Mtoto na Baba waoa nyumba moja - Matatizo katika familia

Elisha Ray

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
323
94
Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo. Mmoja
aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake akasema "

Unadhani familia yako ina matatizo?"
Basi sikiliza kisa hiki.

"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti
mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa
kambo hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba
yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe
wa mkwe wake.

Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa
kiume. mtoto huyo wa kiume alikua ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba
mmoja. Lakini kwa vile alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu papo hapo
akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu.

Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto
wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa
kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia
baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande
wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama
yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe.
Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu
mwenyewe.

SWALI.
Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika
 
Back
Top Bottom