huyu mwalimu amepatiwa mkopo wa 100% wakati mwenzake asiye na ajira amepata 60%.Sasa imebidi dada mtu(mwalimu) na kaka mtu(mjeshi) wamfanyie donee mdogo wao ili kupata hiyo 40%. Sasa hapa kuna mambo mawili ambayo ninayona:
Kwanza hawa ndugu kutrokana na kazi zao, mwalimu na mwanajeshi mishahar yao ilivyo midogo imebidi wazisulubu familia zao ili mdogo wao asome. Pili hiyo inadhihirisha pasipo shaka kwamba bodi ya mikopo haifai haifai na hawawezi kukidhi mahitaji ya watanzania hususani wale wa kutoka familia za kimaskini. Sasa fikiria huyo kijana ameamua kushika chaki, hiyo asilimia 40 ataipata lini?tuition yenyewe siku hizi dar sh.5000 kwa somo moja kwa mwezi atafundisha miezi mingapi na masomo mangapi ili akidhi mahitaji yake?na ana mahitaji mengine kama chakula, malazi, na mengineyo.
kazi bado ndefu sana wajameni, bora bodi ya mikopo ivunjwe.
 
bodi ya mikopo iko pale kisiasa zaidi,hata jinsi ilivyoanzishwa ilikuwa ni kwa manufaa ya wanasiasa ili wapate kuchaguliwa,sio kwa minajili ya utendaji hasa wa kusaidia watanzania.
nampa pole sana huyo dogo...ajitahidi tu kutafuta hela,cha msingi awe na nia tu ,atafanikiwa..
sio bodi tu,serikali yenyewe ni ya kizushi hii..inazingua tu...
 
Naomba ufafanuzi hiyo 60% ndio pesa ngapi, na nikitaka kuwasiliana na huyo mwanafunzi anapatikanaje?
 
Naomba ufafanuzi hiyo 60% ndio pesa ngapi, na nikitaka kuwasiliana na huyo mwanafunzi anapatikanaje?

Wao wapo chini ya College of of Natural and Applied science (former Faculty of Science). Kulingana na fee structure ya chuo, wao wanatakiwa kulipa sh. 1,300,000/=. hivyo basi kama bodi walimpanga group C (60%) yeye anatakiwa kumalizia 40% which is equivalent to sh. 520,000 per year. Kwa miaka miwili anadaiwa sh. 1,040,000/=.

Nimekutumia taarifa zake kwenye private message ili uweze kuwasiliana nae.

Thanks
 
Mradi wa vitambulisho unatarajiwa kugharimu $200 milioni sawa na TShs262,000,000,000.

Hii pesa inatosha tuition 100% kwa wanafunzi 201,000 kwa mwaka mzima. Au tuseme wanafunzi wote wa vyuo vyote vya elimu ya juu kwa miaka angalau 4.

Sasa ni kipi tunachohitaji katika miaka minne ijayo, wataalam zaidi ya 201,000 au vitambulisho?
 
Jamani tunakoenda kubaya, nadhani huyo dogo na elimu yake inabidi aende kisomi,
-atafute hata watu wa wilaya au mkoa wake (aulizie vyama vyao anaweza anzia hapo hapo mlimani),
-pili atafute media, why ITV mara nyingi wanakubali kusaidia matangazo, lakini inabidi ajieleze kwa hisia hasa na vithibitisho.
Kupitia watu wa kwao anaweza pata hata mfadhili mmoja na kupitia media akapata wachangiaji wadogowadogo na pia ajaribu kupitia nyumba yake ya ibada kwani watu hutoa michango kama hii kwa wenye shida ni mwanzo wa baraka.
Asikate tamaa lakini pia asikae muda mrefu mitaani atashindwa kurudi shule.
 
Amtumie SMS JK. It works sometimes. Ni PM nitakupa namba yake.

Hata hivyo inabidi vigezo vyote viwe reviewed ila kuwe na fairness.

Pole san ndugu yangu.

Ila kumbuka there is always Plan B. When one door is closed, there is always another one which is open. Na Kuvunjika kwa koreo si mwisho wa Muhunzi.

Namfahamu kijana ambaye tulisoma naye primary akaishia la saba, sasa hivi ni milionea kupitia biashara halali.
 
Uamuzi wa kupigana ili asome ni uamuzi ambao ipo siku utampa faraja kubwa. Ndio jambo linalotakiwa pale ambapo njia za kawaida zinakuwa zimejaa mizengwe. Upande mwingine, bodi ya mikopo sijui wanajua nini wanatakiwa kufanya au ndo kuendeleza u bwana mkubwa tu. Mambo ya aina hii yanaweza kuleta picha kama kuna nia ya kudhalilisha maskini wasithubutu kusoma. Yaangaliwe vizuri jamani
 
Hata mi naunga mkono hoja yako mheshimiwa mwanaJF. ITV wanatupa mambo mazuri sana, cha msingi aende au aongee na mwanahabri mmoja wa report maalumu atemebelee chuo cha dsm atakuta watu kibao wanaishi kwa mikate, kusoma jawasomi kazi kulala na kuangalia movie tu kwani hali ni mbaya ni mbaya haswa. Report maalum itaokoa wengi, kama ulisikia jana bungeni mchangiaji wa mwisho, alisema: "wanafunzi chuo kikuu mlimani wanalala chumba kimoja hadi kumi, ambapo yeye alilala mtu mmoja au 2 enzi zake chumba hicho hicho. Hiyo ni alama tosha, elimu inabakwa sio inaboreshwa, tena kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.
 
Back
Top Bottom