Mtoto wa Kikwete ashinda kwa kishindo

Please guys, let us give a kid a break!
Amegombea, watu wamempigia kura.. ndio utamu wa demokrasia!
Hail to The Great Thinker Nyani Ngabu bin Julius.. Miafrika ndivyo tulivyo!
 
  • Kibunango, hivi kwa nini kuna sheria inayosema huwezi kujiandikisha kupiga kura hadi ufikishe miaka fulani ?
  • Hawa watoto wanasafiri peke yao ama wanaongozana na ama wazazi wao au guardians wao ?
  • Je, nani anawagharamia kwenye safari na malazi ama wanajilipia ? Kama wanagharamiwa je, ni chombo gani hicho na kinapataje pesa?
  • Kama ni chama cha siasa (CCM) hiyo inaruhusiwa kisheria hivi vikinda kujishughulisha ama kutumiwa kisiasa ?
  • Je, inakuwaje kama mtoto wa miaka kumi hakipendi chama cha baba yake na kwa mtindo huu tunawafundisha nini hawa kinda - kuwa wana tofauti na wenzao ?
  • Je lengo hapa ni kama lile la Al Qaida la kuwasokomezea itikadi tangu utotoni - adui wao hapa ni nani ?
  • Je, ni kweli kuwa CCM hawaoni hatari ya kuwapandikiza watoto wadogo hii tabia ya kubaguana ?
Mababu wa CCM, Wazazi wa CCM, wake wa CCM, Wamama wa CCM, Vijana wa CCM , Chipukizi wa CCM, Wajukuu wa CCM hadi Watukuu wa CCM - jamani tunajenga Taifa gani au ndio mwanzo wa kutanguliza maslahi ya CCM kabla ya taifa.
Kwani Chipukizi imeanza lini??,nijuavyo mimi Chipukizi imeanza tangu enzi za Nyerere(enzi za Chama kimoja),na viongozi wengi tu wa vyama kama CCM,CUF,CHADEMA,NCCR-Mageuzi n.k wamepitia hiyo Chipukizi..Kwangu mimi naona si vibaya kuwashirikisha watoto kama hawa(wenye miaka 10 na kuendelea) kwenye siasa,watakulia(huko) CCM baadae wataamua ama kuendelea na hiyo CCM ama kujiunga na vyama vingine(viongozi na wanachama wengi wa vyama vya siasa Tanzania walipitia CCM ama kwa kuwa Chipukizi ama UVCCM) kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanza..CCM wanajiandalia mtaji/hazina ya kisiasa miaka ijayo..Si vibaya kwa vyama vingine wakaanza kuwaandaa wanachama/viongozi wa kizazi kijacho kwa kupitia Chipukizi...Ni mtazamo tu wakuu..Pamoja
 
Chipukizi ni form ya grooming too, enzi za TANU wakiitwa 'Young Pioneer', Mwalimu alitokanayo China alikolitoa Azimio La Arusha na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea iliyobakia jina tuu kwenye katiba yetu ya Mwaka 1977.

Grooming always ni kitu kizuri, imekuwa ikifanyika for time immemorial kwenye royal families tangu ndoa inajulikana mtoto wa kwanza wa kiume kuzaliwa kuzaliwa ndio mrithi wa kiti cha ufalme wa babaye, hivyo tagu mimba, inakuwa groomed as the heir to the throne.

Mtoto huyo hulelewa kwa makuzi ya anticipated king, heavily mind indoctrination of not who is realy is, but who ought to be, 'king'.

Sasa kuna ubaya gani kuwagroom hawa vijana wadogo chpukizi wa CCM kuhusu chama chao na baadae kinatoa viongozi wazuri tuu, Nape ametokea Chipukizi, yule mwenyekiti wa zamani, Frank Uhahula ambaye sasa ni mkuu wa wilaya, ametokea chipukizi, the logic is to see the potential in them, groom them to make that potential a reality.

Huu msemo wa 'like father like son' unafanywa practical zaidi kwa kumgroom mwanao afuate nyayo zako ndio maana baada ta Karume Baba, sasa Karume ni rais wa Zanzibar, tumeona kwa Kabila, kwa Bush, Ghadhi, Kenyata, Oginga, Kenedies etc sometime baada ya mume ni mke, kama Sonia Ghadhi, Imelda Marcos, Mama Acquino, Winie Mandela etc, hakuna ubaya wowote, zamu za kina, Makongoro, Dr. Mwinyi, Nikolas, Ridhiwan etc zinafuatia with time.

Angalizo:Baba anaweza kuwa kiongozi bora na mwana asiwe, vile vile baba aweza kuwa kiongozi bomu, mwana akaja kuwa kiongozi bora. Issue isiwe kwa vile ni mtoto wa nani, bali iwe ni uwezo binafsi wa mtoto, ability na capability, kazi ya mzazi ni kumjengea tuu interest, ndicho wanachofanyiwa chipukizi hawa.
 
JK mwennyekiti,
Mama Salma (mke) mjumbe
Ridhiwani (mtoto) UVCCM
Khalfani (mtoto) mjumbe wa Baraza la Chipukizi na UVCCM

Sasa chama cha kifamilia na kikabila ni CHADEMA au CCM?

Binafsi huwa naona ni dhana tu potofu kwamba watu wengi wa familia/ukoo mmoja kujiunga na chama fulani(siasa) chama kinakuwa cha kifamilia..

Ukienda nchi za wenzetu utaona hiki ni kitu cha kawaida tu,kwa mfano George H.W Bush alikuwa Rais wa Marekani,baadaye mwanaye George W. Bush akawa Rais pia wa Marekani huku kakaake Jeb Bush akiwa Gavana wa jimbo la Florida(wote hawa ni chama kimoja cha Republican) au ukienda India angalia jinsi Jawaharlal Nehru familia yake ilivyojihusisha na siasa(ndani ya chama cha Congress) kwa kuanzia mwanaye Indira Gandhi mjukuu wake hayati Rajiv Gandhi,mkwewe Sonia Gandhi(Rais wa sasa wa Congress) na sasa wajukuu zake Rahul Gandhi(Katibu mkuu wa sasa wa Congress) na Priyanka Gandhi ambaye taratibu kaanza kujihusisha na siasa za India..Ukiangalia mifano hii miwli(kati ya mingii) utaona kwamba wenzetu hawaangalii kabisa wala kujali haya mambo ya ooh sijui chama cha kikabila wala chama cha kifamilia....So tuachane na mitazamo hafifu kama hii...Pamoja mkuu
 
Chipukizi ni form ya grooming too, enzi za TANU wakiitwa 'Young Pioneer', Mwalimu alitokanayo China alikolitoa Azimio La Arusha na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea iliyobakia jina tuu kwenye katiba yetu ya Mwaka 1977.

Grooming always ni kitu kizuri, imekuwa ikifanyika for time immemorial kwenye royal families tangu ndoa inajulikana mtoto wa kwanza wa kiume kuzaliwa kuzaliwa ndio mrithi wa kiti cha ufalme wa babaye, hivyo tagu mimba, inakuwa groomed as the heir to the throne.

Mtoto huyo hulelewa kwa makuzi ya anticipated king, heavily mind indoctrination of not who is realy is, but who ought to be, 'king'.

Sasa kuna ubaya gani kuwagroom hawa vijana wadogo chpukizi wa CCM kuhusu chama chao na baadae kinatoa viongozi wazuri tuu, Nape ametokea Chipukizi, yule mwenyekiti wa zamani, Frank Uhahula ambaye sasa ni mkuu wa wilaya, ametokea chipukizi, the logic is to see the potential in them, groom them to make that potential a reality.

Huu msemo wa 'like father like son' unafanywa practical zaidi kwa kumgroom mwanao afuate nyayo zako ndio maana baada ta Karume Baba, sasa Karume ni rais wa Zanzibar, tumeona kwa Kabila, kwa Bush, Ghadhi, Kenyata, Oginga, Kenedies etc sometime baada ya mume ni mke, kama Sonia Ghadhi, Imelda Marcos, Mama Acquino, Winie Mandela etc, hakuna ubaya wowote, zamu za kina, Makongoro, Dr. Mwinyi, Nikolas, Ridhiwan etc zinafuatia with time.

Angalizo, Baba anaweza kuwa kiongozi bora na mwana asiwe, vile vile baba aweza kuwa kiongozi bomu, mwana akaja kuwa kiongozi bora.

Umeongea yoote mkuu,umemaliza...Well said
 
Watoto hao walichagua kwa utashi wao, au ni vile huyo ni mtoto wa Rais na kampeni walipiga watu wengine kabisa. Hawa watoto badala ya kuhamasishwa kujipatia maarifa, wanafundishwa mipango ya kifisadi. sijui hata kama wenyewe wanajua wanagombea nini?

tungeelezwa pia kuwa hawa watoto wakati wanagombea walitoa hotuba zipi, ili tujue kama kweli wanajua wanachogombea.
 
ukienda India angalia jinsi Jawaharlal Nehru familia yake ilivyojihusisha na siasa(ndani ya chama cha Congress) kwa kuanzia mwanaye Indira Gandhi mjukuu wake hayati Rajiv Gandhi,mkwewe Sonia Gandhi(Rais wa sasa wa Congress) na sasa wajukuu zake Rahul Gandhi(Katibu mkuu wa sasa wa Congress) na Priyanka Gandhi ambaye taratibu kaanza kujihusisha na siasa za India..

Sonia walishamtwaa kwa njia ile ile waliomtwaa Mahatma Gandhi, Indira Gandhi, Ranjiv Gandhi. Politics, not only a dirty game, but a dengerous too. Siasa sio tuu ni mchezo mchafu, bali ni wa hatari pia, hivyo hiyo chipukizi inawaanaa kwa yote na kukubali yote yakiwemo matokeo na yatokanayo, end results and consequenses.
 
hao ni vijana chipukizi wa ccm kitaifa au ni vijana chipukizi wa ccm ambao ni watoto wa viongozi ambao wapo katika ccm? kuna mtoto wa mlala hoi aliyepata nafasi ya kugombea? wenye dataz plz....

hujaelewaka mkuu, nafikiri unauliza hao ni chipukizi wa taifa la tanzania au chipukizi wa chama cha mafisadi?
 
Sonia walishamtwaa kwa njia ile ile waliomtwaa Mahatma Gandhi, Indira Gandhi, Ranjiv Gandhi. Politics, not only a dirty game, but a dengerous too. Siasa sio tuu ni mchezo mchafu, bali ni wa hatari pia, hivyo hiyo chipukizi inawaanaa kwa yote na kukubali yote yakiwemo matokeo na yatokanayo, end results and consequenses.

Pasco,sijakuelewa hapo kwnye bold
 
Whats is this?? Naona CCM wameamua kufundisha na kupanda mbegu za uzandiki na majungu kuanzia kwa watoto, kweli taifa linazidi kuporomoka! Badala ya kujenga mazingira ya watoto hawa kuwa wanasayansi katika fani mbalimbali, tunawajenga kuwa prospective mafisadi na wapiga siasa!!

Shame to all Tanzanians whether you are in Tanzania or abroad!!!
 
Kwani Chipukizi imeanza lini??,nijuavyo mimi Chipukizi imeanza tangu enzi za Nyerere(enzi za Chama kimoja),na viongozi wengi tu wa vyama kama CCM,CUF,CHADEMA,NCCR-Mageuzi n.k wamepitia hiyo Chipukizi..Kwangu mimi naona si vibaya kuwashirikisha watoto kama hawa(wenye miaka 10 na kuendelea) kwenye siasa,watakulia(huko) CCM baadae wataamua ama kuendelea na hiyo CCM ama kujiunga na vyama vingine(viongozi na wanachama wengi wa vyama vya siasa Tanzania walipitia CCM ama kwa kuwa Chipukizi ama UVCCM) kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanza..CCM wanajiandalia mtaji/hazina ya kisiasa miaka ijayo..Si vibaya kwa vyama vingine wakaanza kuwaandaa wanachama/viongozi wa kizazi kijacho kwa kupitia Chipukizi...Ni mtazamo tu wakuu..Pamoja

Mkuu nimekupata ni bora kuwa na chipukizi wa umoja wa kitaifa, ili tuwafunze watoto uzalendo na kuwaandaa kuwa vijana watakaotetea taifa lao la tanzania as a whole.

Hii mambo ya chipuziki mafisadi haisaidii kitu ni kuwaandaa watoto waje kuwa mafisadi wa kesho warithi ufisadi wa babazao tuitafuna nchi yetu.

kwangu mimi siungi mkono huu upuuzi, lowassa hana mtoto mdogo awe katibu wa dogo ili tukamilishe lile fathers like sons? "hatukukutana mtaani...."
 
Kwani Chipukizi imeanza lini??,nijuavyo mimi Chipukizi imeanza tangu enzi za Nyerere(enzi za Chama kimoja),na viongozi wengi tu wa vyama kama CCM,CUF,CHADEMA,NCCR-Mageuzi n.k wamepitia hiyo Chipukizi..Kwangu mimi naona si vibaya kuwashirikisha watoto kama hawa(wenye miaka 10 na kuendelea) kwenye siasa,watakulia(huko) CCM baadae wataamua ama kuendelea na hiyo CCM ama kujiunga na vyama vingine(viongozi na wanachama wengi wa vyama vya siasa Tanzania walipitia CCM ama kwa kuwa Chipukizi ama UVCCM) kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanza..CCM wanajiandalia mtaji/hazina ya kisiasa miaka ijayo..Si vibaya kwa vyama vingine wakaanza kuwaandaa wanachama/viongozi wa kizazi kijacho kwa kupitia Chipukizi...Ni mtazamo tu wakuu..Pamoja

Nakubaliana nawe. Lengo la awali la Chipukizi wa TANU/CCM lilikuwa ni kuwaandaa vijana kuielewa vyema siasa ya chama chao ili waweze kuwa viongozi na wanachama madhubuti wa chama chao siku za usoni. Akina Mahlangu, Guninita ndiko walikotokea huko lakini kwa bahati mbaya inaelekea wamemezwa na itikadi za kifisadi na kusahau maadili na malengo ya Chama waliyofundishwa wakiwa chipukizi!

Tatizo lililopo ni viongozi kuamua kwa makusudi kuwashindanisha watoto wao na watoto wengine wakielewa wazi kwamba kwa vyovyote vile hao watoto watachaguliwa kutokana na majina yao na si kwa uwezo wao wa kujieleza ama kwa kudhihirisha kwa namna nyingine kwamba wana uwezo wa aina fulani.
 
Imeandikwa na John Nditi, Morogoro;
Tarehe: 30th December 2009

MKUTANO Mkuu wa Uchaguzi wa Chipukizi taifa umemchagua kwa kishindo mtoto wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete, Khalfani Kikwete (11) kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Chipukizi Taifa Tanzania Bara.

Khalfani alipata kura 301 na kuwashinda wagombea wenzake 11. Kwa Tanzania Zanzibar, mshindi alikuwa Abdallah Haji Mgeni. Kutokana na ushindi huo Khalfani ataliwakilisha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM).

Mtoto wa Katibu wa Fedha na Uchumi wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amos Makala, Gabriel Makala (12), amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa.

Gabriel alishinda kwa kupata kura 300 kati ya kura 357, aliwashinda wagombea wanane,kura saba ziliharibika.

Uchaguzi Mkuu huo wa Chipukizi Taifa uliofanyika mjini Morogoro ni wa vijana wadogo wa CCM kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Nafasi ya Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa upande wa Tanzania Bara ilichukuliwa na Gladness Urassa na Ramadhani Guruwe,Tanzania Zanzibar ilichukuliwa na Elias Cassion.

Katika nafasi ya Kamati ya Uendeshaji Taifa Tanzania Bara, ilichukuliwa na Glory Mwambeleko na Asnail King, wakati upande wa Zanzibar, ilikwenda kwa Abdalah Haji Mgeni na Abdulatif Ramadhan Abdullah.

Source: Gazeti la Habari Leo

Badala ya watoto wasome uraia nyie mnawahangaisha kwa mambo ya kipuuzi - hamna kazi ya kufanya?
 
Umeongea yoote mkuu,umemaliza...Well said

Kwani kuna haja ya kupteza mda kutrace where Chipukizi thing originated? Tunapaswa kuangalia vitu vyenye mantic..

1. Kwa kuwa mafisadi wana hela nyingi...lolote kwao ni rahisi

2. Kuwa mtot wa Kikwete kushinda sio maaajabu......kumbukeni uchaguzi ni kulipa fadhila...hao hao waliondesha uchaguzi wangekuwa hatarini kama mtoto wake angeshindwa.....

3. Tusitegemee maajabu...kuchaguliwa ni haki yake...aanze kujifunza kucheka na kusmile mbele za wapigakura maana watanzania ndicho tunachovuna kumchagua baba yake.

4. Kuwa CCM imeshageuka ya wachache tena wenye nazo...sote tunatambua...
 
Sorry Bantalanda, nilimchanganya Sonia na Muhatma Benazil Bhutto, ndiye aliyetwaliwa. Kutwaliwa namaanisha kuuwawa, hao wote waliowawa. Sorry kwa inconveniences caused, you are right.

Nimekusoma mkuu...Pamoja
 
Back
Top Bottom