Mtoto apendi kula, je mbinu gani itumike apende kula?

Mpe maziwa, wangu ana miaka 4 anashindia maziwa, madr wameangaika mpaka wamegive up.
 
Pole sn, hata mm nina mtoto wa umri huo kula ni mtihani, na kuna jamaa yang pia mwanae ni same age na wang, hawataki kula kabisa, tena ni wakiume, ni kunyonya tuu na kula samaki mwanzo mwisho, cha kushukuru uzito unapanda vzur tuu kila mwezi, karibu kumpa samaki wa kuchemsha tuu.
 
Chunguza chakula akipendacho, ukishajua tumia hicho chakula kupenyeza vyakula vingine vyenye virutubisho tofauti bila yeye kujua

mfano anapenda samaki, mpike kwa maziwa badala ya maji, kaanga wali uweke ndani ya samaki

tafuta mtoto wa rika lake, mjanja na anayependa kula muwekee chakula pamoja naye!!
Wadau wataongeza

Bango
 
Duh, kumbe kweli ni tatizo aisee, wa kwangu muda wa kula ni ugonvi yaani karibu mtaa mzima ujue maana natumia nguvu kumlisha na mpaka sasa mtoto anapenda samaki na juice tu! Ushauri wa kitaalamu nilioelezwa haujanisaidia ingawa najitahidi kuutekeleza, Mama yangu kanisisitiza niendelee kumlazimisha vinginevyo itakula kwangu!
Kuna mdau kasema wa kwake pia anapenda samaki tu, najiuliza inakuwaje maana hata kwa kwangu kwa samaki hakuna haja ya kumlazimisha japo samaki wa dar siwapendi kweli! Mara tunaambiwa wana sumu yaani utatautata tu! Wenye uzoefu zaidi karibuni kwa ushauri zaidi!
 
Ni mtoto wa kiume, ndio anatimiza mwaka mmoja. Hapendi kula, licha ya kumbadilishia chakula mara kwa mara. Mama yake humlazimisha kula angalao vijiko viwili.
mtengenezee juisi ya ukwaju au limau mnyweshe saa 1 kabla ya kula chakula.mpunguzie vyakula vyenye mafuta.mengi pia penda kumpa mboga mboga zitamfanya apende kula kwani atahisi njaa na kumfanya apate hamu ya chakula.
 
mtengenezee juisi ya ukwaju au limau mnyweshe saa 1 kabla ya kula chakula.mpunguzie vyakula vyenye mafuta.mengi pia penda kumpa mboga mboga zitamfanya apende kula kwani atahisi njaa na kumfanya apate hamu ya chakula.
Ni msaada kwa mtoto,hakikisha mtoto humkimbizii ugali mgumu na wali.Hao wanahitaji vyakula laini na matunda/juice za matunda.Samaki mchemsho,na kama mnaunga isiwe mafuta mengi,uji ule wa asili wakutengeneza wewe mwenyewe.Kuna mambo mengi sana juu ya watoto.
 
Wa kwangu pia hapendi kula 2yrs na wakati unamlazimisha kula hua anasinzia na kulala kabisa ila ukiacha kumpa anaamka na kuanza kucheza
kwa hali hii napata ushawishi kufungua high quality children daycare center,ili watoto walelewe na wakuzwe katika misingi sahihi ya malezi na makuzi
 
Tatizo nahisi kwa watoto wa kiume zaidi kuliko wa kike.
Wanapenda samaki na juice wachache mboga za majani.
Njia ya kwanza km inawezekana wakat wa kula utafute watoto awe anakula nao karibu.
Njia ya pili kupunguza vyakula vyenye mafuta
NB: WATOTO WA UMRI HUO WANAHITAJI .mUDA MREFU KUBEMBELEZANA NA WAZAZi wa SIKU HIZI HAWANA MUDA MREFU WA KUBEMBELEza watoto hasa ukizingatia dunia ya utandawazi na kutegemea mdada wa nyumbani.kitu muhimu hasa kucheza nae then unampa kidogo kidogo pale anapokubali.ZA
 
Ni mtoto wa kiume, ndio anatimiza mwaka mmoja. Hapendi kula, licha ya kumbadilishia chakula mara kwa mara. Mama yake humlazimisha kula angalao vijiko viwili.
Ulianza kumpa chakula akiwa n miez mingapi?jaribu kutokumpa vyakula vya sukar.uji wekea karanga midogo zilizosagwa wek chumvi.Watot weng wanapenda ladha ya chumvi
 
Back
Top Bottom