Mtoto wa Kawawa alia CCM inakaribia kufa

Mtoto wa Rashid Kawawa na mbunge wa CCM Zainab Kawawa amelia machozi katika kikao cha wabunge wa CCM na kusema hii siyo CCM ya baba yake aliyoijua na kwamba hii ni CCM inayoelekea kuzimu kwa vitendo vya ubadhirifu wa mawaziri wake.
Katika hali ya kushangaza wakati akiangua kilio hicho alisema vijana wote aliosoma nao na marafiki zake wanamzomea na kumshangaa kuwa CCM.
Hali hiyo ilisababisha wabunge wenzie ndani ya kikao hicho kupatwa simanzi kubwa na wengine nao walionekana wakifuta machozi.

Source:RAI
Kikao hicho kimefanyika lini na wapi?
 
Amesema vyema, CCM ya babake siyo CCM ya sasa. Yeye ni mwanasisiemu wa sasa, hivyo ana mchango kwa chama kufa pia, akimaliza kulia atafakari, kisha achukue hatua..!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mtoto wa Rashid Kawawa na mbunge wa CCM Zainab Kawawa amelia machozi katika kikao cha wabunge wa CCM na kusema hii siyo CCM ya baba yake aliyoijua na kwamba hii ni CCM inayoelekea kuzimu kwa vitendo vya ubadhirifu wa mawaziri wake.
Katika hali ya kushangaza wakati akiangua kilio hicho alisema vijana wote aliosoma nao na marafiki zake wanamzomea na kumshangaa kuwa CCM.
Hali hiyo ilisababisha wabunge wenzie ndani ya kikao hicho kupatwa simanzi kubwa na wengine nao walionekana wakifuta machozi.

Source:RAI

Mpendwa Zainabu,

Sio lazima ung'ang'anie kubaki CCM. Kumbuka hata Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alipata kusema angeweza kutoka CCM, kwani CCM sio Baba ua Mama yake!

Usibaki kukaa na wafu. Ingia katika chama kinachojali maslahi na matatizo ya wanyonge.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Msanii tu huyo analia nini kwanza atuambie yeye amepataje huo ubunge wa viti maalum. Vile vile aje atueleze alipataje kazi pale PSPF wakati ana division 0 . CCM wote wasanii tu inasikitisha ndio maana akina SAS, Butiku, Kitine na Warioba waliamua kukaa pembeni wakijitazamia tu.
 
Angekuwa na uchungu na chama cha magamba angekataa kufutwa machozi ya kufiwa na baba yake kwa kupewa ubunge,
 
Zainab ameolewa?

Kama bado najitolea kwenda kumfuta machozi!
 
Hon. Filikunjombe, mfundishe zaina jinsi ya kusaini kuiokoa CCM, machozi hayasaidii. Kuwajibisha mafisadi ndio njia pekee yakuleta kanafuu kadoooooooooogo kwa magamba.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa hali hii, Mwisho Bashe atafanikisha mpango wake wa kuiangusha CCM ili waheshimiane.
 
kwani amefungishiwa ndoa na ccm kama siasa ni hiari ya mtu basi hana haja ya kufanya yote hayo ni yeye kuamka na maamuzi magumu tu.
Usitafute huruma kwa magamba hawatafanya hivyo timua mbiyo kama umeshtuka usingizini.

Umesahau kuwa ni KITU MAALUMU huyu!
kaka yake ndie wa jimbo la NANTUMBO.
 
duh hii kali kumbe kale kaugonjwa kapm ka kulialia bungeni amewaambikuza hta wenzake wa magamba inafurahisha pm analia na wabunge wake wanalia hii c sanaa tu,mm namuona kma mnafiki na mchumia tumbo tu huyo dada hv anajua idadi ya kina mama wanakosa huduma za msingi wanapotaka kujifungua kwenye mahospitali yetu kisa tu ni hao magamba?
 
Analilia nini sasa Huyo Mnafiki!! Akiulizwa anacholilia Hajui!! Chakula ameachiwa mezani sasa analialia nini?
 
mnafiki mkubwa kwani ccm ilimtolea posa mpaka ashindwe kutoka huko? walele sasa hicho ni chama cha machozi na unafiki na magamba!
 
Kilichokuwa kinamliza wala siyo ccm kufa ila ni baada ya kusoma SMS iliyokuwa inasema "aise lile deal letu limekufa waziri kakataa kusaini kutokana na bunge chini ya CDM kuchachamaa kuhusu ufisadi" akaanza kulia Huku akijifanya ccm Inakufa M4C kamata mijizi tafadhali !!!!!!!!!!!!!!
 
Siasa ni usanii uliopitiliza kama mbunge analia je sisi tulioteswa na kupigika kwenye huu mfumo wa kifisadi tufanyeje?
 
kama anataka kuingia mbinguni basi atoke ccm. ccm hii ya leo ni sura mbili, inauma na kupuliza kama panya

Back
Top Bottom