Mtoto huyu anaitaji msaada wetu wa hali na mali

Feb 15, 2009
99
2
WADAU TUMSAIDIE MTOTO TUNTUFYE..

Mtoto Tumtufye Mwakasaka (8) ambaye kwa sasa amekatisha shule na kuja Iringa mjini kutafuta wasamaria wema kwa ajili ya kunusuru maisha yake baada ya mwili wake kuvimba mithiri ya pipa.

Anaomba wabongo na wadau wote pamoja na Rais Jakaya Kikwete kusaidia kunusuru uhai wa mtoto huyo.









Mtoto huyo ambaye anahitaji msaada wa fedha zaidi ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya kwenda nchini India kutibiwa kwa sasa anaishi katika eneo la Bwawani kihesa kilolo katika Manispaa ya Iringa huku akiendelea kutabika baada ya mwili wake kutokwa na malenge lenge sehemu za siri na maeneo mengine huku akiendelea kuvimba mwili kutokana na maradhi ya figo yanayomsumbua.
Kwa mujibu wa mwanablog Fransis Godwin.



tembelea pia Bongo Pix kwa habari zaidi
 
jani tusishie kwenye maafa tu tumsaidie mtoto wetu huyu jamani wapi mamaa pearl
 
Ndugu wadau, nachukua fursa hii, kuwajulisha na kuwashukuru kwa mchango wenu wa kuandika juu ya mtoto Tuntufye Julius Mwakasaka.

Nikiwa kama mjomba wa Tuntufye na ambae nimeishi nae tangu kuzaliwa kwake, nawiwa kusema kua Tuntufye Julius Mwakasaka alitutoka tarehe 17 mwezi wa Pili 2010 kule KCMC Moshi ambapo alipelekwa baada ya kupewa refferal toka Hospitali ya wilaya ya Lushoto.

Mazishi yalifanyika Lushoto- Kialilo kwa bibi yake mzaa mama; Mwalimu Esther Mshana na baadae kilio kupelekwa Mbeya.

Tulimpenda sana, alikuwa Mcheshi na mtundu sana, alikuwa rafiki wa wote ( si kwa unafiki bali kwa hali halisi) Mchokozi ili kutafuta maana na urafiki lakini pia mpole kwa mambo ambayo alikose kama Mtoto. Ninampenda kwa Binasfi yangu.

Ameacha vilio na simanzi kwa wote ZAIDI AMEWAACHIA UPWEKE Ndugu zake; Tunosye na Alice. Nakumbuka sana maneno aliyoandika Tunosye ( 10) kwenye chumba chao wakati mdogo wake huyu anaumwa, maneno haya ambayo yalikuwa faraja kwangu na kwao yalisomeka hivi : TUNTUFYE IS OUR HERO huku mengine yakisomeka kwa kifupi tu Surprise pengine waliamini baada ya ndugu yao kuzunguka na kuhangaika huku na kule angerudi na kucheza nao na pengine kwao ingekuwa kama Surprise!!

Nawapenda wote sana na MUNGU AWABARIKI
 
Back
Top Bottom