Mtoto kunyonya vidole vyake

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,726
312
Hi wana JF,

Nina mtoto wa miezi mitatu bado hajaota meno ila wiki mbili zilizo pita ameanza tabia ya kunyonya vidole vyake sijajua kama ni meno yanataka kumuota sasa yanawasha au ni nini? pia kuna baadhi ya watu wameniambia mtoto akinyonya vidole meno yakiota yatatoka nje hivyo yataharibu shape ya reception ukizingatia mtoto mwenyewe wa kike.

JF members ushauri please
 
pole sana,

hizo dalili kwa kawaida huwapata watoto wadogo, na kitabibu tunaambiwa mtoto anaanza kunyonya kidole tangu akiwa na miezi 7 akiwa tumboni, hivyo usiogope ni hali ya kawaida kwa mtoto pia kama hupendi anyonye vidole unaweza pia ukamnunulia baby sweeter ili asiwe ananyonya vidole,

kuhusu kuwasha kwa fizi pia inawezekana ingawa inaweze isiwe zinawasha ila ni hali yakawaida ya mtoto kunyonya vidole vyake, na wala haina uhusiano wa kuharibu kuota kwa meno ya mtoto, ni maneno tu ya mitaani kwa wakina mama...
 
Hilo la mtoto kunyonya kidole na kuharibu meno yake ni kweli kabisa, lakini kwa sasa mtoto wako ni mchanga mno kuanza kuwa na wasiwasi wa hilo. Ila unaweza kujaribu kumuondoa kidole hicho kila anapokinyonya ili asijenge uzoefu wa kufanya hivyo katika siku za usoni.
 
Asante
 
Baada ya muda gani?
 
Mtafutie pacifier itamsaidia kuacha kunyonya vidole, ila mzingatie usafi la sivyo mtoto ataharisha kama hiyi pacifier haitakuwa kwenye usafi.
 
Wamekudanganya.
Kuna mdogo wangu wa kike alikuwa ananyonya vidole hadi yupo sekondari.
Sahv yupo chuo akiwa chuo akinyonya vidole wenzie wanamtania kwahiyo anaacha ila akirudi nyumbani kazi ile ile.

Reception yake haijaharibika, tena ni mrembo kuliko mimi dada yake. Huyo mwanao akinyonya uwe unamtoa ingawa huyu mdogo wangu tulikuwa tunamtoa tangu mtoto ikafikia kipindi tukachoka maana alikuwa hana dalili za kuacha.
 
Mtoa maada mimi pia pamoja na ndugu zangu kama 4 ni wahathirika wa kunyonya vidole. Do whatever you can to stop your kid. Meno hayawezi kukutana kama mtu ananyonya kidole. Yaani mimi nikikuangalia naweza kukwambia ulikuwa unanyonya kidole utotoni. Dada yangu imembidi atumie ela nyingi sana kutengeneza meno yake ya mbele kwani yeye alikuwa ananyonya kidole gumba hivyo meno yake yalianza kulegea alipofika 35 year (kidole gumba kina madhara zaidi).

Mwanagu nae alianza kunyonya kidole, kila tukienda clinic manesi wananisema kuwa itanigharimu kutengeneza meno yake akikua. Tukafanya mkakati na mume wangu tukamfunga plaster akiwa na mwaka mmoja. It worked kwani alikuwa hana akili ya kujifungua. Ukisubili akawa na akili hatahacha kamwe. Mimi wazazi walianza kunifunga plaster nikiwa na akili. Wakifunga kidole hiki nahamia kingine mpaka walichoka. Now I am blaming them they should have stopped me while I was real young. Wazazi wengi wanahacha watoto wanyonye vidole kwa sababu wanasema mtoto anaenyonya kidole alii ovyo. I am telling you do whatever you can to stop your kid.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni kweli kabisa wewe jaribu kuuliza mtu ambae meno yake hayakutani kama alinyonya kidole utotoni. Na kingine atakuwa anataniwa na wenzake, ingwawa mimi nilikuwa don't care fulani na nilikuwa naendelea kuwaburuza watu darasani. Ila watoto wengine wakiwa bulled wanakuwa wajinga na wanakosa confidence

si kuhasibika inasemekana meno ya juu hasa ya mlangoni hutoka nje kama ngiri
 
kama ukipaka pilipili kwenye kidole inakuaje?

Usimpake mtoto pili pili huo ni ukatili dhidi ya mtoto. Kama ni one year or below plaster inatosha. Nunu za kutosha ili umbadili mara kwa mara kwani zinachafuka. In a week atakuwa amesahau
 
Nimejifunza kupitia post yako,mimi nilijua hakuna madhara maana mimi nilinyonya mpaka niko form 6 na dental formula yangu iko poa tu.
 
Mtoa maada mimi pia pamoja na ndugu zangu kama 4 ni wahathirika wa kunyonya vidole. Do whatever you can to stop your kid. Meno hayawezi kukutana kama mtu ananyonya kidole. Yaani mimi nikikuangalia naweza kukwambia ulikuwa unanyonya kidole utotoni. Dada yangu imembidi atumie ela nyingi sana kutengeneza meno yake ya mbele kwani yeye alikuwa ananyonya kidole gumba hivyo meno yake yalianza kulegea alipofika 35 year (kidole gumba kina madhara zaidi).

Mwanagu nae alianza kunyonya kidole, kila tukienda clinic manesi wananisema kuwa itanigharimu kutengeneza meno yake akikua. Tukafanya mkakati na mume wangu tukamfunga plaster akiwa na mwaka mmoja. It worked kwani alikuwa hana akili ya kujifungua. Ukisubili akawa na akili hatahacha kamwe. Mimi wazazi walianza kunifunga plaster nikiwa na akili. Wakifunga kidole hiki nahamia kingine mpaka walichoka. Now I am blaming them they should have stopped me while I was real young. Wazazi wengi wanahacha watoto wanyonye vidole kwa sababu wanasema mtoto anaenyonya kidole alii ovyo. I am telling you do whatever you can to stop your kid.

Asante kutujuza ,sikuwa najua kama kuna madhara.nimejifunza jema hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom