Mtoto wa kigogo aliyeiba Sh15m kortini, kesi yafutwa chapchap

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,108
MSICHANA wa miaka 17 ambaye anadaiwa kumuibia baba yake mzazi Sh15 milioni, jana alifikishwa mahakamani kujibu shtaka hilo lakini muda mfupi baada ya kusomewa mashtaka, kesi yake ikafutwa.

Msichana huyo, Jane Mpapi, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Majengo iliyo mjini Moshi alifikishwa mahakamani akiwa na mwenzake Lutemba Bainganyi, 18 wakituhumiwa kumuibia Hassan Bendeyeko, ambaye ni mkuu wa Idara ya Miundombinu (AAS), katika ofisi ya mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Hata hivyo, kesi hiyo namba 281/2010 iliyofikishwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobero ilifutwa dakika chache baada ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka yao na kuyakanusha.

Mara baada ya kusomewa mashitaka hayo, wakili wa serikali, Abdalalah Chavulla aliiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo chini ya kifungu 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Kifungu hicho kinampa uwezo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuondoa shitaka lolote mahakamani, lakini chini ya kifungu hicho, DPP anao uwezo wa kuirudisha tena kesi mahakamani pindi ushahidi madhubuti unapopatikana.

Kulingana na hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo jana, wizi huo ulifanyika Mei 10 mwaka huu eneo la Shanty Town kwenye Manispaa ya Moshi.

Fedha hizo zilikuwa dola 11,000 za Kimarekani (sawa na Sh14,850,000 za kitanzania) na Sh800,000 ambazo kwa pamoja zinafanya kiasi cha pesa kilichoibwa kwa Bendeyeko kuwa Sh15,650,000 za Tanzania.

Haikuweza kufahamika mara moja kama watuhumiwa hao walirejeshwa polisi au waliachiwa moja kwa moja.

Mara tu baada ya kutokea kwa wizi huo, ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Kilimanjaro (RAS) ilitoa gari aina ya Nissan na kulijaza mafuta ili Bendeyeko alitumie kwenda Dar es salaam kuwasaka watuhumiwa hao.

Mbali na kutoa gari hilo, ofisi hiyo ilitoa masurufu ya safari kwa siku tano kwa mtumishi huyo pamoja na dereva wake, malipo ambayo baadhi ya watumishi wa ofisi ya mkoa Kilimanjaro wanadai hayakustahili.

Mtoto wa kigogo aliyeiba Sh15m kortini, kesi yafutwa chapchap
 
Tungepata ufafanuzi hizi pesa ni za serekali au za kigogo. Kama ni za serekali kwa nini zilikuwa nyumbani kwake? Au ndio maana amefuta kesi ili naye asiwemo kwenye uzembe? Na kama ni zake anaweza kuzitolea maelezo amezipataje na kwa nini ameficha nyumbani.
 
Back
Top Bottom