Mtoto Aogopa Majini Hospitali ya Mwanyamala

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MTOTO Simon Kombo [10] mkazi wa Mwananyamala Kisiwani amewagomea walezi wake kwenda kupata matibabu katika hospital ya Mwananyamala kwa kile alichodai kuogopa majini yaliyopo katika hospitali hiyo.
Kombo aligoma jana baada ya kujeruhiwa mguu wakati alipokuwa akicheza na watoto wenzake na walezi walitaka kumpeleka hospitalini hapo kwa matibabu.

Hata hivyo mtoto huyo alitoa tahadhari kwa walezi hao kuwa wasimpeleke katika hospitali hiyo kwa kuwa kama wangempeleka hapo huenda atapoteza uhai wake na walezi kuduwaa na kauli ya mtoto huyo.

Walipoendelea kumuuliza ni kwa nini alijibu ”msinipeleke nimeshawaambia, mimi naogopa majini yaliyowekwa pale si mnaona kila siku watu wanakufa pale na matukio ya ajabu ajabu”

Hata hivyo kutokana na kauli za mtoto huyo walezi hao waliogopa kumpekeka hapo kwa kuogopa kauli za mtoto huyo na walijipanga na kumpeleka hospitali binafsi kwa matibabu.
 
Back
Top Bottom