Mtoto Azaliwa Akiwa Tayari Ameishaota Meno

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Kwa kawaida mtoto mchanga huanza kuota jino lake la kwanza anapofikisha umri wa kati ya miezi sita na mwaka mmoja, hali ni tofauti kwa mtoto mmoja wa nchini Uingereza ambaye amewashangaza watu kutokana na meno yake aliyozaliwa nayo.
Mtoto mchanga wa kiume aliyezaliwa nchini Uingereza amekuwa maarufu ghafla kutokana na meno aliyozaliwa nayo.

Kwa kawaida huchukua zaidi ya miezi sita kwa mtoto kuanza kuota jino lake la kwanza, lakini mtoto Oliver James amezaliwa akiwa na meno mawili ya mbele yaliyokamilika.

Wazazi wake, Joanne Jones, 31, na Lee, 32, wanasema kuwa tayari wameishamuandalia tarehe mtoto Oliver kwenda kuonana na daktari wa meno.

Madaktari wa meno wanasema kuwa meno ya mtoto huyo huenda yakang'oka yenyewe kama meno yake ya utoto au yakaendelea kuwepo kama meno yake ya mwanzo ya ukubwani.

Mama wa mtoto huyo mkazi wa Haverhill, Cambridgeshire alisema kuwa wamekuwa wakitembelewa na marafiki wengi na ndugu na jamaa ambao wanataka kujionea meno ya mtoto huyo.

"Oliver ni mtoto mwenye afya njema, tulishangazwa sana kuyaona meno yake, haya si meno yanayoanza kuchipukia, ni meno yaliyokamilika", alisema mama wa mtoto huyo.

"Si kawaida watoto kuzaliwa wakiwa na meno lakini hali ni tofauti kwa Oliver", alimalizia kusema mama wa mtoto huyo.
 
Kwa mila zingine wanasema ni uchuro mtoto kuzaliwa na meno , Na hawa mila zao zinasemaje?
 
Kwa mila zingine wanasema ni uchuro mtoto kuzaliwa na meno , Na hawa mila zao zinasemaje?
Kwa maisha ya sasa inawezekana kutokana na aina za vyakula na chemicals zinazotumika pia nadhani ni masuala ya kimaumbile yanaweza kuwa cause!hasa kwa baba na mama nakumbuka kuna mtoto aliwahi zaliwa na mabaka mwili mzima kumbe tatizo lilikua ni mama yake alitaka kutoa ile mimba!baadae ikashindikana so impact za dawa alizokunywa zikawa tatizo kwa kiumbe kilichozaliwa
 
Back
Top Bottom