Mtoto wa Kikwete ashinda kwa kishindo

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Imeandikwa na John Nditi, Morogoro;
Tarehe: 30th December 2009


MKUTANO Mkuu wa Uchaguzi wa Chipukizi taifa umemchagua kwa kishindo mtoto wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete, Khalfani Kikwete (11) kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Chipukizi Taifa Tanzania Bara.

Khalfani alipata kura 301 na kuwashinda wagombea wenzake 11. Kwa Tanzania Zanzibar, mshindi alikuwa Abdallah Haji Mgeni. Kutokana na ushindi huo Khalfani ataliwakilisha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM).

Mtoto wa Katibu wa Fedha na Uchumi wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amos Makala, Gabriel Makala (12), amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa.

Gabriel alishinda kwa kupata kura 300 kati ya kura 357, aliwashinda wagombea wanane,kura saba ziliharibika.

Uchaguzi Mkuu huo wa Chipukizi Taifa uliofanyika mjini Morogoro ni wa vijana wadogo wa CCM kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Nafasi ya Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa upande wa Tanzania Bara ilichukuliwa na Gladness Urassa na Ramadhani Guruwe,Tanzania Zanzibar ilichukuliwa na Elias Cassion.

Katika nafasi ya Kamati ya Uendeshaji Taifa Tanzania Bara, ilichukuliwa na Glory Mwambeleko na Asnail King, wakati upande wa Zanzibar, ilikwenda kwa Abdalah Haji Mgeni na Abdulatif Ramadhan Abdullah.

Source: Gazeti la Habari Leo
 
hao ni vijana chipukizi wa ccm kitaifa au ni vijana chipukizi wa ccm ambao ni watoto wa viongozi ambao wapo katika ccm? kuna mtoto wa mlala hoi aliyepata nafasi ya kugombea? wenye dataz plz....
 
Mimi nawasikitikia sana hawa watoto wamezaliwa katika kipindi kigumu sana kwa CCM hadi Khalifani afikishe umri wa kugombea ubunge miaka 21, CCM itakuwa hoi bin taabani imegawanyika katika makundi mawili CCM-Asili na CCM-Mtandao/Mafisadi sijui yeye atakuwa upande gani wakati huo.

Pole sana dogo usijali utakuwa kiongozi wa upinzani bungeni maana makundi yote ya CCM yatakuwa upande wa upinzani, CCM-Mtandao chama kikuu cha upinzani.
 
JK mwennyekiti,
Mama Salma (mke) mjumbe
Ridhiwani (mtoto) UVCCM
Khalfani (mtoto) mjumbe wa Baraza la Chipukizi na UVCCM

Sasa chama cha kifamilia na kikabila ni CHADEMA au CCM?
 
Watoto hao walichagua kwa utashi wao, au ni vile huyo ni mtoto wa Rais na kampeni walipiga watu wengine kabisa. Hawa watoto badala ya kuhamasishwa kujipatia maarifa, wanafundishwa mipango ya kifisadi. sijui hata kama wenyewe wanajua wanagombea nini?
 
Hongera washindi tunaamini mtakuwa ndiyo chachu ya maendeleo ya nchi hii. Nafasi za wazazi wenu hazizuii nyie kuwa na madaraka. Kuna wengine wazazi wao wafanyabiashara, wengine wakulima na wana mafanikio makubwa nanyi mmechagua siasa tunawaombea mafanikio yanayozingatia haki na mustakbali mzuri wa Taifa letu. Huenda kizazi chenu kitalikomboa Taifa hili maana kizazi cha sasa ni blahblah na ukosoaji
 
sijui hata kama wenyewe wanajua wanagombea nini?

Hii kweli kali, nasikia wengine wana miaka 7, sasa mtoto wa miaka 7 anakuwa eti kiongozi wa kamati ya Uendeshaji wa Taifa anajua hata uendeshaji maana yake nini labda uendeshaji wa magari ya makopo.
 
Hongereni Chipukizi wote mlioshinda na kupata nafasi ya kuwakilisha chipukizi wengine!
 
Hii kweli kali, nasikia wengine wana miaka 7, sasa mtoto wa miaka 7 anakuwa eti kiongozi wa kamati ya Uendeshaji wa Taifa anajua hata uendeshaji maana yake nini labda uendeshaji wa magari ya makopo.

Ndio maana Tz kila kitu ni siasa, hata miili na viungo vya waTz walio wengi ni siasa tupu!!
 
Huyu mtoto anashiriki au anashirikishwa kwenye siasa? Miaka 11 ni michache sana kunishawishi kuwa huyu mtoto anaelewa lolote khs siasa.
 
Lini atafurahia utoto wake jamni pole dogo!
Kufurahia ni relative inawezekana na yeye ndio anafurahia hapo. Kucheza au kuangalia cartons ni aina tu ya maisha ambayo huchaguliwa.
Hata hivyo muda wa chipukizi haumaanishi kuchukua nafasi ya mtoto kujiendeleza katika masuala mengine.
 
Hata aibu hawaoni!
Watoto au nani? Inawezekana huenda wanaambiwa watoto. Inamaana wao hawana haki ya kuwa viongozi? Wamependelewa? Mbona watoto wa wafanyabiashara wanaokuwa wafanyabiashara hawalaumiwi? Waacheni jamani wakati wetu umepita tupambane na siasa tunazolingana nazo (baba zao). Huenda wakawa wakombozi wetu.
 
Huku ni kutuharibia watoto ambao huenda wangekua ma-daktari bingwa, ma-engineer na fani nyingine mbali na blaablaa za majukwaani.
Ok ngoja 2kubali matokeo huenda Baba wa mtoto muhusika kampima mwanae kaona anamuelekeo wa ki-siasa. Maana ki mtazamo wangu huyu mtoto anaandaliwa kuelekea huko.
P.i.t.y
 
Hongereni Chipukizi wote mlioshinda na kupata nafasi ya kuwakilisha chipukizi wengine!


  • Kibunango, hivi kwa nini kuna sheria inayosema huwezi kujiandikisha kupiga kura hadi ufikishe miaka fulani ?
  • Hawa watoto wanasafiri peke yao ama wanaongozana na ama wazazi wao au guardians wao ?
  • Je, nani anawagharamia kwenye safari na malazi ama wanajilipia ? Kama wanagharamiwa je, ni chombo gani hicho na kinapataje pesa?
  • Kama ni chama cha siasa (CCM) hiyo inaruhusiwa kisheria hivi vikinda kujishughulisha ama kutumiwa kisiasa ?
  • Je, inakuwaje kama mtoto wa miaka kumi hakipendi chama cha baba yake na kwa mtindo huu tunawafundisha nini hawa kinda - kuwa wana tofauti na wenzao ?
  • Je lengo hapa ni kama lile la Al Qaida la kuwasokomezea itikadi tangu utotoni - adui wao hapa ni nani ?
  • Je, ni kweli kuwa CCM hawaoni hatari ya kuwapandikiza watoto wadogo hii tabia ya kubaguana ?
Mababu wa CCM, Wazazi wa CCM, wake wa CCM, Wamama wa CCM, Vijana wa CCM , Chipukizi wa CCM, Wajukuu wa CCM hadi Watukuu wa CCM - jamani tunajenga Taifa gani au ndio mwanzo wa kutanguliza maslahi ya CCM kabla ya taifa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom