Mtoto wa Liberia anatafuta kidume ale nacho midola ya urithi

actually anayetuma msg siyo mwanamke. Mimi niliwasiliana naye hadi point ya mwisho. Ilipofikia kwenye kutuma hela akanambia nitume kwenye akaunti ya mchungaji wake ambaye alinipa jina na akaunti namba yake. Kwa madai yeye yupo kwenye kambi ya wakimbizi haruhusiwi kuwa na akaunti. Jina la mchungaji ni la kiume. Kwa hiyo inaonyesha kwamba huyo jamaa anazo picha za huyu mdada na anazitumia kwa ajili ya utapeli. Nilipopata lile jina nikaingia kwenye mtandao na kutafuta hiyo benk, nikakuta ni ya Nigeria. Nikaforward hilo jina polisi ya nigeria, hadi leo sijawahi kupata majibu.

Ahsante mkuu kwa jitihada zako za kupambana na utapeli, unfortunately watendaji wengi katika serikali za kiafrika ndio wanachama wa mitandao ya kiharifu... madai ya juzi ya mengi hayakustahili kuchunguzwa na jeshi la polisi ambalo watendaji wake wakuu ndio watuhumiwa
 
Bwa bwa bwaaa hebu muunganishe na yule mkuu wa kazi za majuu wataelewana sana! :smiling:
 
endeleeni kutapeliwa tu, west africa kupata mwanamke mrembo hivyo tena aliye kwenye kambi ya wakimbizi ni nadra sana.
 
Bwa bwa bwaaa hebu muunganishe na yule mkuu wa kazi za majuu wataelewana sana! :smiling:

Huyo mtoto muunganisheni na Mr Uti, mnigeria mwenzake mwenye US $ 201,000 labda wataelewana, ugali moto na mboga moto, hakuna kushiba!!!
 
Wengi hapo juu mnakosea sana.Hawa matapeli wakati mwingine hawahitaji benki details bali wanataka UWAJIBU TU KWA EMAIL YAKO!!!Wanakuwa na uwezo fulani wa kuisaka pasiwedi yako na hapo wanaingia ktk akaunti yako ya email na kuwasiliana na ndugu,jamaa au marafiki unaowasiliana mara kwa mara na kuwapiga mzinga kama ni wewe una shida fulani.Kama rafiki/ndugu yako hajajiuliza akamtumia akidhani wewe tayari mmeshaliwa!!KAA CHONJO!nashauri wote mliowajibu MBADILISHE PASIWEDI ZENU.Hayo tu
 
Back
Top Bottom