Mtoto wa Liyumba akamatwa na madawa ya kulevya yenye thaman ya Bil 9 Tsh

huyo ni m1 tu wako watoto wa vigogo na vigogo wengi sana wanaofanya biashara ya unga na ndo mana pamoja na kelele nyingi za upigaji vita lakini biashara inaendelea km kawa na watuhumiwa papa hawakawatwi vinakamatwa vidagaa 2
 
Ana miaka 21 tu, ameshikwa na heroin kilo 200 zenye thamani ya Shilingi bilioni 9. Amekamatwa huko Lindi jana. Kwa mujibu wa polisi kitengo cha madawa, hii imevunja rekodi tangu kitengo hicho kilipoanzishwa mwaka 1990. Kama binti wa Liyumba ni dealer, vp baba yake? Vp na wengine?

Source: Nipashe/Mwananchi.

bilion tisa?mbona ndogo,jaman wapo wadau wale wapakistan kule tegeta walikutwa na mzgo wa sh ngapi,?ni zaid ya bil 9
 
hapo utaskia hakimu wa kesi hiyo atakavyounguruma siku ya hukumu 'ndugu mshtakiwa unahukumiwa kwenda jela miaka sita au kulipa faini isiyopungua Tsh Laki moja na nusu ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya biashara kama hiyo'' tuombe uhai
 
Hizi sio njama kweli? I sniff something, sio kama ya mtoto wa Mengi hii? Ngoja tuone...
 
Ana miaka 21 tu, ameshikwa na heroin kilo 200 zenye thamani ya Shilingi bilioni 9. Amekamatwa huko Lindi jana. Kwa mujibu wa polisi kitengo cha madawa, hii imevunja rekodi tangu kitengo hicho kilipoanzishwa mwaka 1990. Kama binti wa Liyumba ni dealer, vp baba yake? Vp na wengine?

Source: Nipashe/Mwananchi.

No si lazima Liyumba awe anahusika katika hili naomba nimtetee,liyumba ana yake lakini kwa hili hapana kutokana mazingira alokuwepo sasa,huyu dogo ni above 18,ni msichana mkubwa kabisa.Dogo atakuwa alitumwa kwenda kumpokea mtu dizaini mozambuque. ngoja niwang'ate sikio but sitaki maswali kwamba nimejuaje!

Iko hivi,wasfirisha wa madawa wana njia nyingi,za kuwakwepa askari,kinachofanyika hapa ni kwamba kuna mtu anaetumwa kwenda kuchukua mzigo pele(brazil)au musharaf(pakistan)kupitia iran,huyu akishapakia mzigo(dawa za kulevya)anapanda ndege mpaka may be Dubai au nchi za kusini mwa africa kama hapa kwa kesi ya mtoto wa Liyumba kutokana na aliposhikiwa hapo lindi inaonyesha kuna mtu alitoka shamba akashukia mozambique,huyu mtu alitoka na mzigo brazil ama pakistan/iran kazi yake inaisha baada ya kushuka airport ya moja ya nchi nilizozitaja hapo juu amabako hashuki ovyo ovyo lazima kunakua na mchongo wa kushukia hapo yani mabosi wake wanakuwa wameshaseti mambo hapo airport husika hivto jamaa anashuka hapo salama na kuingia mjini then anachukua hotel.Hapo sasa anatumwa kijana kama huyu wa liyumba kutoka hapa bongo na passport yake ya karatasi anasafiri kwa njia ya barabara napita boda ya tz na mozambique anagonga passport yake hiyo ya karatasi kama kawaida hapo boda then aningia mozambique anakwenda mpaka kweny hiyo hoteal aliyofikia yule aliyetoka shamba,hapo wanabadilisha na mzigo huyu dogo aliyetoka bongo anauchukua mzigo then anatambaa nao kivyake kwa njia ya barabara anapita pale boda anagonga muhuri wa kumtoa mozambique huyo anaingia zake Tanzania bila kushukiwa na yeyote kwa kuwa wanajua alienda mara moja mozambique tena na ppt ya karatasi,basi anasafiri mpaka dar anakabidhi mzigo anakula milioni zake 5! kwa safari hiyo ya siku kama 3 tu!lengo la kwenda kumpokea yule ni kuficha ile mihuri ya visa za pele au musharaf zisionekana maana visa za nchi hizo zinajulikana na watu wa madawa,brazili utaenda kufanya nini kama sio madawa tu..?

Habari ndio hiyo,maswali yanakaribishwa,naipenda nchi yangu,nimeamua kusaidia kidogo,ila usinilulize tu nimejuaje!
 
heroinpix.jpg
 
Kweli kabisa Angel na ukijifanya kiherehere wanakutanguliza mbele ya haki huu mtandao ni mkubwa sana
huyo ni m1 tu wako watoto wa vigogo na vigogo wengi sana wanaofanya biashara ya unga na ndo mana pamoja na kelele nyingi za upigaji vita lakini biashara inaendelea km kawa na watuhumiwa papa hawakawatwi vinakamatwa vidagaa 2
 
huyo ni m1 tu wako watoto wa vigogo na vigogo wengi sana wanaofanya biashara ya unga na ndo mana pamoja na kelele nyingi za upigaji vita lakini biashara inaendelea km kawa na watuhumiwa papa hawakawatwi vinakamatwa vidagaa 2

Mods waruhusu tuwataje hili wawekewe mitego,wale jamaa wa mbezi jogoo waliokamatwa na mapodaaaa ni watu wa bata ndefu asubuhi utawakuta wapo mbele ya gadeni na machupa ya litre 1.5 na magazeti wanakula upepo kwa ndani kuna DCM imepaki,na magari mengine madogo,hawa watu wanaua rasilimali watu wa taifa letu
 
kwa vyovyote hayuko peke yake nadhani kuna wakubwa wengi tu. hu ni mwanzo wa ufunuo wa kujua mengi zaidi
 
bilion tisa?mbona ndogo,jaman wapo wadau wale wapakistan kule tegeta walikutwa na mzgo wa sh ngapi,?ni zaid ya bil 9

Sio Tegeta ni mbezi jogoo walikua na mzigo mdogo sana kama wa bil4 na ushee maana ilikua kilo 89 na wakakuta fedha zenye thamn ya mil15 ndani
 
Ana miaka 21 tu, ameshikwa na heroin kilo 200 zenye thamani ya Shilingi bilioni 9. Amekamatwa huko Lindi jana. Kwa mujibu wa polisi kitengo cha madawa, hii imevunja rekodi tangu kitengo hicho kilipoanzishwa mwaka 1990. Kama binti wa Liyumba ni dealer, vp baba yake? Vp na wengine?

Source: Nipashe/Mwananchi.

Jamani nielewesheni vizuri, hivi bei ya bidhaa haramu(kama madawa ya kulevya), inadhibitishwa vipi kuwa ni sahihi?
 
Tz has been made a free zone for every illegal activity na hii inatokana na ulegelege wa serikali wa kutochukua hatua madhubuti kukabili matatizo. politiki kila mahali. haiingii akilini jitu linasimama jukwaani na kusema majina ya viongozi wa dini wanaohusika na biashara ya unga ninayo afu kimya.Mara nina majina ya vigogo wanaohusika afu hakuna lolote. Kimsingi political dons are the major players in this!
 
Mh kama ndo yale yaliyodakwa mkoani Lindi,kwa mujibu wa TBC ni kilo 210 zenye thamani ya Tsh bilioni 9.3!
 
Back
Top Bottom