Mtoto kunyonya vidole vyake

kama ukipaka pilipili kwenye kidole inakuaje?

Kama mtoto bado ni mdogo sana hili la kupaka pilipili silishauri hata kidogo na pia mtoto kama ana akili zake anaweza kukiosha (kwa siri) na kuendelea na burudani yake.
 
pole sana,

hizo dalili kwa kawaida huwapata watoto wadogo, na kitabibu tunaambiwa mtoto anaanza kunyonya kidole tangu akiwa na miezi 7 akiwa tumboni, hivyo usiogope ni hali ya kawaida kwa mtoto pia kama hupendi anyonye vidole unaweza pia ukamnunulia baby sweeter ili asiwe ananyonya vidole,

kuhusu kuwasha kwa fizi pia inawezekana ingawa inaweze isiwe zinawasha ila ni hali yakawaida ya mtoto kunyonya vidole vyake, na wala haina uhusiano wa kuharibu kuota kwa meno ya mtoto, ni maneno tu ya mitaani kwa wakina mama...

Bliss mpendwa, hapo kwenye red unamaanisha dummies?au ni kitu kingine hiki?kama ni hizo, basi
kwa ufahamu wangu na maelezo niliyopewa na midwives pale nilipojifungua
ni afadhali mtoto anyonye vidole (ingawaje pia si vizuri) kuliko kumpa anyonye hizo dummies, hizo zinaharibu meno more than atakavyonyonya vidole.so ningependa kukushauri mtoa mada fanya juu chini mtoto aache kunyonya kidole ILA usimpe dummies kunyonya kama alternative.

nawasilisha
 
Wangu pia anatatizo hilo lakini nilitaka kujua tatizo hilo linasababishwa na nini hasa?
 
hata mimi babu ananyonyaga vidole tumekaa kikao cha ukoo tumekubaliana akilaa tu tumpake pilipili kichaa kwenye vidole hadi vya miguuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom