Mtoto mbaroni kwa kuua

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKAZI wa kijiji cha Madangwa wilayani Lindi vijijini, Somoe Ali ameuawa kwa kupigwa jiwe na mtoto wa umri miaka 12, Hamis Hassani.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Sifuel Shirima alisema jana kuwa Ali alipigwa sehemu ya tumbo na kusababisha bandama kupasuka ndani ya tumbo lake.

Alisema mtoto huyo alimpiga Ali jana jioni saa 12 na ilipofika saa moja usiku alipoteza maisha akiwa nyumbani kwake, wakati wa Sikukuu ya Krismasi.

Awali mtoto Hassani alimpiga mtoto wa Ali mwenye umri miaka 6 Idi Ali wakati walipokuwa wanacheza mpira.

Kamanda Shirima alisema baada ya hapo, Ali alikwenda kumshitaki mtoto huyo kwa bibi yake wakati Hassani akiwa amejificha kwenye kichaka na wakati anarudi ndipo alimrushia jiwe sehemu ya tumboni.

Shirima alisema marehemu alikwenda nyumbani na alipoteza maisha kutokana maumivu aliyoyapata ya kupigwa na jiwe.

Alisema wasamaria wema walimchukuwa hadi kwenye hospitali kwa uchunguzi na kubaini bandama lilipasuka ndani ya tumbo na kusababisha kifo.

Kijana huyo Hassani yuko kituo cha Polisi akisubiri kwenda mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili
 
Back
Top Bottom