Mtoto wa Amin amfagilia Nyerere

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Mtoto wa Amin amfagilia Nyerere

Thursday, 09 April 2009 16:29

Na Werema Wikori, Butiama

Majira

ENEO la Mwitongo jana lilikumbusha mauaji ya Vita ya Kagera na kifo cha Mwalimu Nyerere, baada ya mtoto wa Rais wa zamani wa Uganda, Idd Amin, Bw. Jaffer Amin kuwasili kijijini hapa na kukumbatiana na Bw. Makongoro Nyerere mbele ya lango kuu la nyumba ya Mwalimu.

Hali hiyo iliwafanya baadhi ya wakazi wa Butiama akiwemo kulengwa na machozi, hivyo kuashiria jambo juu ya ujio wa mtoto huyo wa Amini akiwa ni wa tatu wa kiume katika familia ya watoto 60 wa mtawala huyo wa zamani wa Uganda.

Akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wananchi waliojitokeza kumpokea katika maadhimisho hayo ya miaka 30 ya Vita ya Kagera, Bw. Jaffer alisema Afrika ina kila sababu ya kujivunia kumpata kiongozi kama Mwalimu Nyerere.

Bw. Jaffer alisema Mwalimu Nyerere alijenga Tanzania ya umoja, mshikamano na maelewano hatua ambayo sasa inawatambulisha kwa lugha moja ya Kiswahili tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika.

"Ni ukweli usiopingika Mwalimu Nyerere alijenga umoja na kufanya sehemu zote nilizopita kuja hadi hapa Mwitongo kupokelewa vizuri tofauti na baadhi ya watu walivyofikiri," alisema.


Kwa sababu hiyo alisema safari yake kwa mtu aliyemng'oa Baba yake madarakani ni muhimu katika historia kuanza ukurasa mpya na kusahau yote yaliyopita na kujenga mshikamano wa dhati kwa wao, familia, mataifa hayo mawili na Afrika nzima kuacha kulipizana visasi.

Kwa upande wa mtoto wa Nyerere, Bw. Madaraka alisema jambo hilo liliandaliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwa kuwakutanisha kwa pamoja ili kuadhimisha miaka hiyo 30 tangu Vita ya Kagera, limejenga nia ya dhati ya umoja na kufanya sasa vizazi kusahau yaliyotekea wakati huo.

Alisema kutokana na kitendo hicho aliitaka jamii kwa nchi hizi mbili kuangalia upya historia kuwa zimetoka wapi na sasa zinakwenda wapi na kwanini zilifika hapo kwa kupanga maisha mazuri baada ya kuteleza wakati huo.

"Pamoja sasa Tanzania na Uganda ni wamoja. Lakini jambo hili limeongeza nguvu katika uhusiano uliopo na kuzidisha na kuweka nia njema kwa nchi zetu. Nawashukuru sana BBC kwa hatua hii," alisema Bw. Madaraka.

Mtoto wa Amin baada ya kuwasili alipelekwa moja kwa moja katika kaburi la Mwalimu Nyerere ambapo aliweka shada la maua na kushiriki ibada fupi ya dini za Kikristo na Kiislamu.
 
Huyu Jaffar asije kuwa anataka kugombea kitu huko UG....stay tuned.
 
Watoto wa Nyerere wanatia huruma masikini duniani hawapo ahera hawapo.

SAHIBA.
 
Huyu Jaffar naona anajianda kugombea urais huku kwao ndo maana akatangulia Butiama kupata Baraka za Mzimu wa Nyerere. Hakuna raisi yeyote Uganda anayeweza kukaa madarakani bila ridhaa ya Mwalimu
 
Huyu Jaffar naona anajianda kugombea urais huku kwao ndo maana akatangulia Butiama kupata Baraka za Mzimu wa Nyerere. Hakuna raisi yeyote Uganda anayeweza kukaa madarakani bila ridhaa ya Mwalimu

Na tayari ameanza kupata baraka za BBC stay tuned...
 
Huruma kwa maana gani? mbona maisha yao mazuri tu!

Watanzania bwana, sijui mtu anategemea wawe mafisadi?
 
huyu bwana tayari keshaandaliwa na watu wa west, wazungu wameshamchoka Mu7, kupitia kwa mwalimu ilikuwa ni kigezo tu lakini inawezekana keshakuwa na jeshi hapa tanzania linafanya mazoezi sidhani kama kutakuwa na tofauti na yale ya kabila, tusubiri tuone
 
some of the comments here are pathetic, imagine mtu anasema watoto wa Bush na Saddam wakutanishwe - ili iweje? after all, circumstances za vita vya Kagera ni tofauti kabisa na Iraq.

wengi wetu hatujaelewa umhimu wa tukio hilo, kama kawaida yetu tutakuja kubaini miaka mitano baadaye. their meeting had all the necessary blessings you could ask for, it was a success and that was it.

tatizo letu watanzania, tunapenda kupuuza vitu bila kupima uzito wake. kazi yetu kukatishana tamaa wenyewe kwa wenyewe. lakini yale mazito yanayotukabili, yanatushinda.

nadhani vijana wenzangu tumeishiwa ideas, siyo lazima kutoa comment kwa kila post iliyopo hapa nyingine tuziache zipite tu. hatuwezi kuwa hodari kwa kila kitu, those guys Madaraka na Jaffar, are brighter than some of us. they are even courageous, ujasiri wetu uko wapi? kupiga porojo behind the veil of anonymity?
 
Last edited:
..vita ile haikuwa baina ya familia ya Amini na Nyerere, bali mataifa ya Uganda na Tanzania.

..ingekuwa na maana zaidi kama Makamanda na wapiganaji walioshiriki vita ile toka pande zote mbili wakakutanishwa.

..kwa mtindo huu ina maana watoto wa Mwalimu nao watatembelea kijiji cha Koboko alikozikwa Iddi Amini?
 
Comments made in light banter should not be taken with all seriousness.

After all it is the end of the week.

Je, aliomba msamaha kwa niaba ya baba yake?
 
Hivi Maiti (watu walio kufa), wanaweza vipi kuathiri maisha ya walio Hai...!?

Huu ndio "ushirikina" tunaoukataza lakini baadhi yetu "hawasikii". Eti kufagia kaburi la Nyerere ili kupata 'baraka zake'! Hakuzitoa hizo baraka zake angali hai atawezaje yu mauti??

Kweli pana kazi kusambaza da'awah .....
 
Nani aombe msamaha kwa nani?

Mtoto wa Amin awaombe msamaha wahanga wa vita kwa maovu ya baba yake.

Kama papa ameweza kuomba msamaha kwa maovu ya mapapa waliopita sioni kwa nini hili lisiweze kutokea, najua kuna watu watasema ataombaje msamaha kwa maovu ambayo hakuyatenda, the operating part should be kwa niaba ya baba yake.Just recognizing kwamba baba yake alichofanya ni kibaya will put things in perspective.Haya mambo ya kumsifia Nyerere si tabu, tunajua kwamba Nyerere was the shizniz katika kutuweka pamoja and all that.

Je anajua kwamba baba yake aliua watu wengi Tanzania?

Je anajua kwamba baba yake aliingiza Tanzania katika vita iliyoigharimu Tanzania mengi?

Je anaweza kukubali kwamba at the very least baba yake alifanya makosa?

Je anaweza kuchukua fursa hii kuwaomba radhi watanzania kwa niaba ya baba yake kwa makosa hayo?
 
BBC waandae kitu kama hicho kwa mabinti wa Bush na wa Sadam!..
Hii haitakuwa balanced kwa sababu upande mmoja ulimpoteza mzazi wakati upande mwingine ukiendelea kula nchi kwa miaka kumi ijayo. Itabidi wasubiri hadi wazazi wote watakapokuwa wameshafariki kama ilivyokuwa kwa Amin na Nyerere.
 
Back
Top Bottom